Hukumu ya Ulaghai ili Kupata Haki y...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Ulaghai ili Kupata Haki ya Safari Isiyofuata Sheria

Question

Baadhi ya Maprofesa wa Vyuo Vikuu hutumia njia za ulaghai ili kupata kibali cha waajiri wao na kibali cha kusafiri kwa ajili ya kazi nje ya nchi. Ujanja wao huu ni mwingi, ikiwa ni pamoja na kuunda mikataba ya uwongo kwa wenzi wao, ambayo hununuliwa kwa pesa, ili kupata ruhusa ya kusafiri pamoja na mke wake. Je, ni ipi hukumu juu ya hili?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Imethibiti katika sharia ya Kiislamu kwamba mtu lazima awatii wenye mamlaka na kufuata sheria zilizotolewa nao, ikiwa tu si sheria zilizoharamishwa kwa makubalino ya Umma. Ikiwa mtawala amemuwajibisha Profesa wa Chuo Kikuu kutumia muda fulani kabla ya kuruhusiwa kusafiri, na ameweka tofauti katika baadhi ya matukio, kama vile kusafiri ili kuambatana na mke, basi lazima mtu afuate sheria hizi. Ulaghai hauruhusiwi katika hili, kwani unaweza kudhoofisha manufaa anayotaka mtawala kwa kutunga sheria hizi. Na inavyoonekana ni kwamba kama mtawala angejua ukweli wa jambo hilo, angepiga marufuku. Hii inatumika ikiwa hila yenyewe inaruhusiwa. Walakini, ikiwa hila ni marufuku, katazo hilo linasisitizwa zaidi. Hii ni pamoja na kuleta mikataba ya uwongo kwa mume. Kwa sababu inahusisha uwongo, ambao umekatazwa isipokuwa katika hali maalumu na hasa zilizofafanuliwa na Mtoa Sheria, basi hutumia katika hali hizo tu. Maudhui ya swali hili si ya aina sawa na yale yaliyosamehewa na Munga Sharia.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Share this:

Related Fatwas