Hijabu

Egypt's Dar Al-Ifta

Hijabu

Question

Katika kipindi cha hivi karibuni, kumekuwa na sauti kadhaa zinazosema kwamba hijabu si lazima kwa wanawake, jambo ambalo limepelekea baadhi ya walimu na wanafunzi wa shule kuondoa hijabu zao, na baadhi yao wameuliza kuhusu dalili za ulazima wake kutoka katika Qur’ani Tukufu na Sunna. Hali hii imesababisha suala hili kupelekwa kwa Ofisi ya Fatwa ya Misri ili kutoa ufafanuzi sahihi kuhusu hukumu ya kisheria katika jambo hili, pamoja na dalili kutoka katika Qur’ani Tukufu na Sunna ili kuonesha kile kinachohitajika kisharia kuhusu suala hili.

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Kwa hakika hijabu ya mwanamke MUislamu ni wajibu kwa kila aliyefikia umri wa kuvunja ungo, yaani umri ambao msichana huanza kuona hedhi. Hukumu hii imethibitishwa na Kitabu (Qur'ani Tukufu), Sunna na makubaliano ya Umma wa Kiislamu.

Dalili yake kutoka Qurani ni kauli yake Mwenyezi Mungu: { Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. } [Al-Ahzaab: 59]

Na kauli yake (S.W.) katika sura ya An-Nuur: {Na useme kuwaambia Waumini wanawake wayainamishe macho yao kutoyaangalia yasiokuwa halali kwao miongoni mwa tupu, na wazilinde tupu zao na yale Aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu, wala wasionyeshe waziwazi pambo lao kwa wanaume, bali wajipinde kulificha pambo lao isipokuwa nguo za juu ambazo imezoeleka kuzivaa, iwapo hakuna kwenye nguo hizo kivutio cha kupelekea kufitinika nao, na waviangushe vifiniko vya vichwa vyao kwenye uwazi wa sehemu za juu za nguo zao kwenye sehemu za vifua vyao huku wamezifinika nyuso zao ili sitara yao itimie. Na wasiuonyeshe urembo uliofichika isipokuwa kwa waume zao, kwani wao wanaona kutoka kwao wasiyoyaona wengine. Na sehemu ya urembo huo, kama uso, shingo, mikono miwili na sehemu za begani za mikono, zinafaa kuonekana na baba zao au baba za waume zao au watoto wao au watoto wa waume zao au ndugu zao au watoto wa ndugu zao wa kiume, au watoto wa dada zao au wanawake wenzao, walio Waislamu na sio makafiri, au watumwa waliowatawala au wafuasi kati wanaume ambao hawana malengo wala haja ya wanawake, kama vile mapite wanaowafuata watu kwa sababu ya kula au kunywa tu, au watoto wadogo ambao hawana ujuzi wowote wa mambo yanayohusiana na tupu za wanawake na ambao bado hawana matamanio. Na wasipige miguu yao, hao wanawake, wanapotembea ili kuwasikilizisha watu mapambo yao yaliyofichika, kama vikuku(vinavovawa miguuni kama pambo) na mfano wake. Na rudini, enyi Waumini, kwenye kumtii Mwenyezi Mungu katika yale Aliyowaamrisha kwayo kati ya sifa hizi nzuri na tabia njema, na yaacheni yale ambayo walikuwa nayo watu wa zama za ujinga ya tabia na sifa mbovu kwa matarajio mufaulu kuzipata kheri mbili: ya ulimwenguni na ya Akhera.} [An-Nuur: 31], na makusudio ya Khimar katika Aya: ni kile kifuniko cha nyewele kwa mujibu wa Maandiko haya ya wazi ya Qurani Tukufu yenye maana wazi isiyo na haja ya kuelezwa au kufafanuliwa kwa maaana nyingine.

Ama hadithi: Mtume -S.A.W.- amesema: "Ewe Asmaa, mwanamke akifikia umri wa hedhi, si halali kuonekana kwake isipokuwa haya na haya" na akaashiria kwenye uso wake na viganja vyake. Imepokelewa na Abu Daud.

Na amesema tena - S.A.W.-: "Allah hakubali Swala ya mwanamke aliyefikia umri wa hedhi isipokuwa akiwa amevaa khimari (mtandio kichwa)." Imepokelewa na wanazuoni watano isipokuwa An-Nasai.

Ama kwa Ijma’a (makubaliano ya wanazuoni wa Fiqhi): Umma wa Kiislamu, wa zamani na wa sasa, wote wamekubaliana juu ya wajibu wa hijabu. Hili ni jambo linalojulikana katika dini kwa dharura (yaani ni sehemu ya msingi wa dini).

Na hijabu haichukuliwi kama alama au kigezo cha kuwatofautisha Waislamu na wengineo, bali ni amri ya lazima na ni sehemu ya dini yenyewe.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas