Kupetuka Mipaka katika Mahari na Athari zake

Kuna tatizo la kijamii nchini India hasa katika eneo la Milibar, eneo hili linawasichana wengi wa Kiislamu ambao hawakuolewa, kwa sababu ya mahari kuwa juu. Muulizaji anaomba kuwekewa wazi hukumu ya sharia katika hilo?

Soma zaidi....

Mipaka ya Miamala kati ya Wanadoa kabla ya Harusi

Naomba kufahamu kwa ujuzi na maarifa yenu ambayo tunayafuata kwa kuwa sisi si wajuzi wa baadhi ya mambo, hivyo tunaomba ushauri kwa wenye elimu na maarifa, ili tufanye mambo kwa mujibu wa Fatwa zenu katika mambo hayo:

Mimi ni kijana mwenye umri wa kiaka ishirini nane, nimeoa miezi mitano iliyopita lakini sijamuingilia mke wangu, kutokana na hali anayopitia kijana kwa zama zetu, baadhi ya rafiki zangu wameniambia kwamba huyo anazingatiwa kuwa ni mke wangu, na ninaweza fanya nae tendo la ndoa muda wa kuwa tumeshafunga ndoa mbele ya ndugu na jamaa, japo sina haki ya hilo. Nataka kujua ni upi ukomo wa mahusiano yetu ya mke na mume?

Soma zaidi....

Hukumu ya Ndoa ya Misyaar (Ndoa ya Mwanamke kukubali kuacha baadhi ya haki zake)

Tunatarajia kutoka kwenu wanazuoni waheshimiwa kutuelezea maana ya Ndoa ya Misiyaar, na mtubainishe hukumu yao?

Soma zaidi....

Ndoa ya Mwanamke Aliyejitolea

Hivi karibuni kupitia baadhi ya vituo vya runinga kuna mtu amejitokeza na kutangaza kile kinachoitwa “Ndoa ya Mwanamke aliyejitolea” na anasema: Ndoa hii inakamilika ikiwa mwanamke atasema kumwambia mwanamume: “Nimejimilikisha kwako mimi mwenyewe”, kisha mwanamume akamjibu: “Na mimi nimekubali, na nitakuandikia uhuru kwa kusoma Surat Al-Ikhlas kwa - mfano - itakuwa ni thamani ya uhuru wako”. Kisha akasema huyu mtu: Hakika mwanamke kwa maneno haya anakuwa ni mtumwa kwa huyu mwanamume, hivyo anaweza kuishi naye maisha ya ndoa, na kuwa na uwezo mwanamke wa kuimaliza ndoa hii au utumwa huu kwa kusoma Surat Al-Ikhlas kwa nia ya kutengana, basi atakuwa huru kwa mara nyingine,

Huyu mtu anajaribu kuyaunga mkono maneno yake kwa kutumia kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wanne. na mkiogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana} [AN-NISAA, 03].

Pamoja na kauli ya Mola Mtukufu: {Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake wa kiungwana Waumini, na aoe katika vijakazi Waumini iliyowamiliki mikono yenu ya kulia. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa imani yenu. Nyinyi mmetokana wenyewe kwa wenyewe. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao, na wapeni mahari yao kama ada, wawe wanawake wema, si makahaba wala si mahawara} [An-Nisaa, 25].

Na kuwa Mtume S.A.W. alijiwa na mwanamke mmoja na kujitoa yeye mwenyewe mwanamke kutaka kuolewa na Mtume - na wala hakusema nimejioza kwako mimi mwenyewe - basi baadhi ya Masahaba walitaka kumwoa, akamwambia: “Nimekumilikisha kutokana na Qur`ani uliyonayo” anasema: Hakika hii ni dalili ya uhalali wa kuoa mwanamke aliyejitoa kama zawadi yeye mwenyewe kwa mwanamume, na anasema: Hakika makubaliano ya kimataifa ya kuondoa utumwa hayazingatiwi ni jambo la lazima kutekelezwa na Waislamu katika kuharamisha kilichohalalishwa na Mwenyezi Mungu, na anasema pia: Hakika hizi ni jitihada zake ambazo haipaswi kwa yeyote kuzizuia, hivyo tunatarajia uwazi na ukweli wa madai haya kwa upande wa kisharia.

Soma zaidi....

Hukumu ya ndoa ya kimila za utotoni

Ni ipi hukumu ya kisheria ya ndoa za kimila za utotoni?

Soma zaidi....

Ughali wa mahari na athari zake

Ni ipi hukumu ya Kisharia katika ughali wa mahari na athari zake?

Soma zaidi....

Ndoa ya Misyaar

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Soma zaidi....