Kuwatoa kizazi wanyama

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuwatoa kizazi wanyama

Question

Ni ipi hukumu ya kuwatoa  kizazi  wanyama?

Answer

Inaruhusiwa kuwatoa kizazi na kuwazuia kuzaa paka na mbwa ikiwa hili litaondoa madhara yao, kama vile mbwa wa mitaani wanao watishia wapita njia barabarani, lakini sharti ni kwamba mnyama asiteswe au wasiondoe kabisa. Pia inaruhusiwa kuwatoa kizazi na kuwazuia kuzaa mifugo kwa lengo la kuwanenepesha, kwa sababu kuna faida katika hili, ambalo ni ongezeko la uzalishaji wa nyama.

Maelezo

Sharia ya Kiislamu inaamuru kuwafanyia wema viumbe wote.  Imepokewa kutoka kwa Abu Hurarah kwamba Mtume (S.A.W) amesema: ((Mwanamke mmoja aliadhibiwa kwa sababu ya paka ambaye hakumlisha, hakumnywesha maji, na hakumruhusu ale wadudu wa ardhini.” Imepokelewa na Muslim.

Kuteswa kwa mnyama huyo ndiko kulikosababisha mwanamke huyo kuingia Motoni.

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira R.A amesema:  Mtume (S.A.W) amesema: (Mbwa alipokuwa akizunguka kidimbwi cha maji, karibu kufa kwa kiu, kahaba mmoja kutoka katika makahaba wa Wana wa Israeli akavua kiatu chake na kumnywesha maji, na akasamehewa kwa ajili ya hilo) Imepokewa na Bukhari.

Hadithi hii inaashiria kwamba kuwahurumia wanyama ndiyo ilikuwa sababu ya Mwenyezi Mungu kumsamahe mwanamke huyo mzinzi.

Kutokana na hili, Wanazuoni wamesema kwamba hukumu ya kuwatoa kizazi wanyama kwa ujumla ni haramu ikiwa hakuna haja au faida kubwa ya kufanya hivyo. Ibn Abbas (R.A) amesema, kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu:

 {...na nitawaamrisha, basi watabadili aliyo umba Mwenyezi Mungu.} [An-Nisa: 119], amesema: "Hii inamaanisha kuwatoa kizazi wanyama."

Hii ni dalili kwamba imekatazwa kuwatoa kizazi na  kuzuia wanyama kuzaa bila sababu ya msingi, kwa sababu husababisha madhara na mateso kwa mnyama na hubadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ama kuwatoa uzazi na kwauzuia wanyama kuzaa  kwa sababu ya lazima, au kuleta manufaa au kuzuia madhara, inaruhusiwa na hakuna ubaya wowote kulingana na mafundisho ya Kiislamu, kwa masharti yafuatayo:

Kwanza: Haipaswi kusababisha maumivu au mateso kwa mnyama, na hili linapaswa kufikiwa kwa kutia ganzi au kwa njia nyingine kama hiyo.

Pili: Jambo hilo linapaswa kufanywa chini ya usimamizi wa daktari wa mifugo au mtaalamu, ili kulinda uhai wa mnyama.

Tatu: Utoaji uzazi haupaswi kutishia kutoweka kwa mnyama na kuendelea kwa aina ya mnyama huyo.

Ikiwa masharti na vithibiti hivi vitatimia, basi kutolewa kizazi mnyama ni halali. imepokewa kutoka kwa Abu Ad-Darda' R.A. kwamba amesema: "Mtume (S.A.W) alitoa kafara ya kondoo dume wawili waliotolewa kizazi." .

Kwa kuzingatia yaliyo hapo juu, tunaweza kusema kuwa hukumu kuhusu kutoa uzazi na kuzuia kuzaa kwa wanyama ni kama ifuatavyo:

kwanza: Inaruhusiwa Kuwatoa kizazi paka na mbwa ikiwa hili linafanywa ili kupata manufaa makubwa au kuzuia madhara, kama vile jambo la kutisha la kuenea kwa mbwa wa mitaani katika baadhi ya mitaa na vijiji, ambalo linaweka hatari kwa maisha ya watu, kiasi kwamba watu wengi wameitaka serikali kuingilia kati ili kudhibiti hali hili.

Pili: Kuwatoa kizazi wanyama wanaofugwa kwa ajili ya nyama kwa lengo la kuwanenepesha ni halali kwa mujibu wa Wanazuoni wengi, mradi tu mnyama asiteswe.

Tunapata faida Kutokana na yaliyotangulia:

Kunajuzu kuwatoa kizazi wanyama ikiwa ni kwa masilahi, mradi tu mnyama asiteswe na kuhakikiwe kuendelea kuwepo kwa aina ya mnyama huyo.

Share this:

Related Fatwas