Je, Kunajuzu kwa wanaume au wanawake kuvaa pete, bangili, mkufu, saa, au vitu vingine vilivyotengenezwa kwa dhahabu, fedha, shaba, chuma au vinginevyo, au haifai?
Soma zaidi....
Je, ipi hukumu ya dini katika kupunguza au kuondoa nywele za uso na nyusi, hasa sehemu iliyo kati ya nyusi kwa wanawake na wanaume? Naomba jibu liwe la kutosha na la wazi kabisa, kwa sababu jambo hili limekuwa chanzo cha mabishano makubwa. Naomba jibu liambatane na Hadithi za Mtume (S.A.W.) ili kukomesha kauli za watu wasio na elimu
Soma zaidi....
Je, sharia ya Kiislamu inasemaje kuhusu upasuaji wa kubadilisha jinsia kutoka mwanamume kuwa mwanamke au mfano wa hayo? Na je, kuna maandiko ya kisharia au ya kifiqhi yanayounga mkono au kupinga jambo hilo?
Soma zaidi....
Je, inajuzu kwangu kuonekana bila hijabu mbele ya waume wa dada zangu, ijapokuwa nimekuwa nikiishi nao kwa muda mrefu, na wao ni kama ndugu zangu, na pia kuna tofauti ya umri kati yetu?
Soma zaidi....
Katika kipindi cha hivi karibuni, kumekuwa na sauti kadhaa zinazosema kwamba hijabu si lazima kwa wanawake, jambo ambalo limepelekea baadhi ya walimu na wanafunzi wa shule kuondoa hijabu zao, na baadhi yao wameuliza kuhusu dalili za ulazima wake kutoka katika Qur’ani Tukufu na Sunna. Hali hii imesababisha suala hili kupelekwa kwa Ofisi ya Fatwa ya Misri ili kutoa ufafanuzi sahihi kuhusu hukumu ya kisheria katika jambo hili, pamoja na dalili kutoka katika Qur’ani Tukufu na Sunna ili kuonesha kile kinachohitajika kisharia kuhusu suala hili.
Soma zaidi....
Sisi ni wataalamu wa kushona na kutengeneza mavazi ya wanaume, na tunaingiza baadhi ya vitambaa kwa ajili ya kutengeneza tai. Baadhi ya vitambaa hivyo vinaweza kuwa vya hariri asilia, lakini ndani yake huwekwa ujazo wa sufu na bitana ya hariri ya viwandani. Tuna mtu anayehusika na utengenezaji wa tai hizi, lakini anakataa kufanya kazi kwa kutumia vitambaa vya hariri asilia, akidai kuwa ni haramu kwa wanaume.
Soma zaidi....
Je, baba ana haki ya kumlazimisha binti yake kuvaa Hijabu, kumzuia asitoke nje ya nyumba, kumlazimisha kuacha kazi yake kwa sababu ya kutovaa Hijabu, na yote haya kuyafanya sharti ya kuvaa Hijabu? Pamoja na hayo, anafanya hili ndio sharti katika maisha yake ya kila siku?
Soma zaidi....
Ni ipi hukumu ya baba kukaa uchi kabisa mbele ya watoto wake wadogo, na anaweza kufanya hivyo akiwa na umri gani ikiwa inajuzu?
Soma zaidi....
Assalaamu Aleykum. Mimi ninaishi nchini Ufaransa . Nataka kujua ni mavazi gani yanayofaa kwa kutokea barabarani, na kadhalika wakati wa Swala? Ili yasiwe yenye kuvutia (kama shati n.k.) na isifanane na mavazi ya wasiokuwa Waislamu. Na ni ipi mipaka ya kushabihiana na wasio Waislamu katika nchi isiyo ya Kiislamu?
Soma zaidi....
Assalaamu alaykum. Je, mfuasi wa Madhehebu ya Imamu Shafi anaweza kuvitumia vipodozi kama manukato, losheni na shampuu vilivyo na alkoholi ndani yake? Kuna mtu fulani aliniambia kwamba ikiwa alkoholi ni ya ulevi, basi inazingatiwa kuwa najisi, lakini ikiwa haina ulevi, haizingatiwa kuwa najisi. Kwa mfano, alkoholi ya Ethyl ni najisi kwa sababu ina ulevi, wakati alkoholi ya Sitisliy sio najisi kwa sababu siyo ulevi. Najua kwamba kulingana na Madhehbu ya Hanafy, mtu anaweza kutumia aina yeyote ya alkoholi isipokuwa ile iliyotengenezwa kwa zabibu na tende. Tafadhali nifafanulie hili na mniambie ni aina gani ya alkoholi inaweza kutumika kwa mujibu wa Madhehebu ya Shafi?
Soma zaidi....
Nina pete mbili za Ndoa za dhahabu ya manjano, na nilijua kwamba dhahabu ya manjano ni haramu kwa wanaume, kwa hiyo nitatengeneza pete mbili nyingine, lakini swali langu sasa ni: Je, pete zinazotengenezwa kwa dhahabu nyeupe ni haramu kwa wanaume?
Soma zaidi....
Je, ni ipi hukumu ya uvaaji wa kuvutia wa wasichana na mahusiano yao na wavulana ndani ya Chuo Kikuu kwa kisingizio cha urafiki? Je, ni vidhibiti gani vya kisharia vya mchanganyiko huu? Je, ni nini mtazamo wa Uislamu kuhusu wavulana wa wenye tabia za kike ndani ya Vyuo Vikuu?
Soma zaidi....
Mfanyakazi wa serikali mwenye kipato kidogo anasaidia familia ya watu saba. Mapato yake hayatoshi kukidhi mahitaji ya kimsingi ya maisha, kwa hivyo mke wake anafanya kazi ya kutengeneza nywele saluni, na kuwapamba wanawake nyumbani. Anauliza hukumu ya Kiislamu juu ya hili.
Soma zaidi....
Ni ipi hukumu ya Sharia ya Kiislamu kuhusu mavazi ya mwanamke na hukumu ya kudhihirisha nyewele zake?
Soma zaidi....
Kwanza: Ni nini hukumu ya kuvaa suruali iliyobana kwa mwanamke?
Pili: Ni yapi masharti ya lazima yanayotakikana kwa mavazi ya mwanamke katika Sharia ya Kiislamu? Na ni sehemu zipi zinazoruhusiwa kuonekana katika mwili wa mwanamke?
Tatu: Ni ipi hukumu au adhabu ya kuvunja masharti na vidhibiti vya mavazi ya mwanamke?
Nne: Ni nini hukumu ya mwanamke kuweka mapambo na (Make up), uturi wakati anapotoka nje ya nyumba yake hata kwa muda mchache?
Soma zaidi....
Je, inapaswa kwa mwanamke Muislamu kuvaa nguo za rangi za giza na kuepuka rangi ang’avu kama nyekundu, ya manjano na nguo zenye michoro ya maua?
Soma zaidi....
Je, ni ipi hukumu ya kisheria kuhusu kutumia Masanamu yaliyo uchi katika vyuo vya sanaa, ambapo huchorwa au kutengenezwa sanamu ya mtu aliye uchi kabisa — iwe ni mwanaume au mwanamke aliyeacha kufunika sehemu za siri — au nusu uchi kwa kisingizio cha kujifunza uwiano wa mwili wa binadamu au kuhisi maumbo yake? Je, inaruhusiwa kutumia masanamu inayofananishwa na mwanadamu aliye uchi kwa madhumuni haya, au ni haramu?
Soma zaidi....
Je, inatakiwa kwa mwanamke kuficha sehemu inayozunguka chini ya kidevu hadi shingo kwa kuzingatia kuwa si sehemu ya uso, au ni sehemu ya uso inayoruhusiwa kufichuliwa? Tunaomba hukumu ya hilo katika hali ya sala na nje ya sala!
Soma zaidi....
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
