Mikopo ya Vijana kwa Maendeleo na Uwekezaji yenye Riba

Tunayo heshima kubwa kukujulisha kuwa Chama kiko mbioni kuchukua nafasi ya Mfuko wa Jamii katika mchakato wa mikopo ya vijana kwa maendeleo na uwekezaji. Mikopo hii hutolewa kwa viwango vya riba vya masharti nafuu vya takriban asilimia 10, ambayo ni chini ya viwango vya riba vya benki.

Tunatumai unaweza kutufahamisha kuhusu uhalali wa mikopo hii, kwa sababu tunatafuta kufanya matendo mema kwa manufaa ya vijana, tukitafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Tafadhali kumbuka kuwa asilimia 10 inagawanywa kama ifuatavyo:

- Asilimia tano kwa Mfuko wa Jamii.

- Asilimia nne kwa Chama, itumike kwa yatima, masikini, wagonjwa, ajira, na gharama za utawala.

- Asilimia moja kwa makampuni ya bima, ambayo kulipa kwa wale wasioweza kulipa.

Tunatumai utaipatia Jumuiya Fatwa sahihi ya kisharia ambayo kulingana na msingi wake tusonge mbele na mradi huu ikiwa inaruhusiwa, au kuufuta ikiwa ni haramu. Mwenyezi Mungu Mtukufu akujaalie kuwa ni taa, nuru, na muongozo kwetu katika njia ya haki, kwa kufuata sharia ya Mwenyezi Mungu, na kushikamana na kamba madhubuti ya Mwenyezi Mungu, tukifuata nyayo za kipenzi cha Mtume Muhammad (S.A.W).

Soma zaidi....

Bima ya Maisha

Ni nini Hukumu ya Sharia katika Bima ya Maisha?

Soma zaidi....

Kununua Gari Kupitia Benki

Kulingana na ofa iliyowasilishwa na Benki ya Alexandria kwa madhumuni ya kufadhili ununuzi wa magari, tafadhali tunaomba mtupe kwa maandiko kuhusu uhalali wa ofa hii kutoka benki hiyo kwa madhumuni ya kuwanunulia wafanyikazi magari mapya, Pamoja na kizingatia yafuatayo:

1- Mfanyakazi anawasilisha kwa benki bei ya gari analotaka.

2- Mfanyakazi atatia saini kijitabu cha masharti kinachohusiana na benki, ambacho kinasomeka kwa nje "Mkopo wa Ufadhili wa Magari" na kinajumuisha maelezo ya muamala katika kipindi chote cha malipo.

3- Baada ya benki kumtambua mfanyakazi, na ikiwa imekubali kufanya nae muamala, hutoa maagizo kwenye chumba cha maonesho ya magari kuruhusu upelekaji wa gari, ikiweka sharti kuwa umiliki wa gari ni wa benki na itaendelea kuwa chini ya umiliki wake hadi thamani yake ilipwe, pamoja na faida iliyokubaliwa hapo awali na mfanyakazi anayetaka kununua gari hilo.

4- Thamani ya gari inatolewa kwenye chumba cha maonesho ya gari bila mfanyakazi kupokea bei yoyote.

5- Chumba cha maonesho kinafanya mkataba na benki kutekeleza uuzaji wa gari.

Soma zaidi....

Kadi ya Mkopo

Benki yetu inataka kupanua utoaji wake wa bidhaa zinaafikiana na Sharia, kwa kuunga mkono Sekta ya Miamala ya Kiislamu katika Kundi la Benki ya Biashara, na kukidhi mahitaji ya makundi makubwa ya jamii yanayotaka kufuata Sharia katika miamala yao, tunaomba maoni ya kisheria kuhusu utoaji wa benki yetu wa “Kadi ya Uwezeshaji”, ambayo ni kadi ya mkopo na ya benki wakati huo huo. Kadi hii inaweza kutumika kama kadi ya mkopo juu ya akaunti ya sasa ya mteja na akiba. Malipo ya ununuzi wa bidhaa hufanywa moja kwa moja kutoka kwa akaunti ya mkopo ya mteja na benki, bila riba yoyote kutozwa kwa benki.

Pia hufanya kazi kama kadi ya mkopo kwa kuweka kikomo cha matumizi ya Murabaha, kilichotolewa kwa mteja wa benki, kuwawezesha kununua bidhaa kwa kutumia tu fomula ya Murabaha kwa muda maalumu wa ulipaji. Marejesho mahususi yanaamuliwa kwa benki kwa kuzingatia makubaliano na mteja wa Murabaha. Urejeshaji huu haujarekebishwa kulingana na shughuli za Murabaha zilizotekelezwa. Mkataba wa Murabaha unahitimishwa kwa thamani ya manunuzi pamoja na marejesho yaliyokokotolewa na benki. Thamani iliyoahirishwa—thamani ya bidhaa iliyonunuliwa na faida ya benki—hulipwa kwa awamu katika kipindi chote cha Murabaha. Miongoni mwa udhibiti maalum wa kadi hii ni kwamba ni maalumu kwa ununuzi wa bidhaa tu, bila kuruhusu utoaji wa fedha. Pia inakataza ununuzi wa dhahabu, au fedha au sarafu kwa kutumia kadi.

Tunaomba kuangalia jambo hili na kutoa maoni ya kisharia, kulingana na maoni na mazingatio, ili tuweze kuyazingatia kabla ya kutoa kadi.

Soma zaidi....

Hukumu ya Ulaghai ili Kupata Haki ya Safari Isiyofuata Sheria

Baadhi ya Maprofesa wa Vyuo Vikuu hutumia njia za ulaghai ili kupata kibali cha waajiri wao na kibali cha kusafiri kwa ajili ya kazi nje ya nchi. Ujanja wao huu ni mwingi, ikiwa ni pamoja na kuunda mikataba ya uwongo kwa wenzi wao, ambayo hununuliwa kwa pesa, ili kupata ruhusa ya kusafiri pamoja na mke wake. Je, ni ipi hukumu juu ya hili?

Soma zaidi....

Mikataba ya Hewa ya Ajira

Baadhi ya watu katika baadhi ya nchi za Kiislamu hufanya mikataba ya hewa na wale wanaotafuta visa ya nchi hiyo. Baada ya kuingia nchi hiyo, hutafuta kazi huko. Mwenye mkataba—anayejulikana kama mfadhili—hupokea kiasi fulani cha pesa kutoka kwa mwombaji wa visa. Kwa kuongeza, wanaweza pia kupokea asilimia ya kila mwezi ya mapato ya mfanyakazi badala ya ufadhili wao wa kuendelea na kuendelea kukaa nchini. Je, ni ipi hukumu juu ya hili? Vile vile, ni ipi hukumu ya wanaopatanisha mikataba hiyo?

Soma zaidi....

Kufanya kazi katika Benki

Ni ipi hukumu ya kufanya kazi katika Benki za uwekezaji? Kwa kuzingatia kwamba aina ya kazi yangu inahusisha kusajili maombi ya wateja na idara nyingine za Benki.

Soma zaidi....

Kuuza dhahabu iliyotengenezwa kwa awamu

Je, inajuzu kununua dhahabu iliyotengenezwa kwa deni?

Soma zaidi....

Hukumu ya Kununua na Kutumia Bidhaa Bandia, Zisizo za Asili

Watu wengi huuza bidhaa kama vile nguo, vifaa na bidhaa za umeme zinazofanana kwa sura, mtindo na nembo kwa chapa asili, ingawa hawana leseni ya kuuza bidhaa hizi kutoka kwa kampuni asili. Kwa hivyo, hii inaweza kuainishwa kama kuiba bidhaa asili. Je, ni ipi hukumu ya kununua bidhaa hizi ikiwa mnunuzi anajua hilo? Mwenyezi Mungu akulipe kheri.

Soma zaidi....

Mkopo kwa ajili ya kujenga nyumba

Kundi la vijana waliotoka nje ya nchi nchini Marekani, katika jimbo la Oregon, walimwomba mtu aende kwa Mufti ili kupata mwongozo wa mambo yafuatayo:

Wanatamani kujinunulia nyumba ya kuishi badala ya kukodisha au kukaa hotelini. Hawana gharama kamili, na kununua kwa njia iliyopo huko kunapunguza mizigo yao, kwani ni gharama nafuu kuliko kukodisha au kukaa hotelini. Njia ni kwamba nyumba hununuliwa kupitia makampuni ya uwekezaji au kuuzwa na wamiliki wake, na madalali huwaongoza wale wanaotaka kuzinunua. Ikiwa mahitaji yametimizwa, muuzaji na mnunuzi hugeukia Benki. Benki humlipa muuzaji gharama kamili na humkopesha mnunuzi sehemu kubwa baada ya kulipa malipo ya awali. Mkopo huu unalindwa na nyumba, na mkataba unatayarishwa kati ya Benki na mnunuzi unaobainisha kiwango cha riba na muda wa kurejesha. Mnunuzi anaweza kuuza kwa kutumia njia sawa. Swali ni: Je, mkopo huu wa Benki unachukuliwa kuwa aina ya miamala ya riba au la?

Soma zaidi....

Fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa Miradi

Tunaomba rai (ya Uislamu) kuhusu fedha zinazotolewa kwa vijana na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii na Benki kwa ajili ya miradi ya vijana, ingawa zinarudishwa na riba.

Soma zaidi....

Wakala wa kisharia

Ni ipi hukumu ya mteja kuweka wakala katika manunuzi ya malipo kwa awamu?

Soma zaidi....

Kuuza dawa zisizojulikana zinapotoka

Ni ipi hukumu ya Kuuza dawa zisizojulikana zinapotoka na zisizo na kibali? 

Soma zaidi....

Ushauri kuhusu namna ya kulinda maisha mazuri kati ya wanandoa

Vipi tunaweza kulinda maisha mazuri kati ya wanandoa?

Soma zaidi....

Kununua nyumba kabla ya kujengwa

Ipi hukumu ya kununua nyumba kabla kujengwa?

Soma zaidi....

Kuuza dhahabu na fedha kwa malipo ya awamu.

Ipi hukumu za kuuza dhahabu na madini ya fedha kwa malipo ya awamu kwa kuongeza thamani katika bei ya asili?

Soma zaidi....

Kuuza dhahabu

Ipi hukumu ya ziada ambayo sonara anaichukuwa wakati wa kubadilisha dhahabu ya zamani?

Soma zaidi....

Kuuza kwa malipo awamu

Inaruhusiwa kununua gari kwa awamu kutoka benki?

Soma zaidi....

Kushiriki katika mashindano

Nini hukumu ya kushiriki katika mashindano ya kubahatisha michezo?

Soma zaidi....

Kuzuia masilahi

Je, nini hukumu ya baadhi ya wafanyakazi kuzuia maslahi ya watu pasipo na haki?

Soma zaidi....

Miradi bila leseni

Je, nini hukumu ya kufungua viwanda visivyo na leseni?

Soma zaidi....

Zaka ya Hisa katika Makampuni Uwasilishaji wa Uchambuzi

Zaka ya Hisa katika Makampuni Uwasilishaji wa Uchambuzi

Soma zaidi....

Zabuni.

Ipi hukumu ya kushikiri katika zabuni za serikali au binafsi, na kulipia gharama kwa ajili hiyo?

Soma zaidi....