Kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume, kunema katika vikao vya dhikri, na kuwaita mawalii kwa jina la “Bwana Wangu” (sayyid)
Question
Baadhi ya Wahubiri wa Swla ya Ijumaa katika mji wetu walidai kwamba:
1- Kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume ni haramu.
2- Kutembea kwa maandamano, kubeba bendera, na kupiga matari kwa mnasaba wa Maulidi ya Mtume ni haramu.
3- Kufanya mikesha ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume ni haramu.
4- Kununua na kutoa peremende katika siku ya kuzaliwa Mtume ni haramu.
5- Kusimama katika mizunguko ya dhikri na kunema ndani yake ni haramu.
6- Kuita jina la "bwana wangu" kwa vipenzi vya Mwenyezi Mungu ni haramu.
Je, ni ipi hukumu juu ya hilo?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kusherehekea Maulidi ya Mtume (S.A.W) kunachukuliwa kuwa miongoni mwa matendo bora na ibada kubwa kabisa. Kwa sababu ni kielelezo cha furaha na upendo kwake (S.A.W), ambayo ni moja ya misingi ya imani. Imepokelewa kutoka Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), amesema: “Hataamini mmoja wenu mpaka niwe kipenzi kwake zaidi kuliko baba yake na mtoto wake na watu wote”. Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari.
Kusherehekea kuzaliwa kwake Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), ni aina ya kumsherehekea Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), ni jambo la uhakika na halali. Yeye ndiye neema kubwa zaidi juu ya ulimwengu, na kushukuru kwa neema ni jambo la kutamanika na la kusifiwa, na mwenye kuzitekeleza si wa kulaumiwa, bali ni kusifiwa na kushukuriwa.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), yeye mwenyewe ametuwekea aina ya shukurani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuzaliwa kwake adhimu. Imepokelewa kutoka Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), kwamba alikuwa akifunga siku za Jumatatu na kusema: “Hiyo ndiyo siku niliyozaliwa.” Hadithi hiyo imepokelewa kutoka kwa Imamu Muslim kutoka katika Hadith ya Abu Qatadah (R.A). Ni kielelezo cha shukurani kutoka kwake Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), kwa neema za Mwenyezi Mungu juu yake na juu ya taifa kupitia utukufu wake. Kwa hiyo, inafaa zaidi kwa umma kuiga mfano wake (S.A.W), kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema yake na kipawa chake kwa Mteule kwa kila namna ya shukurani. Makusudio yaliyokusudiwa ya kusherehekea kwa uhalali wa kuzaliwa Mtume (S.A.W) ni watu wakusanyike ili kumdhukuru Mwenyezi Mungu, kumwimbia Mtume S.A.W, na kuwalisha masikini kama sadaka kwa Mwenyezi Mungu, na kama tamko la mapenzi kwa Mola Mlezi wa viumbe, Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), ni kama tangazo la furaha katika siku ya kuzaliwa kwake (S.A.W).
Kusherehekea Maulidi ya Mtume (S.A.W) kwa namna tuliyoieleza imekuwa ni desturi ya watangulizi wetu wema tangu karne ya nne na ya tano. Uhalali wake umesisitizwa na Maimamu na Mwanachuoni zaidi ya mmoja katika kazi tofauti au ndani ya vitabu vyao wenyewe, vikiwemo: Abu Shamah Al-Maqdisi, Mwalimu wa Imamu Al-Nawawi; Ibn Al-Hajj katika kitabu chake "Al-Madkhal"; Al-Hafidh Ibn Hajar, mfasiri wa Al-Bukhari; na Al-Jalal Al-Suyuti katika risala tofauti yenye kichwa cha “Husn Al-Maqsid fii amal Al-Maulid - Nia Njema ya Kusherehekea Maulidi ya Mtume.”
Katika mkusanyiko wake mpana wa wasifu wa Mtume, "Subul al-Huda wa Al-Rashad fi Sirat Khair Al-Ibad," Al-Salihi anamnukuu mtu mmoja mwema akisema kwamba alimuona Mtume (S.A.W) katika ndoto na akamlalamikia kwamba baadhi ya watu wanaona kusherehekea Maulidi ya Mtume (S.A.W) ni uzushi. Mtume (S.A.W) akajibu: “Mwenye kufurahi pamoja nasi tunafurahi pamoja naye. Ingawa ndoto hazitoi hukumu ya kisharia, lakini zinaweza kutumika kama ushahidi kwa mambo yanayoafikiana na kanuni za sharia ya Kiislamu.
Desturi ya kununua peremende na kupeana zawadi siku ya kuzaliwa Mtume inajuzu yenyewe. Hakuna uthibitisho wa kuzuia au kuruhusu wakati wowote, hasa ikiwa inaambatana na kusudi la uadilifu, kama vile kuleta shangwe kwa familia au kuunganisha koo. Katika hali kama hizi, inachukuliwa kuwa ni ya kutamanika na yenye kuhitajika, na sharia ya Kiislamu hulipa thawabu vitendo hivyo. Kusema kwamba ni haramu au ni marufuku ni aina ya kulaumiwa ya msimamo mkali.
Ama mila katika baadhi ya mikoa, ambapo wale wanaosherehekea Maulidi ya Mtume (S.A.W) wakibeba mabango yenye maandishi ya aya za kidini, na kuimba nyimbo za kumsifu Mtume na mashairi ya kujinyima, hakuna ubaya wowote katika hilo, maadamu halina chochote kinachopingana na sharia za Kiislamu, kama vile kuchanganyikana kwa kulaumiwa kwa watu, au kuvuruga maslahi ya umma, kuvuruga mambo.
Ikiwa kupiga tari kutangaza ndoa kunaruhusiwa na sharia ya Kiislamu kama njia ya kuonesha furaha juu ya ndoa - kama katika Hadithi ya Al-Tirmidhiy: “Itangazeni ndoa hii, ifungeni misikitini, na pigeni matari kwa ajili yake.” Kutumia tari kueleza furaha juu ya kuzaliwa kwa mbora wa viumbe ni bora zaidi na inafaa zaidi. Kuruhusiwa kwa haya yote ni kwa sharti la kuzingatia adabu sahihi inayotakiwa na sharia ya Kiislamu katika hali kama hiyo.
Ama kusimama katika mizunguko ya dhikri na kuyumba-yumba au kunema ndani yake, tunasema: Mwenyezi Mungu Mtukufu amewataka Waislamu wamdhukuru Mwenyezi Mungu kwa ujumla. Akasema: “Enyi mlio amini! Mdhukuruni Mwenyezi Mungu kwa wingi wa kumdhukuru.” (Al-Ahzab: 41). Na akasema akiwasifu waja wake Waumini: “Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala” (Al-Imran: 191). Na kutoka kwa Abu Musa Al-Ash’ariy-(R.A) kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Mfano wa mwenye kumdhukuru Mola wake Mlezi na asiyemdhukuru Mola wake ni kama mfano wa aliye hai na maiti. Hadithi hii imepokelewa na Al-Bukhari. na Al-Tirmidhi na Ibn Majah.
Na kutoka katika Hadithi ya Abdullah Ibn Busr (R.A) kwamba: “Mtu mmoja alisema, ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sharia za Uislamu zimenizidi nguvu, basi niambie kitu ninachoweza kushika.’ Akasema, ‘Ulimi wako uwe na unyevu kwa kumdhukuru Mwenyezi Mungu”. Msukumo wa ukumbusho umeelezwa katika Sharia Tukufu kwa jumla. Kanuni ni kwamba haizuiliwi kwa hali moja au nyingine au kwa wakati mmoja au mwingine. Kwa kuwa Sharia haikatazi kusimama wala kunema wakati wa dhikri, hii inajuzu, maadamu mwenye kumdhukuru Mwenyezi Mungu anakuwa na utulivu na heshima wakati wa harakati, na wala hajishughulishi na jambo lolote linalopingana na adabu inayotakiwa mbele ya Mwenyezi Mungu wakati wa kumdhukuru.
Na inatakiwa kwa yeyote anayedai kuwa ni haramu au ni marufuku kutoa ushahidi kwa madai yao, jambo ambalo linapingana na kanuni ya msingi. Ruhusa inathibitishwa iwapo harakati itatokea pale mtu anayemdhukuru Mwenyezi Mungu anapolazimishwa na kuzidiwa nguvu, kama vile anapoingizwa katika ukumbusho na kushikwa na hali ya furaha, na kufanya harakati hiyo bila kukusudia, kama mshairi alivyosema:
Na hakika mimi natetemeka kwa kukutaja kwako,
kama ndege anavyotetemeka anaponyeshewa na mvua.
Imepokelewa kutoka kwa Al-Hafidh Abu Nu’aym katika Al-Hilya kutoka kwa Imamu Ali (R.A) kwamba amewaelezea Maswahaba (R.A): “Anapotajwa Mwenyezi Mungu huyumba-yumba kama mti unaoyumba katika siku yenye upepo, na machozi yao yanatoka mpaka nguo zao zinalowa. Hadithi hii inabainisha wazi kwamba Maswahabah (R.A) walikuwa wanatikisika sana katika dhikri. Mwanachuoni Ibn Kamal Basha, Mwanachuoni wa Hanafi amesema alipoulizwa kuhusu suala hili:
Hakuna ubaya katika furaha, ikiwa una yakini na ukweli,
wala katika kuyumba, ikiwa uko huru na madhara.
ukatembea kwa mguu wake, na ni haki kwa yule
Aliyeitwa na Bwana wake atembee juu ya kichwa chake.
Jambo la msingi ni kwamba maadamu hali ya kumdhukuru Mwenyezi Mungu ina nidhamu na maneno ya ukumbusho hayakupotoshwa kwa njia ambayo itaharibu maana yake, basi hakuna sababu ya wazi ya kuharamisha."
Ama kuita jina la ubwana kwa viumbe vilivyoumbwa, ikiwa mwenye ubwana ni Mtume (S.A.W), basi hili linajuzu na linatakiwa kwa maafikiano ya Waislamu. Yeye mwenyewe Mtume (S.A.W) alieleza haya juu yake mwenyewe, akisema: “Mimi ni bwana wa wana wa Adamu,” na katika Hadithi nyingine: “Mimi ni bwana wa wanadamu”. Hadithi hii imepokelewa na Bukhary na Muslim. Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamrisha kumcha na kumtukuza, kama Anavyosema: “ Ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mumsaidie, na mumhishimu, na mumtakase asubuhi na jioni.” (Al-Fath: 9). Sehemu ya heshima Kwake ni kumtukuza Yeye, kama Qatadah na As-Suddi walivyosema: “Na mumhishimu” maana yake ni kumfanya bwana.
Ama kumwita jina la bwana mtu yeyote asiyekuwa Mtume (S.A.W) miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa, hili pia ni jambo la halali kwa mujibu wa matini ya Qur’ani Tukufu na Sunna na matendo ya umma, yaliyofuatana na waliotangulia, bila ya pingamizi lolote. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kuhusu bwana wetu Yahya (A.S): “Alipo kuwa kasimama chumbani akiswali, Malaika kamnadia: Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria Yahya, ataye kuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu, na ni bwana na mt'awa na Nabii kwa watu wema” (Al Imran: 39). Imaam Al Qurtubi amesema: “Hii inaashiria kujuzu kumwita mtu bwana, kama inavyojuzu kwa mtu kuitwa Mpenzi au mkarimu. Ama Sunna: Mtume (S.A.W) amesema kuhusiana na Al-Hasan na Al-Husayn (A.S): "Al-Hasan na Al-Husayn ni mabwana wa vijana wa Peponi." Imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhiy na Al-Hakim, ambao wamezithibitisha.
Na kauli yake Mtume (S.A.W), kama ilivyopokelewa kutoka kwa Al-Bukhari kuhusu A-Hasan Ibn Ali (A.S): “Huyu mwanangu ni bwana. Na kauli yake (S.A.W) kutoka kwa Saad Ibn Muadh (R.A) kuwaambia Maswahaba watukufu: “Simameni kwa bwana wenu. Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari.
Ama kuhusu matendo ya Umma: Miongoni mwao ni kauli ya Umar (R.A) kuhusu Abu Bakr Al-Siddiq na Bilal (R.A): “Abu Bakr ni bwana wetu na alimwacha huru bwana wetu”. Imepokelewa na Al-Bukhari. Kuna Hadithi nyingi za namna hiyo, ambazo Maswahaba walizisikia bila pingamizi wala upinzani. Hii ilijumuisha makubaliano ya kimyakimya juu ya uhalali wake, hali ambayo ni hoja halali, kama inavyothibitishwa katika kanuni za kimsingi.
Kwa hiyo, kuwaita Ahlul-Bayt mabwana na mawalii wema wa Mwenyezi Mungu inajuzu, kwa hakika ndio inavyotakiwa na sharia ya Kiislamu, kwani inadhihirisha tabia njema, na kuwaheshimu. Mtume (S.A.W) amesema: “Si miongoni mwetu asiyewaheshimu wazee wetu, kuwahurumia wadogo zetu, na kutambua haki ya Wanachuoni wetu”. Imepokelewa na Ahmad na Al-Hakim, ambaye ameithibitisha, kutoka kwa Ubadah Ibn Al-Samit (R.A).
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
