Kuwajibika kwa gharama za kumtunza ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuwajibika kwa gharama za kumtunza binti asiyevaa hijabu

Question

Ningependa kujua ikiwa ni wajibu kwa wazazi Waislamu kuwalazimisha mabinti wao kuvaa hijabu na kuwatisha kuwa hawatawatimizia mahitaji yao ikiwa hawatavaa hijabu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Inajulikana kuwa baba ana mamlaka ya kisheria juu ya binti yake,  na sharia ya Kiislamu imewapa wazazi haki ya kuwaamuru mabinti zao kuvaa hijabu bila ya kumwumiza au kumlazimisha kwa nguvu au ukatili. Hata hivyo, hakuna uhusiano kati ya kuvaa hijabu na wajibu wa kutoa matunzo (nafaka). Matunzo ni wajibu wa baba kwa binti yake, awe amevaa hijabu au la. Na katika Rehema ya Uislamu ni kwamba kutotekeleza baadhi ya wajibu wa kidini hakuondoi haki ya kupata matunzo, bali matunzo yanabaki kuwa ni wajibu juu ya baba hata katika hali kama hiyo.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas