Hija na Umra kwa njia ya mashindano

Mimi na baadhi ya rafiki zangu tumeshiriki katika mashindano ya kitamaduni ambayo huandaliwa na moja ya taasisi za misaada, na wakatangaza kwamba zawadi ya mashindano hayo ni safari ya Hija au Umra, je, kunajuzu kwangu kwenda Hija au Umra nitakaposhinda katika mashindano hayo?

Soma zaidi....

Wasia kwa Hija ya Faradhi

Baba yangu imemuwajibikia ibada ya Hija, na ameazimia kuitekeleza, isipokuwa hakuweza kutokana na maradhi yaliyompata kabla ya safari, na ameniambia kwamba akipona, basi atahiji mwenyewe mwaka unaofuata, na akatoa wasia kwamba akifariki nikahiji kwa niaba yake kwa mali yake, na aliendelea na maradhi mpaka akafariki, ni ipi hukumu ya kisharia katika hili?

Soma zaidi....

Kucheza mchezo ili kutimiza gharama za Hija

Ni ipi hukumu ya kucheza mchezo ili kutimiza gharama za Hija? Pamoja na kujua kwamba mchezo huu utakuwa kati yangu mimi na rafiki zangu, na kila mmoja atatoa kiasi cha pesa kila mwezi kwa muda maalumu. Na kila mtu atakuwa na zamu maalumu ya kupokea pesa inayokusanywa kutoka kwa washiriki waengine kila mwisho wa mwezi ukiwa mchezo huo ni wa kila mwezi, kila mwezi anapokea mtu mpaka mshiriki wa mwisho, mimi nitakuwa mtu wa kwanza kupokea.

Soma zaidi....

Kujishulisha na kupiga picha wakati wa Ibada ya Hija na Umra

Nilisafiri katika safari pamoja na (kundi) la mahujaji kwenda Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kutekeleza faradhi ya Hija. Kila tulipopita katika maeneo matukufu, niliona baadhi ya watu waliokuwa pamoja nasi katika kundi la mahujaji wakizidisha sana upigaji picha kwa simu zao kupita kiasi cha kawaida. Jambo hilo lilikuwa linatuletea ucheleweshaji wa kutekeleza ibada kwa wakati unaotakiwa, na pia liliwasababishia usumbufu baadhi ya wazee na watu wasiojiweza. Kwa hiyo niliwaomba kwa heshima wapunguze wingi wa kupiga picha, lakini mmoja wao alinijibu kuwa yeye anajitahidi kupata picha za kumbukumbu kwa  maeneo matukufu. Hata hivyo, waliendelea kufanya hivyo mpaka jambo hilo likamfikia msimamizi wa mpangilio wa safari, naye pia alikasirishwa na kitendo hicho, kwa kuwa kinamkwamisha katika kazi na jukumu lake kutokana na kuchelewa kwa mwendo wetu. Basi, hukumu kwa mujibu wa Sharia ni ipi kuhusu kuzidisha upigaji picha kwa namna hii iliyopitiliza?

Soma zaidi....

Maana ya uwezo katika Hija na Umra

Ni nini maana ya uwezo katika Hija na Umra

Soma zaidi....

Hija ya Mtoto Mdogo inaondoa ulazima wa Hija

Nilihiji na baba yangu nilipokuwa na miaka nane, je Hija yangu hiyo ni sahihi? Na je Hija hiyo inaondoa ulazima kuhiji baada ya kubaleghe au la

Soma zaidi....

Hukumu ya kuchinja Udh’hiya baada ya siku za Tashriiq

Baadhi ya Taasisi za kitaifa na za kiraia zinawawakilisha Waislamu kuchinja Udhiya na kusambaza nyama yake kwa watu masikini wanaostahiki, wakati mwingine idadi ya mifugo watakaochinjwa huwa kubwa sana mpaka muda wa Sikukuu ya Idi na siku tatu za Tashriiq hautoshi, ingawa kuchinja wakati wote wa muda huu, na huenda matayarisho na maandalizi ya kuchinja idadi hiyo ya mifugo yahitaji kuongeza muda zaidi ya siku hizo kwa masilahi yanayozingatiwa; kama vile upatikanaji wa aina maalumu ya mifugo wenye manufaa kwa masikini, au huenda kuongezeka kwa muda wa kuchinja huwa kwa sababu ya nyenzo na vifaa vya shirika maalumu ambalo ni chaguo lililo bora zaidi kwa Taasisi inayosimiamia shughuli hizo, basi je hukumu ya kisharia katika hali hii? Na je, Udh’hiya wanaochinjwa baada ya kupita kwa siku ya Idi na siku tatu za Tashriiq ni halali kisharia? Na je, inawezekana kukubali kauli ya baadhi ya Wanachuoni wa Fiqhi kuwa: kuchinja kunaruhusiwa kuendelea mpaka mwisho wa mwezi wa Dhul-Hijja?

Soma zaidi....

Kuhiji kwa Mali ya Haramu

Nina rafiki yangu, asilimia kubwa ya mali yake ameipata kwa kazi za haramu, na nimekuwa nikimsihi na kumpa mawaidha mapaka ametubu kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, na sasa anataka kwenda Hija kwa sehemu ya mali yake hiyo, je, kunajuzu kwake kuhiji kwa Mali ya Haramu?

Soma zaidi....

Kuhiji kwa niaba ya marehemu mmoja na kufanya Umra kwa niaba ya marehemu mwingine katika safari moja.

Nataka kujua hukumu ya kisharia kwa mtu aliyekwenda Hija, na akatia nia ya umra kwa niaba ya mama yake aliyefariki, na nia ya Hija kwa niaba ya baba yake aliyefariki, na mwaka wa pili akafanya kinyume, kwa maana akatia nia ya Hija kwa niaba ya mama yake aliyefariki na umra kwa niaba ya baba yake aliyefariki, je, hili linafaa?

Soma zaidi....