Hukumu ya kumdai Mume Vitu vya Nyum...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kumdai Mume Vitu vya Nyumbani (orodha ya samani) Atakapo jivua (Khul’u, ) na Matunzo ya Mke Muasi

Question

Ni ipi hukumu ya gharama za Matumizi na matunzo kwa mke Muasi? Na ipi hukumu ya kumdai mume dhahabu na vitu vya nyumbani Atakapo jivua (Khul’u, )?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Fatwa inayotumika – na ambayo inatekelezwa katika mahakama za Misri – ni kwamba mwanamke anayejitoa katika ndoa kwa njia ya khul'u anatakiwa kumrudishia mumewe mahari aliyompa, na pia na kusamehe haki zake za kifedha za kisharia ikiwa mahakama itamhukumia talaka ya khul'u. Hii imechukuliwa kutoka kwa baadhi ya maoni ya Wanazuoni wa Fiqhi kuhusu suala hili, kwa lengo la kupunguza mzigo wa kifedha unaomwelemea mume kwa sababu ya talaka ambayo haikutokana na uamuzi wake.

 

Kuhusu haki za kifedha za kisharia ambazo mke anasamehe anapoomba khul’u', kama ilivyotajwa katika kifungu cha 20 cha Sheria Namba 1 ya mwaka 2000, kilichosema:
"Wanandoa wanaweza kukubaliana kwa hiari yao juu ya khul’u'. Ikiwa hawatakubaliana, na mke akaanzisha kesi na kuikomboa nafsi yake kwa kujitoa katika ndoa kwa njia ya khul’u', kwa kujiondoa katika haki zake zote za kifedha za kisharia na kumrudishia mume mahari aliyompa, basi mahakama itamhukumia talaka hiyo." Haki hizo zinazodondoka ni pamoja na: Mahari yote (ya awali na ya baadaye), ambayo ni malipo yaliyolipwa kwa ajili ya ndoa na ridhaa ya kimwili; matumizi ya starehe (Mut‘aah) – hulazimika kwa talaka za kawaida, lakini haistahiki katika khul’u', matumizi ya eda – pia huondoka kwa khul'u; kwa kuwa lengo la watunga sheria katika kuweka sheria ya khul’u ni kumrahisishia mwanamke kuondoka kwenye ndoa ambayo hawezi kuendelea nayo, bila kumweka mume katika mzigo mkubwa wa kifedha usio wa lazima; hata hivyo, haki zinazodondoka kwa khul'u hazijumuishi; haki ya mwanamke ya kulea watoto (Hadhana), haki za watoto walioko chini ya uangalizi wa mama yao. Mtunga sheria wa Misri, katika kuchukua kwake hukumu za khul'u kutoka katika Fiqhi ya Kiislamu, alilenga kuleta usawa kati ya mwanamume na mwanamke, kwa kuweka kikomo cha fidia ya khul'u – baada ya kuwa huru kabisa katika maoni ya Wanazuoni – kwa kuizuia fidia hiyo ishughulikie tu haki za kifedha zilizothibitishwa kwa mkataba wa ndoa. Hii ilikuwa kwa ajili ya: kumlinda mwanamke dhidi ya unyonyaji wa mume, kuepusha kubatilika kwa khul'u kwa sababu ya kutoainishwa kwa fidia, na kufunga mlango kwa wake kutumia khul'u kama njia ya kujinufaisha kwa mali za waume zao, au kuwaweka kwenye mzigo mkubwa wa madai ya kifedha ambayo mara nyingi huzidishwa.

Hakika, kinachojulikana miongoni mwa watu kuhusu kuandika wa orodha ya vitu vya ndani (inayojulikana kama "orodha ya samani") ni kuwa, kwa nje, ni njia ya kuhakikisha haki ya mke iliyo mikononi mwa mume. Ikiwa mwanamke ametayarisha nyumba ya ndoa kwa kutumia mahari yake ya awali – iwe mume alitoa mahari kwa pesa taslimu au kwa njia ya vifaa vya nyumbani (samani) alivyoviweka kwa ajili ya nyumba – basi vifaa hivyo ni mali ya mke kikamilifu baada ya kuingiliwa, na huwa mali yake nusu yake ikiwa hakuingiliwa, lakini ndoa ilifungwa. Kwa kawaida, vifaa hivyo huhifadhiwa katika nyumba ya ndoa inayomilikiwa au kupangishwa na mume, hivyo vinakuwa chini ya usimamizi wa mume. Kwa sababu ya kupungua kwa ucha Mungu na watu wengi kupuuza haki za wake zao, jamii ikaona ni vyema kuandika orodha ya mali ya vitu vya ndani (orodha ya samani) kama dhamana kamili ya haki ya mwanamke kwa mume wake iwapo kutazuka mzozo kati yao. Jambo hili limekuwa kawaida kati ya watu wengi, ambapo orodha hii inaandikwa kama haki ya kiraia ya mke dhidi ya mume wake, kama vile deni analodaiwa.

Hata hivyo, njia hii ya kuhakikisha haki imekuwa mara nyingi chanzo cha unyonyaji, hasa pale ambapo mke anakataa kuwa orodha hiyo ni sehemu ya mahari yake, ingawa hali halisi ni tofauti. Mara nyingine, orodha nzima inaweza kuwa ndiyo mahari ya kweli ambayo mume alimlipa mke, na kilichoandikwa kwenye hati ya ndoa ni mahari ya maonyesho tu (mahari ya chini isiyo sahihi), kwa lengo la kuepuka ada na ushuru unaotozwa kulingana na thamani ya mahari iliyoandikwa rasmi.

Katika baadhi ya hali, orodha hiyo inaweza kuwa ya pamoja kati ya wanandoa kwa viwango tofauti, na mara nyingine mke anaweza kuwa ndiye aliyenunua vifaa vyote kwa pesa zake au pesa za familia yake. Kwa mujibu wa maelezo haya, hukumu hutolewa kama ifuatavyo: Ikiwa mume atadai kuwa orodha ya mali (au sehemu yake) ni mahari, na akathibitisha hilo kwa ushahidi wa kisheria – iwe ni kwa mashahidi, vielelezo, au dalili ambazo hakimu anaziridhia – basi hukumu hutolewa kwa maslahi yake. Katika hali hiyo, mke analazimika kuirudisha mali hiyo wakati wa khul'u, kwa mujibu wa fatwa na maamuzi ya mahakama yaliyozoeleka, kwa kuwa haichukuliwi tena kama deni, bali ni fidia kwa ajili ya kujitoa kimwili (kuingiliana), na hivyo inahesabiwa kuwa ni mahari inayopaswa kurejeshwa. Lakini kama haikuthibitika mbele ya hakimu, basi orodha hiyo itachukuliwa kuwa ni haki halali ya mke, awe ameomba khul’u au la, na hatalazimika kuirudisha kwa mume.

Kwa msingi huu, na katika tukio lililoulizwa: Uamuzi wa kuwa orodha ya mali – ikijumuisha vito vya dhahabu – ni mahari au sehemu ya mahari, hutegemea uthibitisho wa hakimu, kwa mujibu wa ushahidi, dalili na vielelezo ambavyo hakimu anayo mamlaka ya kuvitathmini na kuchagua anayoiona sahihi pale zinapopingana. Iwapo itathibitika kwake kwamba orodha ya mali au sehemu yake ni mahari au sehemu ya mahari, basi atahukumu irejeshwe kwa mume, kama ilivyofafanuliwa hapo juu. Kuhusu uasi wa mke (Nushuuz), basi athari ya kisharia ikiwa uasi huo umethibitishwa na mahakama, ni kwamba mke hapati haki ya matunzo ya ndoa (nafaka) hadi atakaporejea katika utiifu kwa mumewe na kuacha uasi huo. Hii ni kwa sababu matunzo ni haki ya mke kutokana na kuwa kwake chini ya mamlaka ya mume, kiuhalisia au kwa kihukumu.

Na ni muhimu kufahamu kwamba uasi (Nushuuz) hauwezi kuthibitika kwa mke isipokuwa kwa hukumu ya hakimu baada ya kuchunguza kwa kina madai ya mume.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas