Gharama za Kumwozesha Binti
Question
Je, gharama za kumwozesha binti na matumizi yake ni wajibu wa nani, baba au mama?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Hakuna tofauti kati ya Wanazuoni wa Fiqhi kwamba matunzo ya watoto wadogo – wawe wa kiume au wa kike – ni wajibu kwa baba zao. Imamu Al-Mawardi alisema: "Matunzo ya watoto ni jukumu la baba zao, kwa ushahidi wa Kitabu (Qur’ani Tukufu), Sunna, Ijma’a na maelekezo ya kisharia." Ama kutoka katika Kitabu (Qur’ani Tukufu): Ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na juu ya mwenye mtoto ni kuwaruzuku na kuwavisha kwa wema} [Al-Baqara: 233], ambapo aya hii inaonyesha kwamba gharama za watoto ni wajibu kwa baba, si mama” imenukuliwa kwa muhtasari[1].
Kwa hiyo, Matunzo ya binti ni jukumu la baba, si mama. Baba anawajibika kutoa mahitaji yote muhimu kwa watoto wake kama chakula, mavazi, na mengineyo kwa mujibu wa desturi ya jamii na hali ya kifedha ya mtu kama yeye.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
[1] Alhawy, 11/447, chapa ya Darul-Kutub Al-Ilmiya.
[2] Al-Jami’I liahkam Al-Quran, 3/163, chapa ya Dar A’alam Al-Kutub.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
