Menatul Almanan katika Hukumu za Ta...

Egypt's Dar Al-Ifta

Menatul Almanan katika Hukumu za Tafsiri ya Qur`ani Tukufu

Question

Menatul Almanan katika Hukumu za Tafsiri ya Qur`ani Tukufu 

Answer

Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutambua Utukufu Wake, Ukamilifu wa neema Zake, kutumika uwezo Wake msaada Wake na utiifu Kwake, na kujitenga na Kumuasi pamoja na kutafuta sababu za neema Zake.

Namtakia rehma Mtume Muhammad mja wake na Mtume wake, mbora wa viumbe vyake, kwa kufuata Utume wake, na kuomba uombezi wake, na kutimiza kazi ya ujumbe wake, pamoja na watu wake na Maswahaba zake na familia yake ([1]).

Baada ya Utangulizi:

Masuala ya tafsiri ya Qur`ani Tukufu ni jambo lenye mvutano sana na lenye tofauti, mpaka Wanachuoni wamekuwa pande mbili tofauti, kati ya waliovuka mipaka na waliozembea na waliokati na kati, na miongoni mwao wapo waliofungua mlango na kuzingatia ni katika matendo makubwa mazuri na wenye kuthibitisha kuiweka karibu  zaidi (na Mwenyezi Mungu), wakati ambapo wengine wanaona ni jambo hatari shari na fitina katika dini, na ni njia ya kuharibu Maneno ya Mola wa viumbe, kisha wengine wakasimama kati na kati ya kauli mbili zilizombali na wakajaribu kubana mpasuko, hivyo nikapenda kuchangia katika kulileta jambo karibu na akili, nikakusanya masuala waliyotafautiana – nayo ni moja ya makusudio yanayozingatiwa katika utunzi – nikitangaza kuunga mkono hukumu sahihi Inshaa Allah.

Utafiti umekusanya utangulizi na sura tatu pamoja na hitimisho.

Ama utangulizi: Ndani yake kumezungumzwa historia ya tafsiri ya Qur`ani tukufu na yaliyokuja kwenye tafsiri ikiwa pamoja na mapokezi ya zamani na kuendelea mpaka kufikia hivi sasa katika zama zetu.

Sura ya Kwanza: Anuani yake ni  “Tafasiri ya Qur`ani Tukufu, ufafanuzi na udhibiti”.

Na nimeigawa kwenye sehemu tatu, sehemu ya kwanza nimezungumzia: Misingi ya lugha ya Kiarabu ambayo Qur`ani tukufu imeteremka kwa lugha hiyo. ya pili: Nimezungumzia kuhusu neno “Tafsiri” na kuliweka katika milango:

Mlango wa Kwanza: Maana ya tafsiri kwa upande wa lugha na msamiati.

Mlango wa Pili: Vigawanyo vya tafsiri.

Mlango wa Tatu: Yaliyolazima katika tafsiri kama kazi ya kitaalam.

Katika sehemu ya tatu: Imezungumzia kuhusu Qur`ani Tukufu na kufanya kuwa na milango miwili.

Mlango wa Kwanza: Ufafanuzi wa neno Qur`ani na maana zake.

Mlango wa Pili: Makusudio ya Qur`ani Tukufu.

Sura ya Pili:  Anuani yake ni “Rai mbalimbali katika hukumu za tafsiri ya Qur`ani Tukufu”.

Na nimeigawanya katika sehemu tatu. Sehemu ya Kwanza: Kuhusu hukumu ya kifungu cha kwanza katika vifungu vya tafsiri, nayo ni tafsiri ya neno kwa neno la mfano. Sehemu ya pili: Kuhusu hukumu za kigawanyo cha pili katika uwanda wa tafsiri, nayo ni tafsiri ya neno kwa neno si la mfano.

Na tafsiri hii ina milango miwili, mlango wa kwanza: Dalili za Kisharia kwa wanaopitisha tafsiri hii na majibu yake. Mlango wa pili: Dalili zao za vitendo na ulinganiaji pamoja na majibu yake.

Sehamu ya Tatu: Inahusu hukumu ya kigawanyo cha tatu cha tafsiri, nayo ni tafsiri ya kimaana. Imekusanya sehemu nne. Sehemu ya Kwanza: Dalili za kufaa tafsiri hii na majibu ya wanaipinga. Sehemu ya pili: Vidhibiti ambavyo tunaviona katika hizo tafsiri zinazotegemewa.

Mlango wa Tatu: Faida za tafsiri kwa maana hii. Na mlango wa Nne: Kuondoa yanayoleta shaka kuhusu tafsiri hii.

Na ninategemea Kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu msaada wa kufanikisha na kutimiza pamoja na mwanzo mzuri na mwisho mwema.

Utangulizi wa Kihistoria.

Kuhusu historia ya tafsiri ya Qur`ani Tukufu.

Huenda jambo sahihi sehemu hii ni kuelezea kwa haraka yale yaliyotufikia miongoni mwa mapokezi yanayotusaidia kufahamu mwanzo wa mazungumzo kuhusu tafsiri ya Qur`ani Tukufu au sehemu ya tafsiri kwa mujibu wa tuliyoyapokea, kisha masuala hayo tunayafuatilia ufutiliaji wa kihistoria mpaka kufika kwenye zama zetu hizi za sasa ambazo zimekutana na tafauti kuhusu kadhia hii, na hii kwa nafasi yake ni kutufahamisha sisi katika kuifahamu kisha kufikia hukumu sahihi kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu.

Wahyi kwa Mtume Muhammad S.A.W uliteremka: {Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi} Ashuaraa: [195]. Amri za kulingania dini ya Mwenyezi Mungu kwa mataifa mengine duniani zikaja: {Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote} [Al-Araaf: 158].

Tunaweza kusema kuwa mapokezi ya zamani zaidi ambayo yametufikia kahusu tafsiri ya sehemu ya Qur`ani tukufu ni yale yaliyopokewa na As-Sarkhasy – kutoka kwake Waandishi wamenukuu – kuwa Wafursi walimuandikia Sulaimani Al-Farisy awaandikie Suratul Fatiha kwa lugha ya Kifursi, ndipo akawaandikia, na walikuwa wanasoma hivyo katika ibada ya swala mpaka ndimi zao zikalainika, baada ya kuandika alimuonesha Mtume S.A.W kile alichoandika, na Mtume S.A.W hakumpinga ([2]).

Kisha ukombozi wa Uislamu ukaenea mpaka ukafika maeneo ya Shamu, Misri, Iraq, Furs,i na Rome, watu wengi wakaingia kwenye dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi, na watu wakawa wanasoma Qu'rani tukufu kwa Kiarabu, lugha ya Qur'ani tukufu ikaenea kwa kuenea Uislamu, kwani Qur'ani tukufu na lugha ya Kiarabu vikawa vinalazimiana pamoja.

Waislamu walipokomboa nchi ya Fursi ndipo Qatibah Ibn Musallam alijenga Msikiti huko Bukhara mwaka 94H, na Abubakri Muhammad Ibn Jafar An-Narshakhy amefariki mwaka 348H ametaja kuwa watu wa Bukhara walikuwa wanasoma Qur'ani katika Swala zao ndani ya huo Msikiti kwa Kifursi kwa sababu mwanzoni mwa Uislamu walikuwa hawafahamu Kiarabu ([3]).

Na ikasemwa kuwa watu wa kwanza kutafsiri Qu'rani Tukufu kwa wasiokuwa Waislamu ni watu wa Saryan, kimepatikana kitabu ndani yake kuna tafsiri ya maana ya Aya za Qur'ani kwa lugha ya Kisaryani, hiko kitabu bado kimo ndani ya Maktaba huko Manchester Uingereza, profesa Mankana anasema: “Tafsiri hii imewekwa na Bar Al-Saliby alieshi zama moja na Hajaj bin Youssuf katika theluthi ya tatu ya karne ya kwanza ya Kiislamu” ([4]).

Na profesa Muhammad Hamiduddin amesema: “Qur'ani imetafsiriwa kwa lugha ya Barbara mwaka 127H”

Al-Jahidhwu amesema kuwa Musa Ibn Sayar Al-Answary aliyefariki mwaka 255H alikuwa anatafsiri Qur'ani Tukufu kwa Kiarabu na Kifursi ([5]), na maana ya Qur'ani Tukufu sisi imetufikia kupitia Wanachuoni kutoka miji iliyo wa nyuma ya mto (Kazakhsata) mwaka 345H, na wakaongeza tafsiri za Atwabari aliyefariki mwaka 310H.

Historia ya Tafsiri ya Qur'ani Tukufu katika Lugha za Ulaya ([6]).

Pindi mwangaza wa Uislamu ulipoenea duniani ukaamsha uoni wa  Falme za Ulaya ambazo zilikuwa zimefunikwa gizani, wakajaribu kufuata elimu za Uislamu na maarifa yake na wakachukuwa tafsiri yake kuipeleka kwenye lugha zao.

Kisha baada ya kuanza harakati za watu wa Magharibi wanaojihusisha na elimu za watu wa Mashariki kuliwasaidia kutafsiri Qur'ani Tukufu kwenye lugha zao, malengo yao katika hilo yalikuwa wazi sana, ambapo mara nyingi yalikuwa ni yenye muelekeo wa kupinga Uislamu na kuwafanya watu waukimbie ([7]).

Kwenye hilo inatuonesha kuwa mtu wa kwanza kufanya kazi ya kutafsiri Qur'ani Tukufu ni kundi la Watawa na Wanatheolojia, ambapo Mtakatifu Peter (1156 - 1094) ambaye ni mkuu wa jumba la utawa la Colne nchini Ufaransa alikuwa mtu wa kwanza kudhamini na kusimamia kazi za kutafsiri Qur'ani tukufu kwenye lugha ya Kilatini (1156) akiwa pamoja na Mtawa wa Kiingereza anaitwa “'Robert Rettini' na Mtawa wa Kijerumani anaitwa “Herman”.

Katika barua ya Mtakatifu Peter kwenda kwa Mtakatifu Bernard kulikuwa na yafuatayo: “Mwaka 1141 nimekutana na Robert pamoja na rafiki yake Herman karibu na Opera huko Uhispania wakiwa wametafsiri Qur'ani tukufu kwenye lugha ya Kilatini na wakakamilisha mwaka 1143”, hii ilikuwa tafsiri ya kwanza ya Qur'ani tukufu ikitumiwa na Raymond na Peter wa Toledo, kwa kauli yenye nguvu huyu wa mwisho ndiyo mfasiri wa kweli wa maana ya Qur'ani Tukufu ambapo alikuwa na uwezo mzuri sana wa lugha ya Kiarabu.

Lengo lake lilikuwa kupata maarifa sahihi ya kielimu kuhusu dini ya Kiislamu ili kuupiga vita Uislamu, na kuwa ni silaha kwa Kanisa dhidi ya hatari ya Uislamu, kwani anasema: “Kazi hii ninayoifanya haiwezekani kusemwa: kuwa haina faida, ikiwa kunaugumu kuwaongoa Waislamu waliopotoshwa….basi haitoacha kuwatahadharisha wale wanyonge miongoni mwa wafuasi wa Kanisa”.

Jambo la kushangaza ni kuwa nafasi ya Kanisa imezuia kuchapa tafsiri hii na kuitoa kwa sababu kuitoa kwake ni kusaidia kueneza Uislamu badala ya kuhudumia lengo ambalo limepiganiwa na Kanisa nalo ni kuupiga vita Uislamu. G.H Bousquet anasema: “Tokea mwaka 1141 viongozi wa dini walikutana kwa amri ya “Mtakatifu Peter” Mkuu wa jumba la utawa la Colne ili kutafsiri Qur'ani tukufu kwenye lugha ya Kilatini lengo ni kuupiga vita Uislamu”.

Tafsiri hii iliendelea kuhifadhiwa kwenye kopi mbalimbali, ikizunguka kwenye jumba la utawa kwa muda wa karne nne mpaka pale Theodore Bibliander alipoamua kuichapisha katika mji wa “Bal” huko Uswis mnamo tarehe 11 Januari 1543, na tafsiri hii ikaitwa tafsiri ya “Bibliander” ikawa na utangulizi wa Martin Luther na Philip Melanchthon amezungumza hayo “George Sale” akisema: “Hakika yaliyochapishwa na Bibliander kwa Kilatini akidhania kuwa ndio tafsiri ya Qur`ani Tukufu hayastahiki kuitwa tafsiri, kwani kuna makosa mengi, kufuta na kurekebisha maeneo mengi, hivyo ni vigumu kuidhibiti,  tafsiri hii haikusanyi mfanano wowote na ile tafsiri asilia”.

Huu ushahidi mwingine juu ya uharibifu wa tafsiri hii, tunamnukuu mmoja wa Mustashriki maarufu katika maswala ya tafiti za Qur`ani Tukufu naye ni Mustashiriki wa Kifaransa “Blasher” ambaye anasema: “Tafsiri ya Qur`ani Tukufu ya Toledo kwa sura yeyote ile haionesha kuwa ni tafsiri iliyosalama na ukamilifu” pamoja na hayo, tafasiri hii imetengeneza kiini cha kwanza cha tafsiri zingine za Qur`ani Tukufu zilizobaki kwa lugha ya Ulaya, bali imekuwa na taathira kubwa kiasi cha kuigwa na kufuatwa mfumo wake, kisha baada ya hapo zikaanza kuonekana tafsiri za Qur`ani Tukufu kwa lugha za Ulaya ambapo tafsiri ya kwanza ya Qurani Tukufu kwa lugha ya Kifaransa ilianza kuonekana mwaka 1647 iliandikwa na  Andre De Riore, tafsiri hii ilikuwa gumzo kubwa kwa muda mrefu ambapo iliendelea kuchapwa mara nyingi na kutafsiriwa kwenye lugha mbalimbali za Ulaya. J.D Pearson anasema: “Hakika tafsiri ya Kifaransa ni ya zamani sana, ni tafsiri ya “Andre De Riore” imetolewa chapa nyingi kati ya miaka ya 1647 na 1775, na tafsiri yote ilikuwa inabeba maelezo kwa ufupi kuhusu dini ya Kituruki na baadhi ya nyaraka, kazi hii ilipelekea kupatikana tafsiri ya kwanza ya Qurani Tukufu kwa lugha ya Kiingereza kupitia “'Alexander Ross”, kisha tafsiri zingine kwa lugha ya Kiholanzi kupitia “Glasmacher” na kwa lugha ya Kijerumani kupitia “lang” na kwa lugha ya Kirusi kupitia “'Bestenkov na Frevkin”.

Ndani ya karne ya kumi na saba, ilitolewa tafsiri ya moja kwa moja kutoka lugha ya Kiarabu kwenda Kilatini na Muitaly “Marky” mwaka 1698, na tafsiri hii inazingatiwa ndiyo nguzo ya tafsiri nyingi za hivi sasa, kwani ndani ya kitabu cha lslamologie imekuja kuwa: “Mwaka 1698 Ludwik Marki baada ya zaidi ya miaka arobaini ya utafiti wake wa Qur`ani Tukufu na kwa kupitia Wafasiri mbalimbali Waislamu andiko la Kiarabu la Qur`ani Tukufu lilikuja likiambatana na tafsiri ndogo sana ya Kilatini, tafsiri hii ndiyo ilikuwa ni chanzo cha Wafasiri wengi wa sasa ambao walichukuwa katika tafsiri hii mada muhimu”.

'Henry Lammence alizingatia tafsiri hii ni tafsiri yenye uadilifu sana na marejeo ya Wafasiri wengi wa Ulaya, tofauti tu ni kuwa wao wakati mwingi huwa hawaongelei hilo, matokeo kama anavyosema “Lamence”: “Hakika sisi hatumiliki tafsiri pekee ya Qur`ani Tukufu isiyo na kasoro ndani yake, na iliyokuwa ina uadilifu ni tafsiri kwa lugha ya zamani ya Kilatini ya “Marky” 1691 – 1698 ambayo inategemewa na tafasiri zote zilizokuja baadaye, pasi na tafsiri nyingi kukiri hilo wakati mwingine”.

Ndani ya karne ya kumi na nane, zilitokea tafsiri nyingi pia zenye asili ya Kiarabu, ambapo Muingereza “George Sale” alisambaza moja kwa moja tafsiri kutoka Kiarabu kwenda Kiingereza mwaka 1734 katika utangulizi wake akielezea kuwa Qur`ani Tukufu ni ubunifu wa “Muhammad” na katika utunzi wake na hilo ni jambo lisilokubali mjadala, na Mfaransa “Savary” mwaka 1751 alitoa tafsiri ya moja kwa moja ya Kifaransa, ilipata heshima ya kuchapishwa huko Makka mwaka 1765H, hata Edward Montel anasema kuwa: “Pamoja na tafsiri ya Savary imechapishwa mara nyingi na ya kifahari sana lakini usahihi wake ni mdogo”, mwaka 1840 ilipatikana tena tafsiri ya “Kzimmersky” ambayo inazingatiwa – kwa kulinganisha na tafsiri ya Savary – ni yenye kutumika sana pamoja na yenyewe inakosa uadilifu wa kielimu na ufahamu wa balagha ya Kiarabu, Monte anasema kuhusu tafsiri hii: “Hatuna zaidi ya kuisifu, kwani yenyewe imeenea sehemu nyingi sana ndani ya nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa”.

Mwaka 1925 tafsiri ya “Edward Monte” ambayo ilikuwa na sifa ya udhibiti na usahihi, na ambayo Mwalimu “Muhammad Fuad AbdulBaqi” ameizungumzia kwa alichosema: “Nilikuwa napitia makala ya Amir “Shakib Arslan” kwenye jarida la Al-Manal kuhusu tafsiri mpya ya Qur`ani Tukufu kwa lugha ya Kifaransa iliyotengenezwa na Mwalimu “Edward Monte” na amesema: Yenyewe ni tafsiri ya kina zaidi katika tafsiri zilizopo mpaka hivi sasa, kwani amenukuu utangulizi wa Kiarabu kwenye tafsiri hii, nayo ni tafsiri ya historia ya Qur`ani Tukufu na historia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W na imechapishwa kwenye jarida la Manar, nilinunua tafsiri hii na nikakuta amefikia lengo katika usahihi na ukina na mfasiri ameimalizia kwa faharasa za uchambuzi wa kina mada za Qur`ani Tukufu”.

Na katika mwaka wa 1949 ikajitokeza tafsiri ya “Blasher” ambayo ndani yake kunapatikana Sura zilizopangiliwa sawa na mtiririko wa kihistoria, “Dr.Subhi Saleh” anasema: “Tafsiri ya Qur`ani Tukufu ya Blasher kwa mtazamo wetu itaendelea kuwa ni katika tafsiri sahihi zaidi kielimu ambayo kasoro yake pekee ni mpangilio  wakati wa Sura za Qur`ani Tukufu”.

Na sifa muhimu iliyonayo tafsiri hii ya “Blasher” ni kutumia njia sahihi ya kiuchapishaji, na kuambatisha tafsiri na baadhi ya maelezo na ufafanuzi, na mara nyingi Aya moja inakuja na tafsiri mbili moja wapo inabainisha maana ya mfano na Aya nyingine inaleta maana ya kukisia, na mara nyingi huegemea kwenye maana ya kukisia, na hii ndio imefanya tafsiri nyingi kwa lugha ya Kifaransa kuenea zaidi na kuhitajika, katika kitabu cha “Islamologie” imekuja kuwa: “Yenye kuhitajika katika mkusanyiko wa tafsiri hizi ni tafsiri ya Muingereza “Bill” na tafsiri ya Mfaransa “Blesher” na tafsiri ya Mtaliano “Bosni””.

Inaonekana kuwa “Jack Burke” ana mtazamo tafauti kuhusu tafsiri hii, ambapo anasema: “Tafsiri ya Blasher ina sifa nyingi, kwani yeye ni katika Mustashriki bora wa Ulaya katika sarufi ya lugha ya Kiarabu na fasihi zake, lakini miongoni mwa mapungufu yake ni kuwa mtu wa kisekula, kwa maana hakuwa na uwezo wa kufahamu madhumuni ya kiroho ya Qur`ani Tukufu na pande zake za kisufi, wala hakuna shaka kuwa Blasher ni Mwalimu mkubwa, kwani amekuwa Mwalimu kwangu na rafiki mkubwa, lakini lau tutazungumza kama Wanachuoni mbali kabisa na mahusiano maalum basi mimi ninasema: Hakika tafsiri yake ya Qur`ani Tukufu – pamoja na sifa zilizopo – ina mapungufu yake, lakini yenyewe itabakia kuwa tafsiri bora ya Qur`ani Tukufu kwa lugha ya Kifaransa”.

Mwaka 1966, ikatokea tafsiri ya Mustashriki wa Kijerumani “'Rudi Bart'” na inazingatiwa ni katika tafsiri ya Qurani Tukufu nzuri kwa lugha ya Kijerumani, bali huenda kwa lugha zote za Ulaya kwa wakati huo, kwani mwenye tafsiri amezingatia zaidi kazi zake ziwe za kielimu, na kuwa karibu zaidi na usahihi na uadilifu katika kunukuu maana ya Qur`ani Tukufu kutoka lugha ya Kiarabu kwenda  lugha ya Kijerumani, mpaka yeye pindi anapokutana na neno linamletea shida kulifahamu kwa sura inayokusudiwa au kutojiridhisha na uwezo wake wa kubaini maana yake kwa lugha ya Kijerumani, basi hulithibitisha kwa lugha ya Kiarabu kama lilivyokuja ndani ya Aya Tukufu lakini kwa herufi za Kilatini ili kutoa nafasi kwa msomaji kuunganisha yeye mwenyewe na kumpa maana ambayo anaona inakubaliana na muundo wa maneno pasi ya kulazimisha mtazamo wa mtu.

Baada ya kupita wakati kama Bousquet anavyosema, hakuna tafsiri mpya ya Quran Tukufu nchini Ufaransa iliyopewa uzito pamoja na kuwepo kwa tafsiri nyingi zilizofurika kwenye soko la Ufaransa kipindi cha kati kati ya nusu ya pili ya karne ya ishirini mpaka mwaka 1990 “Jack Burke” alipotoa tafsiri ambayo ilimchukuwa miaka minane mfululizo kufanikisha kazi hii, akitumia kwa msaada tafsiri kumi, ya kwanza ni tafsiri ya Imamu “Twabary” na tafsiri ya “Zamakhshary” miongoni mwa tafsiri za zamani, na tafsiri ya “Muhammad Jamaldeen Al-Qasimy” katika tafsiri za sasa, miongoni mwa sifa za kipekee kwenye tafsiri hii ni ule utangulizi ambao “Burke” ameutumia kuchambua andiko la Qur`ani Tukufu na sifa zake pamoja na madhumuni yake na umaalumu wake ambao  unao, lakini pamoja na hisia kubwa iliyoletwa na tafsiri hii ndani ya Ufaransa na kuzingatiwa wakati huo tukio kubwa la kielimu, lakini mwenyewe anaona kuwa tafsiri yake haitafikia hatua ya ukamilifu, bali itakuwa yenye kuwaelekea Waislamu ambao uwezo wao mdogo wa lugha ya Kiarabu, na wana uwezo mzuri kwenye lugha ya Kifaransa.

Hizi ndio tafsiri muhimu za Qur`ani Tukufu kwa lugha mbalimbali za watu wa Ulaya, na kuna tafsiri zingine nyingi sehemu hii haitoshi kuelezea zote.

Matokeo kama “Lamence” anavyosema: “Hakika sisi hatumiliki tafsiri nzuri ya Qur`ani Tukufu isiyo na kasoro” na sababu ni kuwa Wafasiri wa Qurani Tukufu:

Hawajajaribu kufahamu Maandiko ya Qur`ani Tukufu kabla ya vitu vyote, kama inavyotaka hivyo kanuni ya elimu ya tafsiri, bali wao wamedondokea bila kusita katika kutafuta maana za maneno.

Hawakumaanisha maana za Aya wala maana za maneno.

Hawakuwa na uwezo wa kina wa elimu ya sarufi wala elimu ya balagha ili kufahamu maneno ya kuazima wala ufupishaji wa maneno.

Kutojali sababu za kuteremka.

Kutokuwa na uangalifu na maelezo ya hukumu za kifiqhi na zingine miongoni mwa hukumu zilizopo ndani ya Aya.

Kutokuwa na baadhi ya nyenzo muhimu ambazo zinasaidia kufahamu Aya za Qurani kama Nassi za Hadithi.

Na mwisho, tafsiri zao zilikuwa huru zaidi ya inavyopaswa, jambo lilopelekea tafsiri nyingi kujifunga kimaana kwa msomaji, kuongezea kukosa mvuto na kuathiri, R. Aznaldez anasema: “Tafsiri za Kirafansa ni kama tafsiri zingine za Qur`ani Tukufu vyovyote itakavyokuwa aina zake udhibiti wake ukubwa wa muundo wake lakini hazina athari ndani ya moyo wa asiye Muislamu, kama Qur`ani Tukufu pekee inavyoathiri ndani ya mioyo ya Wacha-Mungu”.

Kisha tukio kubwa likatokea wakati Kamaliyun walipodondosha utawala wa Kiislamu (1343H, 1924), kisha wakafanya kazi ya kuondoa na kufuta lugha ya Kiarabu, na watu kulazimishwa kusoma Qur`ani Tukufu kwa lugha ya Kituruki, bunge la wakati huo likaagiza “Kamati ya mambo ya dini” kutafsiri Qurani Tukufu kwenye lugha ya Kituruki” ([8]).

Baadhi ya wapagani wa Kituruki walisambaza chuki kwa watu wao, lakini waliwasha moto na wakataka kuachana na Qur`ani Tukufu iliyoteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa lugha ya Kiarabu na kuitafsiri kwenye lugha ya Kituruki.

Lengo lao lilikuwa ni kuondoa kila kilicho cha Kiarabu kwa raia wa Kituruki ili kurahisisha kujitoa kwenye Uislamu, pindi walipo tafsiri Qur`ani Tukufu kwa lugha ya Kituruki si kwa lengo la kufahamika na Waturuki kwani tafsiri kwa lugha yao zilikuwa nyingi lakini walifuta kila iliyokuwa ya Kiarabu ([9]).

Na kwakufuata hilo Wahindi nao walitafsiri Qur`ani Tukufu kwenye lugha ya Kiingereza, kama walivyoitafsiri kwenye lugha ya Urdu ([10]).

Yaliungwa mkono na mustashrikina yaliyotokea katika kazi za kutafsiri Qur`ani Tukufu na yaliyogundulika katika tafsiri hizi ikiwa ni pamoja na upotoshaji, na yale yaliyofanywa na Waturuki wa Al-Kamaliyun na kuleta kimbunga kikubwa ndani ya ulimwengu wa Kiislamu, tafsiri ikaleta vita vikali kati ya wanaounga mkono na wanaopinga pamoja na wahafidhina, kila kundi likaja na hoja yake na kila upande ukawa unajibu upande mwengine kwa kutumia vitabu barua magazetu na majarida na hasa hasa nchini Misri, hayo yalikuwa ndani ya nusu ya kwanza ya karne iliyopita Hijry.

Vita hivi vilianza kwa mfululizo wa makala kati ya wanaokubali fikra ya kutafsiri Qur`ani Tukufu ambapo Mwalimu Muhammad Farid Wajdi alianza kutoa makala ndani ya magazeti mawili ya Al-Ahram na Mukattam pamoja na kutoa maelezo yake ya kukubaliana na yaliyofanywa na Waturuki nchini kwao, makala hizi zilisahihishwa na kuhaririwa na baada ya hapo propaganda za Kituruki ziliondolewa, kisha baada ya miaka makala hizi zikachapwa kwenye barua huru kwa anuwani “Dalili za kielimu za kufaa kutafsiri maana ya Qurani  Tukufu kwenye lugha za kigeni” vile vile Sheikh Muhammad Mustafa Al-Maraghi Sheikh Mkuu wa Al-Azhar wakati huo alichapisha makala kwenye magazeti ya wiki ya kisiasa ya Al-Ahram akikubaliana na fikra ya kutafsiri Qur`ani Tukufu na akikusanya dalili za Kifiqhi, nazo ni makala ambazo vile vile zilihaririwa na kuchapishwa baada ya mwaka 1932 katika barua huru kwa anuwani “Tafiti katika tafsiri ya Qurani Tukufu na hukumu zake” kisha mwaka 1936 zikachapishwa tena kama ambatisho kwenye jaridu la Al-Azhar, pia Sheikh Abdulrahman Al-Jazairy alikubaliana na kazi hiyo ya tafsiri ya Qur`ani Tukufu na katika hilo akatunga ujumbe kwa anuwani “Ufafanuzi mzuri katika kujibu wale wenye kuzuia tafsiri ya Qur`ani Tukufu” ([11]).

Mtu wa kwanza aliyejibu makala za wanaokubali kwa kutumia magazeti ni Dr. Abulwafaa Attaftazany mwalimu Falsafa ya Kiislamu ([12]) kisha baada ya hapo yakafuata majibu mengi ambayo kwa ukweli yalikuwa na nguvu zaidi na mengi zaidi ya maandishi ya kukubali, miongoni mwa wapingaji wa aina ya tafsiri ambayo inatakiwa na wanaopitisha ni Sheikh Muhammad Hasanain Makhluf ambaye katika hilo aliandika utafiti kwa anuwani: “Hukumu ya tafsiri ya Qurani Tukufu na kuisoma kwake kuiandika kwake kinyume na lugha ya Kiarabu” ([13]), na Sheikh Muhammad Rashidi Ridha, katika hilo aliandika makala ikiwemo na tafsiri ya Al-Manal ([14]) kama alivyoandika kitabu chake “Tafsiri ya Qur`ani Tukufu na ubaya uliomo”, mwengine ni Sheikh Muhammad Shakir  naibu rais  wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar aliandika tafiti kwa anuwani “Kauli ya upambanuzi katika tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa lugha za kigeni”, na Sheikh Muhammad Bakhit Al-Mutwii Mufti wa Misri aliandika kitabu “Hoja ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake katika kubainisha ukweli wa Qur`ani Tukufu na hukumu za kuandikwa kwake na kutafsiriwa” ([15]), miongoni mwao pia ni Sheikh Muhammad Sulaiman, Mjumbe wa Mahakama kuu, alitunga kitabu chake “Yametokea matukio katika Uislamu kutangulia kutafsiri Qur`ani Tukufu” ([16]), na Sheikh Mustafa Shatwir katika waraka wake ambao aliufikisha kwa Sheikh Mkuu wa Al-Azhar ambao ulibeba anuwani “Ukumbusho wa kwanza maono na mitazamo juu ya hatari iliyopo kwenye tafsiri ya maana ya Qur`ani Tukufu i”[17], kisha katika kitabu chake “Kauli sahihi katika hukumu ya tafsiri ya Qurani Tukufu”[18], vile vile Mwalimu Muhammad Al-Hahayawi katika kitabu chake “Tafsiri ya Qur`ani Tukufu lengo la kisiasa na fitina katika dini” ([19]), pembezoni mwa Sheikh Al-Islamu wakati wa utawala wa Al-Otham, Sheikh Mustafa Swabry ambaye alitengeneza dibaji kwenye hicho kitabu chake chenye kuzuia tafsiri ya Qur`ani Tukufu “Masuala ya tafsiri ya Qur`ani Tukufu”[20] ambacho kinazingatiwa ni katika kitabu kilichokusanya yote ya mlango huu, hii vile vile kutoeleza kwake maudhui ndani ya kitabu chake “Msimamo wa akili elimu na ulimwengu kutoka kwa Mola wa viumbe” pamoja na makala nyingi ambazo zilichapishwa katika magazeti na majarida yaliyotolewa wakati huo ([21]).

Maudhui iliendelea bila kufikia ufumbuzi, tafsri ziliendelea kwa aina zake pamoja na kuwa na kasoro, na idadi ilifikia inayoweza kuhesabiwa kutoka lugha ambazo zilitumiwa na Waislamu katika kutafsiri au kujaribu kutafsiri maana za Qur`ani Tukufu kiasi cha lugha “124”, idadi hii ni pamoja na baadhi ya lugha ambazo zinatumiwa na Waislamu, ambapo kuna Waislamu wanazo tafsiri zilizochapishwa kwa lugha zao, na baadhi ya Waislamu Barani Afrika wana tafsiri zilizonukuliwa kwa maelezo.

Sura ya Kwanza

Tafsiri ya Qur`ani Tukufu ufafanuzi na vidhibiti.

Sura hili inakusanya sehemu tatu:

Sehemu ya Kwanza: Misingi ya lugha ya Kiarabu ambayo Qur`ani Tukufu imeteremka kwa lugha hiyo.

Sehemu ya Pili: Maana ya neno (Tafsiri) pamoja na mkusanyiko wa vidhibiti.

Nayo ina milango Mitatu:

Mlango wa Kwanza: Maana ya tafsiri kwa upande wa lugha na istilahi.

Mlango wa Pili: Aina za tafsiri.

Mlango wa Tatu: Yaliyolazima katika tafsiri kama kazi ya ujuzi.

Sehemu ya Tatu: Maana ya (Qur`ani Tukufu).

Nayo ina milango Miwili:

Mlango wa Kwanza: Ufafanuzi wa neno (Qur`ani) na maana zake.

Mlango wa Pili: Makusudio ya Qur`ani Tukufu.

Sehemu ya Kwanza: Misingi ya Lugha ya Kiarabu iliyoshuka na Qur’ani Tukufu

Hakuna katika umma zote uma uliopewa nguvu ya maneno ubainifu mawanda mapana kama ulivyopewa umma wa Kiarabu, yote hayo ilikuwa ni kutilia mkazo kuletwa kwa Mtume S.A.W,  Kitabu hiki kimekuwa ni dalili ya wazi ya Utume wake, kama ilivyofanywa alama kwa kila Nabii aliyeletwa miongoni mwa mambo yanayofanana na wakati wake aliotumwa, kwa mfano Nabii “Musa A.S” ilikuwa ni “Kuachana kwa bahari, mkono, fimbo, kupasuka mawe, na alama zake zingine za zama za uchawi.

Na Nabii “Issa A.S” ilikuwa ni kufufua wafu, kutengeneza ndege kutokana na udongo, kuponya wagonjwa wa mbaranga na ukoma kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu, na alama zingine za zama za tiba.

Na Nabii “Muhammad S.A.W” alama yake ni Kitabu hiki ambacho lau watakusanyika wanadamu na majini ili watunge mfano wa maneno ya Kitabu hiki basi hawataweza, hata kama watasaidiana wao kwa wao, na alama zingine za zama za ubainifu ([22]).

Qur`ani Tukufu imeteremshwa kwa lugha ya Kiarabu. Mwenyezi Mungu Amelitaja hilo sehemu nyingi ndani ya Kiatabu chake, Akasema: 

{Hakika Sisi tumeiteremsha Qur`ani kwa Kiarabu ili mpate kuzingatia} Yusuf: 2.

{Na ndio kama hivi tumeiteremsha Qur`ani kuwa ni hukumu kwa lugha ya Kiarabu} Al-Raad: 37. {Na namna hivi tumeiteremsha Qur`ani kwa Kiarabu}Twaha: 113.

{Ameuteremsha Roho Muaminifu * Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji * Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi} Al-Shuaraa: 193 - 195.

{Qur`ani ya Kiarabu isiyo na upogo, ili wamche-Mungu} Al-Zumar: 28.

{Hichi ni Kitabu kilicho pambanuliwa Aya zake, cha kusomwa kwa Kiarabu kwa watu wanao jua} Fussilat: 3.

{Na namna hivi tumekufunulia Qur`ani kwa Kiarabu} Al-Shuuraa: 7.

{Hakika Sisi tumeifanya Qur`ani kwa Kiarabu ili mfahamu} Al-Zukhrufu:  3.

{Na hichi ni Kitabu cha kusadikisha na kilicho kuja kwa lugha ya Kiarabu} Al-Ahqaf: 12.

Isipokuwa Mwenyezi Mungu anakanusha lugha nyengine yeyote Anasema:

{Na Sisi hakika tunajua kwamba wanasema: Yuko mtu anaye mfundisha. Lugha ya huyo wanaye muelekezea ni ya kigeni, na hii ni lugha ya Kiarabu cha wazi} Al-Nahli: 103. “Jambo linaloonesha kuwa Yeye ni Muarabu na kwa lugha ya Kiarabu na wala Yeye si mgeni wala lugha ya kigeni, mwenye kutaka kuifahamu Qur`ani Tukufu basi kwa  lugha ya Kiarabu atafahamu, na wala hakuna njia ya kutaka kuifahamu isiyokuwa njia hii” ([23]).

Mazungumzo kuhusu misingi ya lugha ya Kiarabu na ufafanuzi wa yaliyomo miongoni mwa uzuri wa maneno na maana nafasi haitoshi kwenye tafiti kama hii kutokana na uwingi wake bali tutaelezea maelezo mafupi ya haraka haraka.

Msingi mkubwa wa lugha hii ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ameichagua kuwa ndio lugha ya ujumbe wa mwisho wa dunia nzima wenye kufuta baadhi ya jumbe ziliotangulia:  {Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi} Al-Shuaraa: 195. Kitabu hiki akakifanya muujiza: {Sema: Wangeli kusanyika watu na majini ili walete mfano wa hii Qur`ani basi hawaleti mfano wake, hata wakisaidiana wao kwa wao} Al-Israa: 88. Na kuna mfungamano kati ya muujiza na lugha ya ambayo imeteremshiwa ([24]).

Lugha ya Kiarabu ina misingi katika maneno yake muundo wake na mfumo wake, kwa upande wa maneno kuna maneno ya visawe maneno yanayoshirikiana na meneno ya kinyume, Ahmad Ibn Faris anasema: “Ikiwa utataka lugha zengine zibainishe ubainifu kama wa lugha ya Kiarabu hili ni kosa, kwa sababu sisi lau tutajenga hoja ya kuelezea kuhusu upanga na sifa zake kwa lugha ya Kiajemi basi hatutaweza kufanya hivyo isipokuwa tutataja kwa jina moja, na sisi tunalitaja panga katika lugha ya Kiarabu kwa sifa nyingi, vile vile mnyama kama simba farasi na wingine ni miongoni mwa vitu vinavyoitwa kwa majina ya visawe, basi haya utayapata wapi kwenye lugha hizo? Na lugha zingine zina upana wa kiasi gani kuzidi upana wa lugha ya Kiarabu?” ([25]).

Tatizo ambalo anakutana nalo mfasiri ni kuwa hakuna maneno ya visawe kwa sura zote kati ya maneno mawili, bali ni lazima kuwepo tafauti, kwa mfano: Neno “Al-Swiraatw” na neno “Al-Twariq” na neno “Al-Sabiil” pamoja na kushirikiana katika maana moja kwa maana ya njia au barabara lakini kila moja lina maana zaidi isiyokuwepo kwenye neno lengine kwa mujibu wa sehemu yake kwenye maneno, hivyo mwenye kutafsiri anakutana na ugumu katika kuelezea maana ya ndani ya kila neno ([26]).

Hii ni kwa upande wa maneno, na kwa upande wa muundo na mfumo lugha ya Kiarabu ni pana mno, Ibn Fatibah anasema: “Hakuna katika umma zote umma uliopewa ubainifu na uwanda mpana zaidi ya walivyopewa Waarabu….”  ([27]).

Hivyo unatubainikia ugumu wa tafsiri ya andiko lolote la lugha ya Kiarabu kwenye lugha zingine, basi ni vipi ikiwa neno hili ndio Qur`ani Tukufu?

Kwa mtazamo huu inapaswa kuwepo muelekeo wenye nguvu wa kueneza lugha ya Kiarabu kati ya Waislamu wasio Waarabu ili kuzidisha juhudi za tafsiri, kwani huu ndio ufumbuzi wa kivitendo ([28]).

Sehemu ya Pili: Maana ya Neno “Tafsiri” na Vidhibiti Vikuu.

Sehemu hii ina milango Mitatu:

Mlango wa Kwanza: Maana ya tafsiri kwa upande wa lugha na kimsamiati.

Mlango wa Pili: Vigawanyo vya tafsiri.

Mlango wa Tatu: Yaliyo lazima kwenye tafsiri kama kazi ya kiufundi.

Mlango wa Kwanza: Maana ya tafsiri kwa upande wa lugha na kimsamiati.

Maana ya tafsiri kwa upande wa lugha:

Al-Jawhary anasema: Husemwa ametafsiri maneno yake: Pindi anapo yatafsiri kwa lugha nyengine, na kwa neno hilo kunapatikana jina la mtafsiri, na uwingi wake ni watafsiri ([29]).

Na Al-Zamakhshary amesema: Kila kitu kilichotafsiriwa hali yake hiyo ni tafsiri yake.

Na katika kamusi ya : Al-Turjuman wa Al-Tarjaman: Mfasiri wa lugha, naye ni ambaye hutafsiri maneno kwa maana hunukuu kutoka lugha moja kwenda lugha nyengine ([30]).

Akasema Ibn Junay, ama mfsiri ameelezwa kwa herufi ya kwanza ya Kiarabu ya kuwekwa silabi ya dhuma mwanzo wake ([31]).

Kwa kuzingatia maneno ya watu wa lugha tunakuta kuwa “Tafsiri” katika lugha inaweza kuitwa kwa maana nyingi:

Huitwa na kukusudiwa tafsiri na ufafanuzi wa maneno kwa lugha yake, na pia yaliyosemwa na Ibn Abbas: Ni mfsiri wa Qur`ani Tukufu.

Hukusudiwa vile vile tafsiri ya maneno kwa lugha isiyokuwa lugha yake, na pia yaliyonukuliwa kutoka lugha kwenda lugha nyingine ([32]), kama mwenye kamusi alivyotaja.

Kwa maana hii “Fulani ametafsiri” ni pindi anapotaja tafsiri yake, na tafsiri ya fulani: Ametaja historia yake na maisha yake, na akaashiria kwenye kamusi ya “Al-Wasitwu” kuwa kilichozalishwa ([33]).

Kana kwamba asili ya neno inarejea kwenye ufafanuzi, hivyo huitwa kila chenye ufafanuzi ndani yake, husemwa: Ufafanuzi wa mlango huu ni hivi, kwa maana anuwani yake ([34]).

Maana ya tafsiri kimsamiati na mazoea:

Maana ya pili ya tafsiri ya kimazoea imekuwa kana kwamba makusudio ya maana wakati wa kuitwa, kumekuwa na maelezo mengi ya Wanachuoni kimsamiati katika udhibiti wa maana ya tafsiri na ambayo yote yanazunguka kuhusu maana hii, kwa kutafautiana masharti na maneno yanayoingizwa katika ufafanuzi, huenda maneno mazuri katika ufafanuzi wake ni: “Kuhamisha maneno kutoka lugha kwenda lugha nyingine na kutimiza maana na madhumuni yote ya asili”.

Na baadhi yao wanasema: “Kuelezea maana ya maneno katika lugha kwa maneno mengine kutoka lugha nyingine na kutimiza maana na madhumuni yote ya asili”, hivyo kunukuu au kuelezea kunakuwa ndio kanuni kuu na vipengele vyingne vinavyokuja vinakuwa ni ufafanuzi.

Kauli yao katika ufafanuzi wa pili: “Kuhusu maana ya maneno” huondoa maelezo kuhusu maana iliyopo wakati inapotoka kwa mara ya kwanza katika sura ya tamko.

Na kauli yao: “Kutoka lugha nyingine” huondoa tafsiri kwa lugha asilia na huondoa pia maelezo ya kisawe sehemu ya kisawe au maneno badala ya maneno mengine yanayofanana nayo kwa upande usio na tafsiri na lugha moja sehemu zote.

Na kauli yao “Pamoja na kutimiza asili ya maana na makusudio” huondoa tafsiri ya maneno kwa lugha isiyokuwa lugha yake, kwani tafsari haina sharti la utimizaji wa asili ya maana zote na makusudio, bali inatosha kubainisha hata kwa upande mmoja ([35]).

Huenda mwenye kusema: “Kunukuu maneno” ameangalia tafsiri ya neno kwa neno, na mwenye kusema: “Kuelezea maana ya maneno” ameangalia tafsiri ya kimaana.

Mlango wa Pili: Vigawanyo vya tafsiri.

Wakati wa kuzingatia vigawanyo vya tafsiri ambavyo vimetajwa na Watafiti, tunakuta kuwa mgawanyo wa kijitihada na kuwa kuna muingiliano kati ya vigawanyo, huenda miongoni mwa sababu ya hilo ni kukosekana undani katika kuainisha udhibiti wa kila sehemu, na kusudio lake, hakuna shaka kuwa kuingiliana huku ndio sababu ya matatizo wakati wa kutaja hukumu za tafsiri, huenda vigawanyo vingi ni vilivyotajwa kwenye baadhi ya vitabu katika masuala haya ([36]), ambapo sehemu ya tafsiri kwa mazingatio yaliyopita yanagawanyika sehemu tatu. Nazo: 

Tafsiri ya neno kwa neno la mfano: Baadhi yao huita tafsiri ya neno, na maana yake: Kutafsiriwa mfumo wa Qur`ani Tukufu kwa lugha nyingine kwa usimulizi, ambapo nafasi ya neno umoja huchukuwa nafasi ya neno la umoja, na mtindo wa tafsiri huchukuwa nafasi ya mtindo mwingine, na mafasiri hukusudia asili ya kila neno analifahamu na hulibadilisha kwa neno linalolingana nalo ndani ya lugha inayotafsiriwa, pamoja na hilo hupelekea kujificha asili ya maana inayokusudiwa kwa sababu ya tafauti za lugha mbili kwenye matumizi ya maneno katika maana inayokusudiwa ([37]).

Tafsiri hii inakaribia kuwa muhali, kwa sababu mpaka iwezekane lazima mambo kuwepo mawili:

Kuwepo maneno katika lugha inayotafsiriwa kuelekea yaliyosawa na maneno katika lugha inayotafsiriwa ili iwezekane asili ya kila neno katika tafsiri kuchukuwa nafasi ya mwenzake katika asili.

Kufanana lugha mbili katika dhamiri na viunganishi vya maneno na visivyokuwa hivyo miongoni mwa vinavyounda mpangilio ([38]).

Masharti haya mawili magumu kwenye kutafsiri maneno ya watu, ni vipi Qur`ani Tukufu maneno ya Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe, hivyo imehukumiwa kuwa ni muhali kutafsiri neno kwa neno la mfano kwenye Qur`ani Tukufu ([39]).

Tafsiri ya neno kwa neno si mfano wake: Nayo ni kutafsiri mfumo wa Qur`ani Tukufu kwa kiasi cha nguvu ya mafsiri, wala halazimiani neno sawa na neno bali la muhimu kwa mafsiri miundo na sura nzuri ya maana na lengo ([40]).

Sura ya tafauti ya hii na iliyopita “neno kwa neno la mfano” ni kuwa ya kwanza mafsiri analazimika kutumia neno sehemu ya neno, wala haangalii maana, wakati aina ya pili “Neno kwa neno si mfano wake” mafsiri huangalia maana lakini kwa mujibu mfumo wa Qur`ani Tukufu na utarataibu wake pasi ya kuongeza au kufafanua, kusudio lake si kubainisha na kutafsiri kama ilivyo kwenye tafsiri ya maana ifuatayo.

Tafsiri ya ufafanuzi au “Tafsiri ya maana ya Qur`ani Tukufu” ukweli wa tafsiri hii yenyewe ni sherehe na ufafanuzi wa maana ya Qur`ani Tukufu kwa lugha nyingine, pasi ya kulinda mfumo asili na utaratibu wake, kwani mafsiri anafanya kazi ya kusherehesha maana ya Qur`ani Tukufu na kufafanua, pamoja na kuweka wazi jumla zake, kuchimbua hukumu, kuelekeza maana, kutaja sababu na hali za kuteremka, na yasiyokuwa hayo miongoni mwa maana ambazo anazikusudia mfasiri ([41]). Urefu wake na ufupi wake unakuwa kwa mujibu wa mfumo wa mwenye kufasiri na wala hakuna uhusiano na mfumo uliopo, anaweza kufasiri Aya katika kurasa nyingi, na anaweza kuzifasiri kwenye maneno machache, na tafasiri hii baadhi yao huita “Tafasiri ya ufafanuzi” na wengine wanaita “Tafasiri ya maana ya Qur`ani Tukufu” hakuna mvutano kwenye msamiati na jina ikiwa maana inayokusudiwa imedhibitiwa. Na bora zaidi katika kuitwa mfano wa tafsiri hii “Tafsiri ya ufafanuzi wa Qur`ani Tukufu” au “Tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa lugha fulani” ili kuwekwa mbali na mkanganyiko, wala haifai kuita tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa upande wa kilugha kwa jina hili kutokana na tulichofahamu kuwa neno tafsiri ya Qur`ani Tukufu linashirikiana kati ya maana nyingi, na maana inayokuja haraka kwenye akili wakati inapoitwa si yenye kukusudiwa.

Hapa ni lazima tubaini tafauti kati ya “Tafsiri ya maana” na “Tafsiri ya neno kwa neno si la mfano wake” ambapo muingiliano unapatikana kati ya tafsiri hizo mbili kwa baadhi ya Watafiti, na baadhi yao hawatafautishi kati yake na kuzingatia zote ni moja, ukweli ni kuwa kati ya tafsiri hizo mbili kuna tafauti hata ikiwa ni ndogo, na ili kuweka wazi tafauti hii ninasema:

Katika tafsiri ya neno kwa neno “si la mfano” mfasiri huchunga mfumo wa Qur`ani Tukufu na utaratibu wake, kwani mfasiri anataka kuleta ujenzi wa Qur`ani Tukufu uliopangiliwa kwa mujibu wa taratibu zake, kwa lugha ambayo anaitafsiria, huiondoa kwenye asili, lakini halazimiani na maneno kama ilivyo kwenye “neno kwa neno la mfano”, na wala si sherehe na ufafanuzi wa maana kama ilivyo kwenye tafsiri ya maana, na mfasiri katika tafsiri ya maana hana mahusiano na asili ya tafsiri isipokuwa kwa upande sherehe yake na ufafaunuzi wake, yenyewe hujenga asili ya tafsiri sio tafsiri mbadala, na hizi ni baadhi ya tafauti kati ya tafsiri ya neno kwa neno “la mfano” na “lisilo la mfano” na “Tafsiri ya maana” huenda tafauti inatuwia wazi kati ya vigawanyo hivi:

Tafsiri ya neno kwa neno “la mfano” na “si la mfano” ni mfumo huru unaochunga kuachana na asili yake, na kuchukuwa nafasi yake, tafauti na tafsiri ya maana yenyewe ni sherehe na ufafanuzi wa asili wala haisimami mbadala.

Tafsiri ya neno kwa neno “la mfano” na “si lenye mfano” haifai kuondoana kwa sababu ni sura inayotokana na asili, hivyo ni lazima kuwa sawa pasi ya kuongezeka, tafauti na tafsiri ya maana mwenye kufasiri huongeza kwa mujibu wa mfumo katika tafasiri.

Tafsiri ya neno kwa neno, hujumuisha utimizaji wa maana na makusudio ya asili, tafauti na tafsiri ya maana yenyewe inasimama kwenye uwazi kwa njia ya ujumla au ya ufafanuzi, huleta maana yote au baadhi yake, kwa mujibu wa hali ya mfasiri na mwenye kutafsiri ([42]).

Mlango wa Tatu: Yaliyolazima katika tafsiri moja kwa moja.

Ili kufikia tafsiri ya neno kwa neno au tafsiri ya maana lazima yafikiwe mambo mane:

Jambo la Kwanza: Ufahamu wa mfasiri lugha mbili, lugha ya asili na lugha ya tafsiri.

Jambo la Pili: Kufahamu kwake mbinu zake misingi yake fasihi zake na maana zake ([43]).

Jambo la Tatu: Tafsiri kutimiza asili ya maana zote na makusudio kwa sura ya kujiridhisha.

Jambo la Nne: Muundo wa tafsiri uwe unaojitegemea mbali na asili ambapo inawezekana kujitenga na kuchukuwa nafasi yake kana kwamba hakuna asili wala tawi, ufafanuzi wa hilo utakuja katika tafauti kati ya tafsiri na ufafanuzi .

Yaliyolazima katika tafsiri ya neno kwa neno:

 Na tafsiri ya neno kwa neno baada ya mambo haya manne husimama kwenye mambo mawili mengine:

Jambo la Kwanza: Kuwepo maneno katika lugha ya tafsiri yaliyosawa na maneno ambayo asili yanatambulika ili kuwezekana kila neno la tafsiri kuchukuwa nafasi ya neno lengine asili kama ilivyoelezewa katika maana ya tafsiri ya neno kwa neno.

Jambo la Pili: Lugha mbili kufanana katika dhamiri iliyojificha na viunganishi ambavyo vinaunganisha maneno ili kuunda muundo sawa katika mfanano huu, kwa hakika tumeweka sharti hili la kufanana kwa sababu tafsiri hii kuiga asili katika taratibu zake kunahitajika, kisha masharti haya mawili ni magumu na mawili mengine ni magumu zaidi ya masharti ya kwanza, hivyo haiwi kukuta katika lugha tafsiri ya maneno yaliyosawa na maneno yote asili, kisha hakuna mfanano kati ya lugha mbili inayohamishwa na inayohamishiwa katika dhamiri zilizojificha na katika viunganishi kati ya maneno ili kutengeneza miundo ([44]).

Sehemu ya Tatu: Qur.ani Tukufu na Misingi yake.

Nayo ina milango Mitatu:

Mlango wa Kwanza: Kusudio neno Qur`ani.

Mlango wa Pili: Makusudio ya Qur`ani Tukufu.

Mlango wa Kwanza: Kusudio la neno Qur`ani.

Hivi sasa tumemaliza maelezo kuhusu watu wa kwanza kuelezea neno tafsiri ya Qur`ani, tunasimama kisimamo chengine kwa upande wa pili nao ni upande wa Qur`ani yenyewe ili kubainisha hapa makusudio yake na kufahamu aina za maana zake na makusudio yake ikiwa ni maandalizi ya kufikia hukumu sahihi kuwa inawezekana kutafsiriwa neno kwa neno au hapana.

Kusudio la Qur`ani:

Makusudio ya Hapa katika sehemu hii, tafsiri ni matamshi ya kimiujiza si sifa ya zamani sifa ya maneno wala maneno ya kihukimu wala nakshi iliyoandikwa, bali kusudio la Qur`ani lilikuwa kuhusu matamshi ya kimiujiza kwa sababu tafsiri iliongezewa, na ni wazi kuwa tafsiri haizungumzii isipokuwa kilichokuwa matamshi ya kweli yaliyo kwenye sura ya herufi na sauti, wala haizungumzii sifa ya zamani wala maneno ya kihukimu yasiyoonekana wala nakshi zilizoandikwa isipokuwa kwa sehemu ndogo ya maelezo.

Maana ya Qur`ani ni aina mbili:

Kwa vile tafsiri inapaswa kukusanya maana zote asili hivyo ni lazima maneno yeyote yawe na aina mbili za maana, nazo ni: Maana ya asili na maana ya upili,Maana ya asili ya maneno yeyote ni yenye kuleta faida hata yakija kwa mfumo wowote ni sawa sawa hata kwa lugha nyengine, na yameitwa maana ya asaili au maana ya kwanza kwa sababu ni maneno ya kwanza kufahamika, na yameitwa asili kwa sababu ni yenye kuthibiti hayatafautiani kwa kutafautiana wazungumzaji wala wanaozungumzishwa wala lugha ya kuzungumzia bali ni maneno yaliyo sawa yawe ya Kiarabu au ya kigeni au lugha ya mjini au mabedui au kwa mtambuzi au mjinga.

Ama maana ya upili au maana ya pili ni maneno yanayoeleweka kwa kuongeza maana ya maneno ya kwanza, na yameitwa maneno ya pili kwa sababu huchelewa kidogo kufahamika, na yameitwa maneno yanayofuata kwa sababu hubadilika kwa kubadilika yale ya asili, kwani hutafautiana kwa kutafautiana hali za wanaozungumzishwa na kwa kutafautiana uwezo wa wazungumzaji na kwa kutafautiana lahaja na lugha kinyume na ile ya kwanza ([45]). 

Mlango wa  Pili: Makusudio ya Qur`ani Tukufu

Pamoja na kuwa tafsiri kwa kawaida ni lazima izungumzie makusudio yote asili lakini ni lazima tufahamu kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuteremsha Kitabu chake Kitakatifu amekuwa na makusudio makuu matatu ambayo ([46]):

Kuwa ni uongofu kwa watu na majini, ifanye kazi ya kumuunga mkono Mtume S.A.W, na kisomo chake kuwa ibada kwa Mwenyezi Mungu.

Kusudio la Kwanza: Uongofu wa Qur`ani Tukufu

Uongofu wa Qur`ani Tukufu unasifa kuwa ni uongofu kwa wote timilifu na upo wazi.

Ama uongofu kwa wote ni kuwa kwake uongofu kwa wanadamu na majini ndani ya zama zote na maeneo yote. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema:

{Na nimefunuliwa Qur`ani hii ili kwayo nikuonyeni nyinyi na kila inayo mfikia} Al-An’aam: 19. Mola Mtukufu Akasema tena:

{Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilichobarikiwa, chenye kuhakikisha yaliyo tangulia, na ili uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake} Al-An’aam: 92. Mola Mtukufu Akaendelea kusema tena:

{Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote} Al-Aaraaf: 158.

Na katika Aya nyengine Mola Mtukufu Amesema tena:

{Na wakati tulipo waleta kundi la majini kuja kwako kusikiliza Qur`ani. Basi walipo ihudhuria walisema: Sikilizeni! Na ilipo kwisha somwa, walirudi kwa watu wao kwenda kuwaonya * Wakasema: Enyi watu wetu! Sisi tumesikia Kitabu kilicho teremshwa baada ya Musa, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake, na kinacho ongoza kwenye Njia Iliyo Nyooka * Enyi watu wetu! Muitikieni Mwenye kuitia kwa Mwenyezi Mungu, na muaminini, Mwenyezi Mungu atakusameheni, na atakukingeni na adhabu chungu * Na wasio muitikia Muitaji wa Mwenyezi Mungu basi hao hawatashinda katika ardhi, wala hawatakuwa na walinzi mbele yake. Hao wamo katika upotovu ulio wazi} Al-Ahqaf: 29 – 32.

Ama utimilifu wa uongofu huu ni kuwa umekusanya yaliyobora zaidi kufahamika na mwanadamu na kufahamika na historia katika uongofu wa Mwenyezi Mungu kwa watu na kujumuisha kila kinachohitajika na viumbe katika masuala ya imani maadili ibada na mashirikiano kwa aina zake tafauti, na umekusanya kati ya masilahi ya viumbe kwa hivi sasa na baadaye, na kutengeneza uhusiano wa mwanadamu na Mola wake na kwa ulimwengu ambao anaishi na kuwezesha kwa njia bora zaidi kati ya mahitaji ya roho na mwili. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema:

{Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na Magharibi. Bali wema ni wa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali, kwa kupenda kwake, jamaa na mayatima na masikini na wasafiri, na waombao, na katika ugombozi, na akawa anashika Sala, na akatoa Zaka, na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanaovumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; hao ndio walio sadikisha, na hao ndio wajilindao} Al-Baqarah: 177.

Mwenyezi Mungu Mtukufu akaendelea kusema:

{Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliyemcha-Mungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye habari}. Al-Hujraat: 13. Mola akaendelea kusema:

{Enyi mlio amini! Kuleni vizuri tulivyokuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu} Al-Baqarah: 172. Na akasema tena kwenye Aya nyengine:

{Na itakapo kwisha Swala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa} Al-Jumaa: 10. Na Aya nyingine nyingi.

Ama kwa upande wa uwazi wa uongofu huu ni kueleza kwake maelezo mazuri yenye kuathiri na kuwa na njia zote za uwazi na ukinaishi kwa mtindo wa muujiza katika ufikishaji wake na ubainifu wake pamoja na maana nyepesi na ya kina, wepesi wake na kina chake kinategemea kitabu cha ulimwengu kinachozungumza na kuleta mifano inayovutia yenye akili ya kina katika sura nzuri inayoonekana na hukumu zinazozindua akili juu ya uzuri wa Uislamu na utukufu wa Sharia na visa vilivyojaa hekima vinavyoipa imani nguvu yakini na kulea nafsi, fikra na hisia, na kumsukuma mwanadamu kwenye kujitoa na kuyaelekea maendeleo pamoja na kumjengea mustakabali mwema unaomfanya kana kwamba yupo wakati wa hivi sasa macho yanamuona kama mchana wa saa kweupe, mifano ya hayo ndani ya Qur`ani Tukufu ni mingi, itatupelekea kutoka nje ya mada yetu.

Jambo muhimu kufahamu sehemu hii ni kuwa uongofu wa Qur`ani Tukufu miongoni mwake ni pamoja na kunufaika na maana asili ya Qur`ani Tukufu, pia kunufaika na maana zake, ama sehemu ya kwanza ni wazi haihitaji uwakilishi ni sehemu ya makubaliano kati ya wote, ama sehemu ya pili kuna undani uliopelekea baadhi ya watafiti kujenga mjadala, kwani uwazi wake kwa mifano unategemea ufunguzi wa Kitabu Kitukufu:

Miongoni mwake: Kunufaika na adabu ya kuanza na Bismillah katika kila jambo la kuzingatiwa, kuzingatia Mwenyezi Mungu kuanza Kitabu chake na bismillah, na katika ufunguzi wake wa bismillah katika kila Sura isipokuwa Suratul-Tawbah.

Pia: Faida kutaka msaada wa kitu chochote hakutegemewi isipokuwa kwa jina la Mwenyezi Mungu pekee, ikichukuliwa kuongezwa kwenye tamko takatifu sifa ya (Al-rahman Al-rahim) Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

Fahamu kuwa usomaji wa Qur`ani Tukufu na upekee wake unafungamana na maana zake za pili na faida inayopatikana zaidi ya kufungamana na maana zake za msingi na faida inayopatikana kwa mazingatio yaliyoelezwa, kwa vile maana ya msingi ni mzunguko wa peo ndogo, ama maana ya pili ni bahari kubwa yenye mawimbi mengi yanayonesha elimu ya Mwenyezi Mungu na hekima zake pamoja na utukufu wa Kimungu na kuonesha baraka za Mwenyezi Mungu na ufunuo wake kwa wale aliyowapa baraka hizi na funuo hizi miongoni mwa waja wake aliyowachagua na warithi wa Maneno yake na Wanachuoni wanaofanya kazi. Mwenyezi Mungu atujaalie miongoni mwao kwa neema zake na ukarimu wake.

Kusudio la Pili: Muujiza wa Qur`ani Tukufu.

Kusudio la pili la kuteremshwa Qur`ani Tukufu ni kusimama kwenye mdomo wa dunia ikiwa ni alama inayoshuhudia Ujumbe wa Mtume Muhammad S.A.W na ibakie muujiza wa kudumu unaozungumza uongofu na dini ya haki dhidi ya dini zote, na sura za miujiza ya Qur`ani Tukufu ni nyingi sana hapa si sehemu ya kuelezea kwa kina, hapa tunaashiria kuwa ufasaha wake mkubwa ni sura ya wazi katika sura za miujiza, bali hiyo ni sura yake ya wazi zaidi kuwepo kwani kila kiwango cha Aya tatu zinakuwa muujiza hata kama kiwango hiki kitakuwa cha Aya moja ndefu, kwani Mwenyezi Mungu aliwapa changamoto vinara wa lugha kuleta sura ya mfano wa Sura ya Qur`ani Tukufu na Sura fupi sana nayo ni Suratul-Kauthar na Aya zake tatu fupi, ikiwa vinara na magwiji wa lugha katika zama za ustawi wake walishindwa basi wengine ndio wameshindwa zaidi, tumeeleza kuwa ufasaha wa Qur`ani Tukufu unapatikana kutokana na kuwa na umaalum na mazingatio zaidi nao unapita kama mapito ya maji katika kijiti cha kijani au mapito ya roho ndani ya mwili.

Hakuna shaka kuwa kusudio hili kwa makubaliano haliwezi kufanyiwa kazi kwa kutafsiri kwani Qur`ani Tukufu pamoja na kuwa ni muujiza kwa maana nyingi katika jumla zake, isipokuwa yenyewe muujiza wake unazunguka katika Aya zote ikiwa ni pamoja na ufasaha wake umekuja kwa muktadha maalum, na hili kwa makubaliano ya Wasomi haliwezi kunukuliwa kwenda kwenye lugha zengine ([47]).

Kusudio la Tatu: Kusoma Qur`ani Tukufu Ibada.

Kusudio la tatu la kuteremshwa Qur`ani Tukufu: Ni waja kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa kusoma Qur`ani Tukufu na kujiweka karibu kwake pamoja na kuwalipa kwa kule kurudiarudia kusoma maneno yake hata kama msomaji hana ufahamu wa maana yake, ikiwa kusoma kutaendana na ufahamu basi malipo huongezeka juu ya malipo. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:

{Hakika wale wanao soma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakashika Swala, na wakatoa kwa siri na kwa wazi katika tulivyo waruzuku, hao hutaraji biashara isiyo haribika * Ili Yeye awalipe malipo yao kwa ukamilifu, na awazidishie kutokana na fadhila zake. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye shukrani} Fatir: 29 – 30.

Na Mtume S.A.W amesema:

“Mwenye kusoma herufi moja ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu basi anamalipo na malipo ni mara kumi ya mfano wake, sisemi neno Alifu herufi Laam herufi na Miim herufi”[48]

Kisha sifa hii ya Qur`ani Tukufu ni ya pekee, kwani hakuna malipo ya kuisoma tu bali lazima kutafakari na kuzingatia, hata ibada ya swala ambayo ni msingi wa dini mtu hapati thawabu zake isipokuwa kwa kiwango cha mazingatio yake, lakini Qur`ani Tukufu imekuwa na sifa hii ya pekee ya hukumu takatifu na faida kubwa, miongoni mwa faida hizo: 

Kupatikana sababu muhimu katika sababu za kuhifadhi Qur`ani Tukufu na kubakia ikiwa yenye kulindwa kutokewa na mabadiliko na mageuzi ambayo yalifanywa kwenye Vitabu vya Mwenyezi Mungu vilivyotangulia, malipo haya makubwa ambayo Mwenyezi Mungu ameyahidi kwa mwenye kusoma Kitabu chake Kitakatifu hata kama hafahamu maana zake ikiwa ni pamoja na kuwafanya watu kupenda kusoma Qur`ani Tukufu na kuwasukuma kufanya wingi wa kusoma na kuhiifadhi, hakuna shaka kuwa kusomwa sana na kuwepo kwa wasomaji wengi na wenye kuhifadhi kunaifanya Qur`ani Tukufu kuzunguka sana kwenye ndimi za watu na kuwa wazi zaidi kwa watu wa matabaka yote, hapa hakuna yeyote wa kuthubutu kubadilisha chochote ndani ya Qur`ani Tukufu la sivyo atakutana na ushindani mkubwa kutoka kwa wenye kuifahamu Qur`ani Tukufu kama ilivyotokea kwa baadhi ya waliojaribu kufanya uhalifu huu miongoni mwa maadui wa Uislamu.

Kupatikana umoja wa kilugha wa Waislamu unaoimarisha umoja wao wa kidini na kurahisisha njia za maelewano na mashirikiano kati yao hivyo hilo kuimarisha nguvu za safu zao na kuimarisha pia makali yao na kuinua neno lao.

Hiyo ni hekima kubwa ya Mwenyezi Mungu ameidhihirisha kwenye Uislamu kupitia Mtume huyu asiyejua kusoma na kuandika katika zama za zamani miongoni mwa zama za historia na kufanikiwa kukubwa kupitia lugha ya Waarabu kukapatikana mataifa mengi yenye lugha tafauti na kuchimbuka wengi waliowatangulia Waarabu katika elimu za Qur`ani Tukufu na elimu za lugha ya Qur`ani Tukufu.

Msomaji hatua kwa hatua huelekea kwenye mazingatio na kuwongoka kwa uwongofu wa Qur`ani Tukufu kwa njia ya upendo huu na kwa kupitia mfumo huu wenye hekima. Qur`ani Tukufu

Kwani leo mwenye kusoma Qurani hali ya kuwa hafahamu maana zake ataisoma kesho hali ya kuwa mwenye kufahamu maana yake, na mwenye kuisoma kesho akiwa anafahamu maana yake ataifanyia kazi keshokutwa, hivi ndivyo msomaji anahama kutoka daraja kwenda daraja ya juu zaidi mpaka anafika kwenye lengo baada ya huo mwanzo, kila mwenye kupita kwenye mwendo huo atafika, na Mwenyezi Mungu amrehemu, Ibn Atwaa Al-Sakandary pale anaposema katika hekima zake:

“Usiache Qur`ani Tukufu kwa kutojihudhurisha kwako kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu kujisahau kwako mbali na Qur`ani Tukufu ni kubaya zaidi kuliko kujisahau kwako na kuwepo Qur`ani Tukufu kwani huenda ukainuliwa kwa Qur`ani Tukufu pamoja na uwepo wa kujisahau na kuifikia Qur`ani Tukufu kwa umakini, na kutokana na Qur`ani Tukufu kwa umakini na kufikia Qur`ani Tukufu pamoja na kuihudhurisha nafsi, na kutoka Qur`ani Tukufu pamoja na uwepo wa kujihudhurisha na kufikia Qur`ani Tukufu pamoja na kuwepo hali ya kukosekana kujihudhurisha na hilo kwa Mwenyezi Mungu ana nguvu nalo” ([49]). 

Sura ya Pili: Rai katika hukumu ya tafsiri ya Qur`aniTukufu.

Maudhui hii sehemu kuu tatu:

Sehemu ya kwanza: Hukumu ya tafsiri ya neno kwa neno linalofanana.

Sehemu ya Pili: Hukumu ya tafsiri ya neno kwa neno lisilofanana, na inajumuisha milango miwili:

Mlango wa Kwanza: Dalili za wanaopitisha Kisharia na pingamizi zake.

Mlango wa Pili: Dalili za vitendo ambazo zinaonekena ni lazima kwenye hizo tafsiri za neno kwa neno na majibu yake.

Sehemu ya Tatu: Hukumu ya tafsiri ya kimaana.

Inakusanya milaango minne:

Mlango wa Kwanza: Dalili za kufaa tafsiri hii na majibu ya wasiokubaliana nayo na majibu juu ya majibu haya.

Mlango wa Pili: Misingi ambayo inayotarajiwa kwenye tafsiri hizo.

Mlango wa Tatu: Faida za tafsiri kwa maana hii.

Mlango wa Nne: Kuondoa shaka kuhusu tafsiri hii.

Hukumu ya Tafsiri ya Qur`ani Tukufu.

Wakati wa tafiti yetu kuhusu historia ya tafsiri kulitokea vita vikali kati ya kundi la Wanachuoni kuhusu masuala ya tafsiri, na Wanachuoni katika hilo kuna moja ya kauli ya tatu:

Wahalalishaji pasi ya pingamizi, jambo ambalo linaongeza uhalali wa kazi za tafsiri zisizokua sahihi.

Upingaji mkali, unaopelekea kuzuia baadhi ya njia za ufikishaji uwongofu wa Qur`ani Tukufu.

Mfuata mfumo wa kati na kati ambapo hukusanya kati ya usimamizi wa umaalumu wa Qur`ani Tukufu kulinda utukufu wake na kufikisha dini ya Mwenyezi Mungu kwa wanadamu.

Na katika sababu kubwa za mgawanyiko wa mwenendo wa tafiti na kupingana na makutano ya pande za maelezo ni kujisahau sehemu ya mzozo ambayo inapelekea ukanushaji na uthibitishaji kati ya pande mbili katika jambo moja, na kuimarisha juhudi za wenye kutafautiana katika kuthibitisha wakati ambapo hakuna hata mmoja anayepinga kuthibiti kwake, au kukanusha wakati hakuna yeyote anayepinga ukanushaji wake, pindi itakapoondolewa sehemu ya mvutano tunakuta kila mmoja kati yao hukubali ayasemayo mwenzake, hata kama  itatafautiana mivutano na kudhaniwa kati yao kunatafauti, mwisho kabisa jambo hurejeshwa kama ni tafauti tu ya maelezo na wala si tafauti katika mazingatio hata kama wao watakubaliana hatua kwa hatua juu ya mazingatio haya basi maelezo yasingetafautiana na wala kusingezuka kabisa tafauti, hivyo ingilio sahihi la kufahamu hukumu ya Kisharia katika masuala ni kugawa sehemu na vipengele kwa kila sehemu na tafauti iliyopo kati yake.

Sehemu  ya Kwanza: Hukumu ya tafsiri ya neno kwa neno linalofanana.

Baada ya kuzingatia maelezo yaliyotangulia ya maana ya aina hiyo ya tafsiri tunaweza kusema kuwa hukumu ya tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa maana hii ni isiyowezekana kikawaida na Kisharia ([50]), kwa maana kutowezekana kupatikana kwa kawaida na ni haramu Kisharia kuthubutu kujaribu kufanyahivyo.

Katika kutowezekana kwake kwa kawaida tuna njia mbili za dalili:

Njia ya Kwanza: Tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa maana hii inapelekea kutowezekana, na kila kinachopelekea kutowezekana hakiwezekani, na dalili ya kupelekea kutowezekana ni kuwa lazima kufikiwa ukamilifu wa maana za msingi za Qur`ani Tukufu na ile maana ya pili pamoja na kufikiwa makusudio yake yote matatu ya msingi na maana zote hizo mbili haziwezekani. Ama maana ya kwanza: Ni kwa sababu maana ya pili ni yenye vigezo vyake vya juu vya ufasaha na muujiza, na haiwi kwa mwanadamu kufahamu hayo kuongezea pia kuelezea hayo katika maneno yake na kama itakuwa basi muujiza huu hautafikiwa. Ama maana ya pili: Ni kwa vile makusudio ya kwanza ya Qur`ani Tukufu nayo ni kuwa kwake uwongofu ikiwa itawezekana kufikiwa katika tafsiri kwa upande wa kila kinachofahamika miongoni mwa maana asili za Qur`ani Tukufu hilo haliwezekani kufikiwa kwa upande wa kila kinachofahamika miongoni mwa maana za Qur`ani Tukufu kwa sababu ni zenye vigezo vya juu vya muujiza wa ufasaha wake kama ilivyoelezwa.

Vile vile makusudio ya pili ya Qur`ani Tukufu nayo ni kuwa kwake Alama, haiwezekani kufikiwa na maneno ya mwanadamu awe Muarabu au si Muarabu na kama si hivyo basi isingefaa kuwa muujiza.

Haya yanazingatiwa pia kwenye makusudio ya tatu ya Qur`ani Tukufu nayo ni kuwa kisomo chake ni ibada, hivyo haiwezekani kufikiwa kwa tafsiri kwa sababu tafsiri ya Qur`ani Tukufu si Qur`ani Tukufu kabisa, na kisomo chake ibada kwa hakika imekuja katika umaalumu wa Qur`ani Tukufu na maneno yake kwa muundo wake na taratibu zake pasi ya maneno mengine yeyote au miundo mengine hata kama itakuwa ni ya Kiarabu yenye visawe ya asili ya maneno na muundo.

Njia ya pili: Tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa maana hii ni kama mfano wa Qur`ani Tukufu, na kila mfano wa Qur`ani Tukufu haiwezekani, ama kuwa kwake mfano wa Qur`ani Tukufu ni kwamba imekusanya maana zake zote na makusudio yake yote na wala haijaacha kitu, na ukusanyaji wa maana za Qur`ani Tukufu na makusudio yake ni mfano wake kwa maana inafanana, ama kila kinachofanana na Qur`ani Tukufu hakiwezekani kwa sababu Waarabu wameshindwa kuleta mfano wa sura ndogo ya Qurani wakashindwa kuiga na wao wakati huo wakiwa waandamizi wa fasaha na ubainifu na shime kubwa ya kuwa wenye kushinda katika kiwanja hiki, ikiwa hawa kwa hakika wameshindwa moja kwa moja basi inakuwaje kwa wengine miongoni mwa waliochini yao kifasaha na ubainishaji ni wenye kushindwa zaidi.

 Ikiwa wanadamu na majini imethibiti kwao neno kushindwa kuleta mfano wa sura ndogo na fupi sana kama ya Qur`ani Tukufu kwa kutumia lugha yao ya Kiarabu na kushindwa kwao kutaonekana zaidi ikiwa watajaribu kwa kutumia lugha nyengine isiyo ya Kiarabu, kwa sababu kuunganisha lugha katika uandishi kati ya maneno mawili kazi yake ni pamoja na kuweka karibu mfanano ikiwa lugha hizo mbili zenye kuwezekana kutokana na misingi ya ufasaha ni mmoja wakati ambapo imeshindikana na lugha inayoshindanishwa, lakini ikiwa kutatafautiana lugha ya iliyoshindwa na lugha inayoshindanishiwa basi inakuwa ni mbali sana kuwepo mfanano wa kina kwa sababu misingi ya ufasaha kati ya moja ya lugha mbili si misingi hiyo hiyo ya ufasaha katika lugha nyengine, kwani hupatikana misingi hiyo kwenye lugha moja isiyopatikana kwenye lugha nyengine hivyo hupatikana ubora tafauti na ugumu wa kufanana, kwa haya wengi wamezungumza miongoni mwa wanalugha kuwa tafsiri ya kina ya maandiko ya kifasihi katika lugha yeyote ni jambo lisilowezekana na yanayozunguka kwa watu miongoni mwa wanayodhani tafsiri za baadhi ya vitabu vya kifasihi zimejengwa na aina ya usamehevu katika kunukuu maana za asili na malengo yake kwa kukaribiana na wala si kwa uhakika hivyo si tafsiri za kina kama zilivyotafsiri za sayansi sheria na nyaraka zilizopangiliwa zenyewe ni tafsiri za kweli zinazotokana na kunukuu asili ya maana na malengo yake yote kwa uhakika na wala si ukaribu ([51]).   

Dalili ya uharamu Kisharia.

Baada ya kuthibiti kwa kawaida kutowezekana hizo tafsiri hapa tunabainisha uharamu wake kisharia, na hilo ni katika njia nane:

Njia ya Kwanza: Jambo lisilowezekana kwa kawaida limeharamishwa na Uislamu vyovyote litakavyokuwa hata kwa njia ya duwa au maombi, na lolote lisilowezekana iwe tafsiri autafsiri, kwa sababu ni aina ya mambo yasiyo na maana na upotezaji muda na juhudi, na jambo hili limekatazwa kabisa kwa makubaliano ya wanachuoni, kuongezea kwenye hilo kuwa ombi lisilowezekana ni ujinga wa kutojua kanuni za ulimwengu za Mwenyezi Mungu na hekima zake katika kuunganisha sababu na visababishi vyake vya kawaida ikiwa ni huruma kwa waja wake kwa sababu Mwenyezi Mungu kwa watu ni Mpole na Mwingi wa huruma.

Njia ya pili: Jaribio la tafsiri hii kuna madai ya uwezekano wa kupatikana mfano au mifano ya Qur`ani Tukufu, huo ni uwongo wa wazi uliojaa hali ya kutowezekana kwa hilo ([52]).

Njia ya Tatu: Jaribio la tafsiri hii linahamasisha watu kukiacha Kitabu cha Mola wao wakitosheka na kitabu mbadala wakidhania tafsiri yake, na pindi muda unapokuwa mrefu wa tafsiri hizi jina la tafsiri litaondoka na kubakia jina la Qur`ani Tukufu peke yake, na wanasema hii ni Qur`ani Tukufu ya Kiingereza na ile Qur`ani Tukufu ya Kifaransa na mfano wa hayo na kugawa kwa kuita Qur`ani Tukufu tafsiri na mwenye shaka ya hilo basi na aangalie yale yanayofahamika na watu katika vitabu tulivyonavyo vya tafsiri ya vitabu mbalimbali na kuita tafsiri nyingi katika dini elimu fasihi sheria na mifano yake, hivyo ni jambo gani litakalozuia kila nchi katika nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu kuwa na Qur`ani Tukufu yake ya mtindo huu ikiwa tutakubali kauli ya kufaa tafsiri hii, je baada ya hapo tunashaka katika uharamu wa kila kinachopelekea watu kuwaweka mbali na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kugawanyika kwao pamoja na kupotosha kwao katika kuita kwao.

Njia ya Nne: Sisi ikiwa tutafungua mlango wa tafsiri hii potofu kwa hakika watu wataizonga kila umma na kila kundi litafanya kazi ya kutafsiri Qur`ani Tukufu kwa dhana yake na kwa lugha yake fasihi na ya mitaani, na kuzaliwa mengi yasiyo na idadi kutokana na tafsiri hizo nayo hakuna shaka zitakuwa ni zenye kutafautiana kati yake, na tafauti hii itaharibu jengo la Waislamu na kutafautisha mshikamano wao na kuwapa maadui nafasi ya kupata miongoni mwao na kuamsha kati yao fitina isiyo na macho kama vile kuukata usiku wenye giza nene.

Njia ya Tano: Kuwepo kwa tafsiri hizi zenye dhambi kunaondoa nguzo kubwa katika nguzo za uwepo wa Waislamu kijamii kama umma wenye nguvu imara, hilo ni kwa sababu kesho watatosheka na tafsiri hizi kama tulivyosema, na wakati wowote watakapotosheka bila shaka yeyote wataachana na lugha asili pamoja na elimu zake na fasihi zake, historia inaonesha kuwa lugha asili ya Qur`ani Tukufu ni kiunganishi katika viunganishi vyenye nguvu kati yao na kiunganishi hiki kuwa na athari kubwa katika kusaidia na kuimarisha umoja wa umma na kuujenga pale walipokuwa wanasoma Qur`ani Tukufu i yenyewe na wakifundisha kutokana na Qur`ani Tukufu elimu za lugha ya Kiarabu na fasihi zake ili kuleta ufahamu mzuri ili kuhudumia elimu na kuikuza, na kung’arisha anga yake wasomi wengi Waarabu na wasio Waarabu katika kuhudumia Kitabu cha Mwenyezi Mungu na elimu zake, kutokana na hilo lugha ya Kiarabu imekuwa lugha ya Waislamu wote na kiunganishi cha pamoja kati yao kwa mataifa yao mbalimbali na lugha zao za ndani bali imeondoa lugha nyingi za ndani katika lugha hii mpya lugha ya Qur`ani Tukufu.

Na sisi katika zama hizi ambazo tumezongwa na lugha za kigeni na kuwepo vita dhidi ya lugha yetu ya Kiarabu, kwamba vita hii ya kilugha inatusisitiza kukusanya nguvu zetu ili kulinda lugha yetu na kulinda njia za kubakia kwake na kuenea kwake,  njia hizi zikiongozwa na kubakia Qur`ani Tukufu kwenye Kiarabu chake,  na kuzuia kwa wanaofanya kazi ya kutafsiri Qur`ani Tukufu neno kwa neno na yanayopaswa kwetu kuwafanyia ugumu na kutowarahisishia katika kulinganisha tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa maana hii kwa tafsiri nyengine katika kufaa na kuwezekana basi yapo wapi maneno ya mja yaliyoshindwa maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyo muujiza.

Al-Shaafi anasema ndani ya kitabu cha Al-Risaalah: “Kila Muislamu anapaswa kujifunza lugha ya Kiarabu kwa juhudi zake zote mpaka ashuhudie kuwa hakuna mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hakika Muhammad ni mja wake na Mtume wake, na asome Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kutamka utajo wa Mwenyezi Mungu katika mambo aliyolazimishwa miongoni mwa uletaji wa Takbiir na katika aliyoamrishwa miongoni mwa tasbiih na usomaji wa Attahiyyatu na mengine yasiyokuwa hayo, kila elimu inapozidi kwa kutumia lugha ambayo Mwenyezi Mungu ameifanya ndio lugha ya Mtume wa mwisho na kuteremshia Kitabu chake cha mwisho inakuwa ndio bora zaidi kwake” ([53]).

Njia ya Sita: Mwenye kufahamu mifumo ya lugha ya Kiarabu na akafahamu maneno ya ndani kwa kusikia na akawa na ufasaha mzuri wa maneno na ufasaha wake wa juu, atakuwa na uhakika pamoja na uyakini kuwa Qur`ani Tukufu ni ya kipekee katika sura yake na elimu kwa Wasomi katika ubainifu wake, kwa sababu yaliyomo miongoni mwa mifumo ya ufasihi na muziki wa kimatamshi ni jambo lilovuka viwango vyote:

{Lau Qur`ani ingeliendeshewa milima, au kupasuliwa ardhi, au kusemeshewa wafu, (basi ingelikuwa Qur`ani hii). Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu} basi baada ya haya inakuwaje kwa kiumbe kuelezea kwa kutumia tafsiri kuwa ipo sawa na Qur`ani Tukufu au inafafa ([54])?

Sehamu ya Tatu: Hukumu ya tafsiri neno kwa neno lisilofanana.

Aina hii ambayo imekuwa na tafauti na uandishi mwingi kwa hakika imekuwa ikizunguka kwenye hilo na kuwa na hukumu tafauti kwani baadhi wamehalalisha na wengi wamefuata waliowatangulia wao katika kuharamisha.

Aina hii inaweza kutokea na wala si yenye kushindikana kama ile iliyotangulia lakini tafauti katika kufaa kwake na wala si uwezekano wake, nayo ni aina ambayo watu wanaojihusisha na elimu za watu wa Mashariki walijaribu kama ilivyotajwa katika utangulizi wa kihistoria.

Sheikh Al-Maraghy anasema: “Hakuna shaka kuwa tafsiri ya neno kwa neno haina uwezo katika Aya zote za Qur`ani Tukufu, ndio, baadhi ya Aya inawezakana, kutokana na hilo haifai kuswali kwa Aya yeyote iliyotafsiriwa, hata Aya ambayo imetafsiriwa tafsiri ya neno kwa neno” ([55]), na akasema sehemu nyengine: “Na sisi tunatambua kuwa tafsiri ya neno kwa neno ni ngumu ndani ya Qur`ani Tukufu yote, na inawezekana katika Aya nyingi” ([56]).

Ukweli ni kuwa usahihi ni uharamu wa aina hii ya tafsiri kama ile iliyotangulia, na hii ni kauli yenye nguvu kwa ujumla wa dalili na kauli za waliopitisha ni dhaifu, nitataja dalili zao na njia za utoaji wao dalili, kisha namalizia kila dalili na ukosoaji wake pamoja na jibu lake.

Mlango wa Kwanza: Dalili za wanaopitisha Kisharia na upingaji wake.

Wanaopitisha aina hii ya tafsiri wametumia dalili zifuatazo:

Hadithi ya Imamu Bukhary, ambayo ndani yake kuna taarifa ya Mtume S.A.W kutuma barua kwa Mfalme Harqal akiandika: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu” kama ilivyokuja ndani yake:

{Enyi watu wa Kitabu njooni kwenye neno lilosawa….} Aya, hakuna shaka kuwa barua hii ilitafsiriwa kwa mfalme Harqal kwa njia ya tafsiri zake na Mtume S.A.W anafahamu moja kwa moja na kama si hivyo basi asingeituma, hii imeonesha juu ya kukubali kwake Mtume S.A.W tafsiri ya Qur`ani Tukufu ambayo hakuna shaka yenyewe ni tafsiri ya neno kwa neno ya barua.

Ninajibu dalili hii kwa mambo kadhaa:

Jambo la Kwanza: Aya hii na mfano wake miongoni mwa zinazotajwa katika barua ya Mtume S.A.W haikukusudiwa kufikisha mifumo ya Qur`ani Tukufu na kisomo chake kuwa ibada, bali ni nukuu iliyokusudiwa utekelezaji wa maana kusudiwa kwenye sehemu hii.

Jambo la Pili: Maelezo yaliyokuja kwenye barua hii ni mfano wa Qur`ani Tukufu na wala si Aya kamili kwa sababu Aya inaanza na maneno: {Sema Enyi watu wa Kitabu} ndani ya barua imeanza na: “Na nyie watu wa Kitabu” vile vile Aya haina herufi ya “wawu” jambo linaloipa nguvu ni mfano wa Qur`ani Tukufu na si Qur`ani Tukufu ([57]).

Jambo la Tatu: Imamu Bukhary mwenyewe hakukusudia kuileta Hadithi hii kama dalili ya kufaa tafsiri ya Qur`ani Tukufu ya neno kwa neno, ameileta katika mlango uliotafsiriwa “Mlango unaoelezea yanayofaa kutafsiri Taurati na Vitabu vya Mwenyezi Mungu kwa lugha ya Kiarabu na lugha zengine” ([58]) hii ikaonesha kuwa imefahamika kusudio ni tafsiri ya ufafanuzi na wala si tafsiri ya neno kwa neno.

Kutolea dalili kwa maneno ya Imamu Abu Hanifa na majibu yake:

Wamesema kuwa imamu Abu Hanifa na wenzake wamepitisha kwa asiyejua Kiarabu kusoma alichafahamu katika tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa lugha isiyo ya Kiarabu kama vile lugha ya Kifursi inayomuwezesha kusimamisha swala yake, hii ni dalili ya kufaa tafsiri ya Qur`ani Tukufu ya neno kwa neno na kutimia katika swala.

Ukweli ni kuwa mimi sitaki kurefusha kwa kuelezea kauli nyingi katika kubainisha hilo au kujibu ambapo vitabu vingi katika masuala haya vilikuwa umuhimu wake kunasibishwa na dalili hii ikiwa kama dalili au upingaji na mimi ninaona kuwa dalili ya upande huu unaoelezewa na watu wa madhehebu ya Abu Hanifa haifai kuwa dalili kwa mambo kadhaa:

Jambo la Kwanza: Maelezo ya watu wa Abu Hanifa katika hili yalikuwa kwenye lugha ya Kifusri ambayo – kama inavyofahamika – ni lugha iliyokaribu zaidi na lugha ya Kiarabu bali Kiarabu na Kifursi zinagongana kwa kiasi cha 40% ya maneno, hivyo haifai kulinganisha na lugha zengine miongoni mwa lugha hata kama Imamu na wenzake wamepitisha hilo katika lugha ya Kifursi wala isichukuliwe wamepitisha kwenye lugha zengine ambapo wameweka sharti mawili katika tafsiri ambayo inafaa kuswalia:

Neno linalotafsiriwa liwe linafanana na neno lingine kwa upande wa mizani na maana.

Mwenye kuswali kuwa na yakini kwamba anachosoma ni maana hiyo hiyo ya neno la Kiarabu ([59]) na hii haiwezekani kufikiwa zaidi ya lugha ya Kifursi bali na hata katika lugha ya Kifursi ni katika sentensi ndogo ndogo.

Jambo la Pili: Sababu ambayo ameitaja Abu Hanifa ya kutofaa kusoma kwa tafsiri nayo ni: Yenyewe si ya moja kwa moja, kwa kuwezekana kusudio la Mwenyezi Mungu Mtukufu si tafsiri hiyo, na inaweza kuwa ni maneno ya watu ([60]), ninasema: Sababu zote hizi zinafikiwa katika tafsiri kwani haiwezekani kabisa kwa yeyote kudai kuwa maana ya tafsiri ndio kusudio la Mwenyezi Mungu Mtukufu moja kwa moja, wala yenyewe si katika maneno ya watu, kwani mantiki katika hili inapelekea kuwa hukumu ya kusoma kwa kutumia tafsiri inachukuwa hukumu ya kusoma kwa tafsiri kwa kukutana sababu katika hizo.

Kauli ya Abu Hanifa pamoja na maelezo haya bado ni dhaifu inagongana na dalili za wazi pia na Jamhuri ya Maimamu.

Kutokana na udhaifu wa dalili za Abu Hanifa katika masuala haya wengi miongoni mwa watu wake wameongea wazi kuacha kufanyia kazi kauli hii, kama alivyosema Mwanachuoni Abi Al-Laithu Al-Samarkandy, na Kadhi Abi Zaidi Al-Dabuusy pamoja na Sheikh Al-Islaam Al-Marghayaany ([61]).

Wakati wa uhakiki madhehebu ya Abu Hanifa yanatofautina na madhehebu mengine juu ya mtu aliyeingia kwenye Uislamu na wala hajawa na wakati wa kutosha wa kujifunza Qur`ani Tukufu kwa kiasi cha kutosheleza kuswali basi huyo katika muda huo ambao hauzidi siku moja au mbili kunakuwa na tafauti kati ya Abu Hanifa na wengine ([62]).

Mmoja wa Wanachuoni wa madhehebu ya Abu Hanifa anasema: “Ama mwenye kushindwa kusoma Qur`ani Tukufu kwa lugha ya Kiarabu huyo ni kama mjinga kwa sababu hajui kusoma lakini ikiwa itachukuliwa kuwa amekwenda kinyume na akasoma Qur`ani Tukufu kwa lugha nyingine basi katika hilo kuna mapokezi ya aina mbili kusishi na kubatilika na akakubali mwenye kitabu cha Al-Bahri kati ya hayo mawili na kuchukuwa kauli ya kuharibika ikiwa anachokisoma ni kisa au amri au katazo kwa sababu anazungumza maneno na wala si ukumbusho, na kauli ya kutoharibika ikiwa anachosoma ni utajo au upwekeshaji, kwa sababu utajo kwa lugha yeyote hauharibu swala si kwa sababu kusoma kwa tafsiri ya Qur`ani Tukufu kunafaa, kwa hakika kauli imepita kuwa kusoma kwa tafsiri kumezuiliwa Kisharia kwa hali zote” ([63]).

Katika dalili yenye nguvu iliyotolewa na Abu Hanifa ni ile hadithi ya Salman imepokewa kuwa Wafursi walimuandikia Salman R.A wakimtaka awaandikie Suratul-Fatihah kwa lugha ya Kifursi, na walikuwa wanasoma hivyo kwenye swala mpaka pale ndimi zao zikazoea lugha ya Kiarabu ([64]) nayo ni hadithi batili kwa mitazamo mingi:

Mtazamo wa Kwanza: Ni hivi ikiwa imekusudiwa kuwa aliwaandikia tafsiri ya Suratul-Fatihah kwa lugha ya Kifursi basi ni namna gani hilo linakuwa njia ya kulainisha ndimi zao na wao hawakusoma isipokuwa kwa lugha yao? Ikiwa itakusudiwa kuwa aliiandika kwa hati ya Kifursi basi hati ya Kifursi ipo karibu sana na hati ya Kiarabu, pia hakuna uhusiano wa kulainisha ndimi.

Mtazamo wa Pili: Ni kwamba Hadithi hii asili yake haifahamiki pia haufahamiki upokezi wake hivyo haifai kuifanyia kazi.

Mtazamo wa Tatu: Ni kuwa lau ingelikuwa na upokezi basi wangekuwa wengi.

Mtazamo wa Nne: Kumekuwa na tafauti katika tamko la Hadithi, baadhi yake walitafsiri “Suratu- Qur`ani Tukufu Fatihah” na baadhi yao ni Bismillah Rahmani Rahiim, na wengine “Aya ndani ya Qurani”.

Mtazamo wa Tano: Wafursi hawakuingia katika Uislamu isipokuwa ndani ya zama za utawala wa Omar Ibn Khattab R.A basi ni vipi Mtume S.A.W alikubali hilo.

Mtazamo wa Sita: Lau ingekuwa ni sahihi basi Umma usingetafautiana swala kufaa kwa kutumia tafsiri.

Mtazamo wa Saba: Mwenye kuzingatia Hadithi atafahamu kuwa Bismillah yenyewe haikutafsiriwa kwao kikamilifu kwa sababu maneno haya ambayo yamekuja kwenye upokezi yenyewe ni tafsiri ya Bismillah hayakuja na neno sawa na neno la Al-Rahaman, kana kwamba hilo ni kutokana na kushindwa kwa lugha ya Kifursi kuwepo mfano wa Jina hili Tukufu, na hii ni dalili kuwa kusudio la tafsiri hapa ni tafsiri ya kilugha na wala si tafsiri ya mazoea kama upokezi utazingatiwa ni thabiti.

An-Nawawi anasema: Madhehebu yetu ni kuwa haifai kusoma Qur`ani Tukufu bila kutumia lugha ya Kiarabu ni sawa sawa awe na uwezo wa lugha ya Kiarabu au hana uwezo nayo, ni sawa sawa akiwa ndani ya swala au nje ya swala ikiwa atasoma Qur`ani Tukufu ndani ya swala kwa kutumia tafsiri yake badala ya kusoma Qur`ani Tukufu yenyewe basi swala yake haitakubalika ni sawa sawa akisoma vizuri au hapana, haya ndio madhehebu yetu na maelezo hayo Jamhuri ya Wanachuoni wamesema miongoni mwao Imamu Maliki na Ahmad pamoja na Daud, na Abu Hanifa amesema inafaa na swala ni sahihi moja kwa moja, na Abu Yusuf na Muhammad wamesema inafaa kwa asiyeweza na si mwenye kuweza…. Wakajenga hoja – kwa maana ya Jamhuri – kuwa tafsiri ya Qur`ani Tukufu si Qur`ani Tukufu kwa sababu Qur`ani Tukufu ni hii mifumo ya kimuujiza na tafsiri huondoa huu muujiza hivyo haifai, na kama vile shairi tafsiri yake hulitoa kuwa kwake shairi basi vile vile Qur`ani Tukufu, akarahisisha Imamu Al-Haramaini akasema: Nguzo yetu ni kuwa Qurani ni muujiza na kinachozingatiwa katika muujiza wake ni maneno yake….baada ya utangulizi huu tunasema, tafsiri ya Qurani kwa makubaliano ya Waislamu si Qur`ani Tukufu kwani hakuna yeyote anayekwenda kinyume kuwa mwenye kuzungumza kwa maana ya Qur`ani Tukufu kwa lugha ya Kihindi hiyo si Qur`ani Tukufu, na wala alichokitamka si Qur`ani Tukufu na mwenye kwenda kinyume na haya anakuwa ni mpingaji, na kutafsiri shairi la Imruu Qais sio shairi lake basi ni vipi tafsiri ya Qur`ani Tukufu inakuwa Qur`ani Tukufu ([65]).

Na Ahmad Ibn Faris anasema: “Hakuna mtazamo wa kauli ya mwenye kupitisha kusoma Qur`ani Tukufu ndani ya swala yake kwa kutumia lugha ya Kifursi kwa sababu Kifursi ni tafsiri na wala si muujiza, bali Mwenyezi Mungu Mtukufu ameamrisha kusoma Qur`ani Tukufu ya Kiarabu iliyo na muujiza, lau itapitishwa kusoma tafsiri ya Kifursi basi vitabu vya tafsiri na vyengine katika vitabu vya maana za Qur`ani Tukufu kwa matamshi ya Kiarabu vingekuwa ni bora swala kufaa, na hili hakuna yeyote anayelisema” ([66]).

Zarkashy naye amesema: Haifai tafsiri ya Qur`ani Tukufu Qur`ani Tukufu kwa lugha ya Kifursi na lugha zengine bali ni lazima kuisoma kwa asili yake ambayo inaendana na muujiza kwa kukosekana hilo kwenye tafsiri, na kushindikana lugha zengine ubainifu ambao upo zaidi kwenye Kiarabu pasi na lugha zengine, hivyo ikiwa haifai kuisoma kwa tafsiri ya Kiarabu iliyoshindwa kwa mifumo yao basi haitofaa tafsiri kwa lugha zengine,  haya yamedhihirisha kuwa tafauti ya kinachoelezewa kutoka kwa Abi Hanifa kufaa kuisoma kwa lugha ya Kifursi hakifikiwi kwa kukosekana uwezo wa kuleta sura yake ([67]).

Kutole dalili kwa maneno ya Al-Shatwbiy na majibu yake.

  Wakachukuwa dalili kauli ya Al-Shatwbiy katika kitabu cha Al-Muwafaqati ([68]): “Katika lugha ya Waarabu kwa upande wa maneno ni yenye kuonesha maana za mitazamo miwili: Mtazamo wa kwanza, kwa upande wa kuwa ni maneno na ibara zenye kuleta maana moja kwa moja nayo ni dalili ya asili. Mtazamo wa pili: Kwa upande wa kuwa kwake ni maneno na ibara zilizojifunga zenye kuleta maana zenye kuhudumu, nayo ni dalili inayofuata.  Upande wa kwanza: Ndio ambao unashirikisha lugha na kwa upande huo huishia makusudio ya wazungumzaji na wala hahusishi umma bila ya umma mwengine kwani ikiwa katika uwepo kumepatikana kitendo kwa mfano cha Zaidi kusimama kisha mwenye lugha akataka kuelezea kuhusu Zaidi kusimama, kwa upande huu inawezekana katika lugha ya Waarabu kuelezea kuhusu kauli za watu waliotangulia miongoni mwa watu wasio wa lugha ya Kiarabu na kuelezea maneno yao, na inakuja katika lugha ya kigeni kuelezea kauli za Waarabu na kuzizungumzia na hii hakuna tatizo ndani yake.

Ama upande wa pili: Nao ni ambao unahusisha lugha ya Waarabu katika hiyo simulizi na hiyo habari, kwani kila habari katika hali hii inapelekea mambo yenye kuhudumia hiyo habari kwa mujibu wa mtoa habari na muelezewa habari na habari yenyewe hivi sasa na aina za mwenendo wa uwazi kuficha kufanikisha na zisizokuwa hizo” baada ya Shatwiby kusema haya akasema: “Na kwa aina hii ya pili ibara zimetafutiana na maelezo mengi ya Qur`ani Tukufu kwa sababu katika baadhi ya Sura kisa huja kwa njia na baadhi ya Sura zengine huja kwa njia nyengine, na katika njia ya tatu huja kwa njia yake, na hivi ndivyo Hadithi zilizoeleza si kutokana na aina ya kwanza isipokuwa ikiwa haijaelezea baadhi ya fafanuzi kwa baadhi ya zengine na kuelezea katika baadhi ya zingine na hilo pia hutokana na hali pamoja na wakati “kwani Mola hakuwa Mwenye kusahau” kisha akasema: “Pindi linapothibiti hili basi haiwezekani kwa mwenye kuzingatia sura hii ya mwisho kwa maana ya dalili zinazofuata kutafsiriwa maneno ya Kiarabu kwa maneno ya kiajemi kuongezea kutafsiriwa Qur`ani Tukufu na kuhamishiwa kwenye lugha isiyo ya Kiarabu isipokuwa kwa kuchukulia kuwa sawa lugha mbili katika matumizi kama ilivyoelezwa mfano wake, pindi linapothibiti hilo katika lugha inayotafsiri kutoka lugha ya Kiarabu huwezekana lugha moja wapo kutafsiri lugha nyengine, Ibn Qatiba amepinga uwezekano wa kutafsiriwa Qur`ani Tukufu kwa maana kutafsiriwa kwa sura hii ya pili, ama kwa sura ya kwanza inawezekana, na kwa upande wake anaona ni sahihi kutafsiri Qur`ani Tukufu na kuelezea maana zake kwa ujumla na kwa yule asiyefahamu basi anaweza fahamu maana zake kwa tafsiri hiyo na hilo ni jambo lenye kufaa kwa makubaliano ya Waislamu na makubaliano haya kuwa ni hoja katika kufaa tafsiri kwenye maana ya asili”.

Wakasema: Maneno haya yenye dalii na utafiti uliotoka kwa Mwanachuoni Mtukufu na muhakiki, na mwenye mitazamo ya kina, akiwa anatamka juu ya kufaa kutafsiri Qur`ani Tukufu pamoja na kuwepo kwa dalili.

Majibu ya haya ni kama ifuatavyo: “Maneno ya Al-Shaatwibi yapo wazi kuwa kinachowezekana ni kunukuu maana asili ya Qur`ani Tukufu, na katika kuita kwake neno tafsiri ya Qur`ani Tukufu inayopelekea hizo maana asili peke yake anakusudia kuita kilugha tu, na hili hatutafautiani bali tunaliunga mkono na kulihamasisha pamoja na vigezo ambavyo tutavielezea kwenye sehemu yake.

Ama tafsiri ya neno kwa neno ambayo ndio iliyoibua tafauti, kwa upande wa Al-Shaatwibi haikubali kabisa wala kuzungumzia si katika Qur`ani Tukufu wala isiyo Qur`ani Tukufu katika maneno ya kifasihi, na katika hili tuna dalili tano:

Dalili ya Kwanza: Amesema katika lugha ya wazi inayokubalika: “Pindi inapothibiti hii basi mwenye kuizingatia sura hii ya mwisho hawezi kutafsiri maneno ya Kiarabu kwa maneno ya Kiajemi (yasiyo ya Kiarabu) kuongezea kutafsiri Qur`ani Tukufu na kuhamishia kwenye lugha isiyo ya Kiarabu”

Dalili ya Pili: Katika tamko lilotajwa amenukuu kutoka kwa Ibn Qutayba kuwa amepinga uwezekano wa tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa sura hii ya pili, kisha akathibitisha juu ya kupinga huku kwa mwelekeo huu.

Dalili ya Tatu: Alisitasita wakati wa utafiti wake katika tafsiri, kusita huku kunaonesha kuwa hajakataa moja kwa moja rai inayopingana na madhehebu yake bali ni utafiti tu, ama hukumu inapokelewa katika moja ya kauli zao “Utafiti unawezekana na hukumu yenye kukubalika”na dalili ya kusitasita kwake ni pamoja na iliyokuja katika juzuu ya pili ya kitabu chake cha Al-Muwafikaati pindi aliposema: “Pindi inapothibiti kuwa maneno kwa upande wa dalili zake juu ya maana kuna pande mbili ni lazima kuangalia upande ambao hukumu yake ina manufaa: Je, anahusisha upande wa maana asili au inajumuisha pande zote mbili.

Ama kunufaika kwake kwa upande wa kwanza hakuna tafauti yeyote, ama kunufaika kwake na upande wa pili ndio sehemu ya kusitasita, na kila upande katika pande mbili kuna mtazamo” kisha akasema: “Kunaweza kubainika mgongano wa dalili katika masuala, na kuonekana upande wenye nguvu kati ya pande mbili ni upande wa wenye kuzuia manufaa ya hukumu, lakini unabakia mtazamo mwengine: Huenda kukawa na dalili juu ya maana zaidi kwenye maana asili, nayo ni adabu za Kisharia na maadili mema vinakuwa na mazingatio katika Sharia, upande wa pili unakosa dalili kwa ujumla, katika hali hiyo hutengeneza kauli ya kuzuia moja kwa moja ([69]), kusitasita huku kukowazi ([70]).

Dalili ya Nne: Kauli yake: “Na kwa upande wake amepitisha tafsiri ya Qur`ani Tukufu na ufafanuzi wa maana zake kuu, na yule asiyefahamu anakuwa na nguvu ya kuelewa maana zake na hilo ni jambo linalofaa kwa makubaliano ya Waislamu” ushahidi wake umeonesha tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwamba anakubali tafsiri ya maana ambazo ni tafsiri ya uchambuzi na wala si tafsiri ya neno kwa neno.

Mlango wa Pili: Dalili za vitendo na kiulinganizi ambazo zinaonekana ni lazima kwenye tafsiri ya neno kwa neno na majibu yake:

Dalili ya kwanza na jibu lake:

Wanasema kuwa ufikishaji wa uwongofu wa Qur`ani Tukufu kwa umma wa kigeni ni jambo la lazima kutokana na kufahamika kuwa ulinganiaji kwenye Uislamu ni kazi ya wote haihusishi kizazi fulani wala kabila, na huu ufikishaji wa lazima unategemea tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa lugha yao kwa sababu hawana uwezo wa lugha ya Kiarabu wakati ambapo Qurani imekuja kwa lugha ya Kiarabu, na jambo ambalo wajibu hautimii isipokuwa kwa jambo hilo basi nalo linakuwa ni wajibu.

Majibu ya hayo ni kama ifuatavyo:

Jambo la Kwanza: Ufikishaji huu kwao hautegemei tafsiri ya Qur`ani Tukufu ya neno kwa neno iliyozuiliwa bali inawezekana kutafsiriwa kwa maana ya kilugha nayo ni tafsiri yake na kufafanua maana zake pasi ya kutumia lugha yake ya Kiarabu, na inawezekana kuwafikishia uwongofu wa Qur`ani Tukufu na mafundisho yake pamoja na mambo mema ya Uislamu na sifa zake za kipekee na kuondoa shaka ambazo zinawatokea katika hilo, ima kwa mazungumzo ya mdomo au utunzi wa muundo wa tafiti zinazosambazwa au majarida au vitabu vinvyochapishwa mlinganiaji huteua katika hivyo kilicho sahihi zaidi na hali za walinganiwa na kilicho chepesi zaidi kwake na mafanikio zaidi katika ulinganiaji wake kwao.

Jambo la Pili: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu hajatukalifisha yasiyowezekana, kwani Mwenyezi Mungu haiamrishi nafsi isipokuwa kwa jambo linaloliweza, na ikibainika kutowezekana kutafsiri Qur`ani Tukufu kwa maana hiyo iliyozoeleka ni wazi Mwenyezi Mungu hawezi kutuamrisha kwenye hilo.

Jambo la Tatu: Kauli ya tafsiri hii ni wajibu hulazimisha kitu kisichowezekana nacho ni mgongano katika hukumu za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hilo ni kwamba Mwenyezi Mungu ameliharamisha kama ilivyoelezewa hapo mwanzo,  basi iweje ije kauli inayosimama kuwa amewajibisha pamoja na kuwa Mtwala ni mmoja naye ni Mwenyezi Mungu na sehemu ya hukumu ni moja nayo ni tafsiri na wenye kuhukumiwa ni wamoja nao ni walioamrishwa ndani ya zama zote na sehemu zote.

Jambo la Nne: Hakika Maswahaba Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe kwao wakiwa ndio taa na mwangaza wa uwongofu na watu wa tabaka bora kabisa katika waja wema wa umma waliotangulia na watu wenye shime kubwa ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu na radhi za Mtume S.A.W na wenye kufahamu zaidi siri za Uislamu na kiini cha Sharia zake, hata siku moja hawajawahi kufikiri juu ya hii tafsiri lakini si hivyo tu hata kujaribu kuileta bali walikuwa kama Mtume Mtukufu S.A.W alivyokuwa wakilingania kwa kutumia njia walizolingania nazo kwa uchangamfu mzuri na wa kushangaza katika kueneza Uislamu kuleta ukombozi, lau tafsiri hii ya neno kwa neno ingekuwa ni sehemu ya wajibu katika Uislamu basi katika waja wangefanya haraka sana kuiendea ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Maswahaba zake, na lau wangefanya hivyo basi ingenukuliwa na wengi kwa sababu mfano wake ni sawa na mengi yaliyonukuliwa na wengi ([71]).

Dalili ya Pili na jibu lake:

Wanasema kuwa uandishi wa Mtume S.A.W wa barua zake kwenda kwa Wafalme na wakubwa wasiokuwa Waarabu kunalazimisha Mtume S.A.W kukubali juu ya tafsiri kwa sababu hizo barua na hayo maandishi ndani yake yamekusanya Qur`ani Tukufu na wao ni Waajemi kwa maana si Waarabu na mapokezi sahihi yametaja kwa uwazi kuwa Mfalme Harqal akiwa ni miongoni mwa hao waliolinganiwa na wafasiri wakamtafsiria maandishi ya Mtume S.A.W ndani yake kukiwemo Aya za Qur`ani Tukufu.

Jibu la hoja hii:

Ni kuwa maandishi haya ya Mtume S.A.W hayalazimishi Mtume S.A.W kukiri juu ya tafsiri iliyozoeleka isiyokubalika bali hiyo ikiwa italazimika basi italazimika kukubali na kupitisha aina ya tafsiri inayofaa nayo ni tafsiri ya maana ya hizo barua si kwa lugha ya Kiarabu kwa sababu tafsiri kwa maana ni inatosha kufahamika madhumuni na maudhui ya barua zilizopelekwa pamoja na kuwa barua hizi tukufu hazikukusanya Qur`ani Tukufu yote wala Aya kamili bali yote yaliyomo ni uigaji mchache sana na wala hakuna shaka kuwa uigaji Qur`ani Tukufu hauchukui hukumu ya Qur`ani Tukufu yenyewe, na kuangalia hayo maandishi na hizo barua – nayo ni maelezo maarufu – yanatutosheleza sisi kuepuka kurefusha upokezi wake kwa maandishi yake ili kufanya dalili juu ya tunayoyasema.

Dalili ya Tatu na jibu lake:

Wanasema tafsiri ya Qur`ani Tukufu i iliyozoeleka inapokuwa ngumu kwa upande wa maana zake basi yenyewe inawezekana kwa upande wa maana zake za kiasili, na kutokana na hili basi tutafsiri Qur`ani Tukufu, kwa maana sisi tunukulu maana zake za asili pake yake hasa hasa kwa kuwa yenyewe inakusanya uwongofu unaokusudiwa na Qur`ani Tukufu i na wala si maana zisizo asili.

Jibu la hoja hii:

Tafsiri kuitwa kwa maana hii inayokusudiwa lau ingekuwa inahusishwa kwa muitaji wake bila ya kukutana na desturi, basi hotuba zingedharaulika na mambo yangekuwa mepesi na kuwezakana kufikiwa ukiukaji hata kwa mbali, lakini desturi ambayo tunazungumzia haifahamiki neno tafsiri isipokuwa ni sura inayotokana na sura asili, ikitosheleza maana zake zote na makusudio yake hakuna tafauti kati yake isipokuwa gamba la kimatamshi, hivyo sisi tumenukulu maana asili peke yake ya Qur`ani Tukufu kisha tukawaambia hawa watu desturi hii ndio tafsiri ya Qur`ani Tukufu, tunakuwa tumewapotosha hawa watu kwa upande mmoja, kisha tunakuwa tumeipunguzia Qur`ani Tukufu haki yake ya utukufu na ukubwa kwa upande mwengine, hivyo tukadhani kuwa Qurani ina mfano wake unaopambana nao na mfanano wake unaelezea wakati ambapo yale tuliyokuja nayo hayakuwa isipokuwa ni sura ndogo ya sehemu yake, na kati ya sura hii na utukufu wa asili kuna hatua tafauti.

Dalili ya Nne na jibu lake:

Wanasema wale waliotafsiri Qur`ani Tukufu kwenye lugha za kigeni wamebadili maana zake na kuchafua uzuri wake na wamekosea makosa makubwa, hivyo sisi ikiwa tutatafsiri Qur`ani Tukufu kwa maana zake itawezekana kusahihisha hayo makosa na kurejesha kwenye Qurani Tukufu mazingatio yake katika mtazamo wa hao ambao wanasoma hizo tafsiri zenye kupotosha, na tutaondoa vikwazo ambavyo vimewekwa kwenye njia yao ya kuelekea katika uwongofu wa Uislamu, kwa kufanya hivyo tunakuwa tumetekeleza ujumbe wetu katika kueneza na kulingania dini hii iliyonyooka.

Jibu la hoja hii:

Wale ambao wanadhania kuwa wao wametafsiri Qur`ani Tukufu kwa tafsiri za lugha za kigeni kuwa wamechafua uzuri wake na kufunika nafasi yake kwa kukiri kwenu, hivyo ikiwa nyinyi mmetafsiri mliyotafsiri na mkajaribu majaribio yenu basi hakuna shaka hivi karibuni mtatumbukia sehemu waliyotumbukia, na mtagusa kwa nafasi yenu ukubwa wa Qur`ani Tukufu hii na Utukufu wake vyovyote mtakavyofikia undani na viwango vya elimu na uelewa mkubwa kwa sababu Qur`ani Tukufu ni yenye nguvu zaidi na kuzuia zaidi kufikiwa na mjenga taswira yeyote akiwa binadamu au jini, ama ikiwa mtajaribu kutafsiri Qur`ani Tukufu kwa maana ya tafsiri ya maana zake kwa kuitafsiri kwa lugha ya kigeni basi huo ni msimamo mwengine tunakuungeni mkono na tunakubaliana nanyi kwenye hilo na kuwataka wenye uwezo katika hilo ([72]).

Sehemu ya Tatu: Hukumu ya tafsiri ya maana:

Waandishi wa vitabu wametafautiana katika masuala ya tafsiri vile vile katika aina hizi za tafsiri, wengi wao wameona inafaa, na wachache wameona kutofaa.

Miongoni mwa waliona kutofaa ni pamoja na Sheikh Abu Sulaiman Anarah na Sheikh Muhammad Mustafa Al-Shatwir, Ustadhi Muhammad Al-Hahayawi ([73]) na wengineo.

Na sisi tupo pamoja na Jamhuri ya Wanachuoni katika kuhalalisha tafsiri hii na hilo ni kwa vigezo mbalimbali tutavielezea hapo baadaye.

Mlango wa Kwanza: Dalili za kufaa tafsiri hii na majibu ya wapingaji pamoja na majibu juu ya majibu hayo:

Dalili zetu kwa yale tuliyosema pamoja na wenye kupitisha ([74]) ni dalili ya jumla ya kauli za viongozi wa madhehebu mbalimbali na nitataja kauli kisha kumalizia na kile walichojibu wale wapingaji wa tafsiri hii kisha na ambatisha jibu juu ya hilo jibu.

Kauli za watu wa madhehebu juu ya hukumu ya tafsiri ya maana ya Qur`ani Tukufu:

Maneno mengi ya wazungumzaji yamejikita kuhusu hukumu ya kusoma tafsiri ya Qur`ani Tukufu ndani ya swala je hiyo inafaa kwa mtu asiyeweza lugha ya Kiarabu au haifai, hivyo hawakuongelea hilo isipokuwa wachache miongoni mwao juu ya hukumu ya tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa ujumla, bali maneno yao huleta hisia kana kwamba jambo hili halina haja ya kuelezea hukumu yake kutokana na utukufu wake, ikiwa hakuna tafauti katika kufaa maana na kauli ya wengi imejifunga kwenye hilo basi tafsiri yake inafaa – kwa maana ya tafsiri ya maana zake – kwa kupitishwa pia na Wanachuoni wengi.

Pamoja na haya wameelezea zaidi ya mmoja juu ya kufaa kwake – miongoni mwa yanayojumuisha kufaa kwake – na hizi ni baadhi ya kauli zao:

Watu wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa:

Al-Kamal Ibn Al-Hamaam anasema: “Ikiwa imezoeleka kuisoma Qur`ani Tukufu kwa Kiajemi au akitaka kuandika Msahafu kwa hiyo lugha, huzuiliwa, ikiwa atafanya kwenye Aya moja au mbili hakuna katazo, ikiwa ataandika Qur`ani Tukufu na maana kila herufi na tafsiri yake inafaa” ([75]).

Na katika kitabu cha Al-Nafhatul-Qudsiyah cha Sharnablaly anasema: “Ufupi wa maelezo yaliyotangulia ni haramu kuandika Qur`ani Tukufu kwa lugha ya Kifursi isipokuwa kuandikwa kwa Kiarabu na kuandikwa maana ya kila herufi na tafsiri yake” ([76]).

Watu wa madhehebu ya Imamu Maliki:

Hapo nyuma tumeelezea maneno ya Al-Shatwiby na kubainisha kuwa anakusudia tafsiri ya kimaana, na maelezo ya Ibn Batwal Al-Maliky ambayo yamenukuliwa na Ibn Hajar yatakuja.

Wanaopinga wakajibu kuhusu maneno ya Al-Shatwiby kama ifuatavyo:

Amepitisha tafsiri ya asili ya maana na haiwi hii isipokuwa kwa tafsiri jumla na wala si tafsiri maalum kwa wale ambao hawanufaiki na maana hizo bali kufaidika kwao kunatokana na maana si za asili na ambazo haziwezekani.

Amefanya dalili ya kufaa hiyo tafsiri ni makubaliano ya Wanachuoni juu ya kufaa tafsiri ya maana, na hili lenye kupingwa kwa sababu waliokubaliana juu ya kufaa tafsiri ya kwa lugha ya Kiarabu hawajakubaliana juu ya kufaa tafsiri ya Qur`ani Tukufu.

Haya ndio maelezo ya maneno yao kwa kuongezea na yaliyotangulia kuelezewa wakati wa kumjibu aliyetolea dalili maneno ya Al-Shatwaby juu ya tafsiri ya neno kwa neno pamoja na jumla ya majibu mengine hayatoshelezi ndani yake juu ya uwazi wa ubatili wake ([77]).

Tunajibu juu ya jibu la Kwanza:

Kauli kuwa tafsiri asili ya maana haileti faida isipokuwa kwa watu wa kawaida , ndani yake kuna matokeo hayajaelezwa kwenye tangulizi sahihi, na huko nikupingana,  ambapo maana za kiasili – nazo ni makusudio makuu ya maneno yote – hakuna shaka katika kunufaisha kwake kila msomaji wa hayo maneno, basi ni namna gani ikiwa maneno ndio maneno yaliyobora zaidi, hivyo faida ingekuwa inatokana na maana zake asili hazilinganishwi wala kupingwa, kisha kupinga huku ndani yake ni kukubali faida za hiyo tafsiri kwa hali yeyote ile, kisha ikiwa tutawakubalia kwa kauli hii basi hiyo tafsiri ingekuwa yenye kutakiwa pia kwa sababu hakuna shaka kuwa watu wa kawaida katika kila umma wengi na asilimia kubwa, hivyo kutaka kwao manufaa ni jambo linalotakiwa na zuri halina shaka, na mwisho Al-Shatwibi mwenyewe anaona umuhimu wa hilo ambapo maneno yake katika masuala haya ameyakamilisha kwa kauli yake: “Kwa upande wake – kwa maana ya upande wa maana za asili – ni inafaa tafsiri ya Qur`ani Tukufu na kuelezea maana zake za jumla, na kwa asiyefahamu Kiarabu atafahamu kwa kufahamu maana zake, na hilo ni jambo linalofaa kwa makubaliano ya Waislamu hivyo makubaliano haya yamekuwa ni hoja katika kufaa tafsiri kwa maana ya asili” hii inatosha kuvunja hayo madai yao.

Ama jibu la Pili:

Tunajibu kuwa amepinga katika mambo yaliyowazi ambapo makubaliano ya Wanachuoni juu ya kufaa tafsiri ya maana ni dalili yenye nguvu juu ya kufaa tafsiri hiyo ya maana, na hili linafahamika kwani tafsiri yako ya maneno yanayokusudiwa kwa kutumia lugha miongoni mwa lugha ni dalili ya uwezekano wa tafsiri inayokusudiwa kwa kutumia lugha yeyote nyingine, ikiwa litakanushwa hili basi kwetu isingesimama tafsiri ya lugha yeyote ile,

pindi ilipowezekana kufahamika makusudio ya maneno ya watu kwa lugha zao mbalimbali pamoja na uwingi wake na ufafanuzi wake hiyo ni katika alama kubwa za Mwenyezi Mungu na hekima zake, na makubaliano ya Wanachuoni wa kila umma juu ya uwezekano wa tafsiri inayokusudiwa ya maneno yeyote kwa lugha yeyote hata lugha zikitafautiana kwa upande wa ufasaha na viwango vya balagha, haya yote yanasisitiza maneno ya Al-Shatwibi ambapo hakuna tafauti kati ya mfafanuzi na mtafsiri isipokuwa huyo mmoja anaweka ubainifu na ufafanuzi maana ya neno la Kiarabu na mwengine neno la kigeni.

Viongozi wa Madhehebu ya Imamu Shaafiy:

Kaffalu anasema katika fatawa yake: “Kwangu mimi ni kuwa hakuna awezaye kuleta Qur`ani Tukufu kwa lugha ya Kiajemi. Akaambiwa: Hivyo hakuna yeyote anaweza kutafsiri Qur`ani Tukufu. Akasema sio hivyo, kwa sababu hapa – kwa maana katika tafsiri – inafaa kuleta baadhi ya makusudio ya Mwenyezi Mungu na kushindikana baadhi ya mengine, ama mtu akitaka kuisoma Qur`ani Tukufu kwa lugha ya Kiajemi haiwezekani kuleta makusudio yote ya Mwenyezi Mungu kwa sababu tafsiri ni kubadilisha neno kwa neno lengine linalochukuwa nafasi yake na hilo haliwezekani tafauti na tafsiri ya kimaana hivyo haikusudiwi tafsiri hii” ([78]).

Na Ibn Hajar amesema katika kitabu cha Al-Fat’hu: Ibn Battwal amesema: Kwa upande wa kuzungumzia tafsiri ni kuwa Ufunuo au Wahyi wote ukiwa wa kusomwa au si wakusomwa kwa hakika umeteremka kwa lugha ya Waarabu, wala hili halikusudiwi kuwa Mtume S.A.W ameletwa kwa watu wote Waarabu na wasio Waarab na wengineo kwa sababu lugha ambayo iliteremshiwa Wahyi ni lugha ya Kiarabu naye S.A.W hufikisha kwenye makundi ya Waarabu nao hutafsiri kwa wasiokuwa Waarabu kwa lugha zao” ([79]). Ibn Hajar ameikubali kauli hii na wala hajaipinga.

Kauli ya watu wa madhehebu ya Imamu Hambali na majibu ya wanaopinga pamoja kuwajibu majibu yao:

Ibn Muflihu amesema katika kitabu cha Al-Furuui: Sheikhe wetu amesema: “Tafsiri Inapendeza penye haja kwa mwenye kuhitaji kuifahamu Qur`ani Tukufu kwa kutumia tafsiri, na wengine wakasema maana hii, na kutolewa onyo kwenye Qur`ani Tukufu pasi na lugha hiyo kama tafsiri ya cheti” ([80]).

Na Al-Bahuty amesena ndani ya kitabu cha Kasshaf Al-Qannai: (Ni bora penye haja ya tafsiri yake) kwa maana ya Qur`ani Tukufu. (Pindi itakapohitajika kufahamika kwake kwa kutumia tafsiri) hiyo tafsiri itakuwa ni ibara ya maana ya Qur`ani Tukufu, na maana yake kwa hiyo lugha haitakuwa Qur`ani Tukufu wala muujiza kama maelezo yalivyotangulia. (Na) katika hili: Kwa hakika (Kumekuwa na onyo kwa Qur`ani Tukufu) kwa maana: Yenye kuelezewa maana yake kwa hiyo lugha. (Pasi ya hiyo lugha, kama vile tafsiri ya cheti)[81].

Ibn Taimiya anasema: Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:

{Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa watu wake ili apate kuwabainishia} Ibrahimu: 4.

Na wala hajasema, na hatukumtuma Mtume isipokuwa kwa watu wake, lakini hakutumwa isipokuwa kwa lugha ya watu wake ambao kwanza anawaambia wao ili wawafafanulie watu wake, pindi wanapobainisha kwa watu wake yale anayoyataka ndipo kwa hilo hufikia makusudio yao na makusudio ya wengine, kwani watu wake ambao wamefikishiwa kwanza wanaweza kufikisha neno kutoka kwake na wanaweza kunukuu maana kutoka kwake kwa ajili ya yule asiyefahamu lugha ya Kiarabu, na wengine wanaweza kujifunza kutoka kwao lugha yake na kufahamu kusudio lake, hoja husimama kwa waja na kupata uwongofu kutoka kwa anayenukuu kwa Mtume S.A.W maana na wakati mwengine akanukuu neno au tamko, kwa hali hii inafaa kunukuu Hadithi zake kimaana, na Qur`ani Tukufu inafaa kutafsiri maana zake kwa asiyefahamu lugha ya Kiarabu hii ni kwa makubaliano ya Wanachuoni, na baadhi yao wakapitisha mtu kusoma Qur`ani Tukufu si kwa Kiarabu kwa yule mwenye kushindwa kuisoma kwa Kiarabu, na wengine wamepitisha moja kwa moja, na Jamhuri ya Wanachuoni wamepinga kusoma Qur`ani Tukufu kinyume na lugha ya Kiarabu pamoja na kuwa wamepitisha kuitafsiri ili wafahamu wasioweza Kiarabu, pia wamepitisha tafsiri yake na ubainifu wa maana zake pamoja na kuwa ubainifu wa maana si Qur`ani Tukufu ya kusomwa vile vile tafsiri yake” ([82]).

Na anasema katika sehemu nyengine: Ama kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Hakika Sisi tumeiteremsha Qur`ani kwa Kiarabu ili mpate kuzingatia} Yusuf: 2.

Na kauli yake: {Na lau tungeli ifanya Qur`ani kwa lugha ya kigeni wangelisema: Kwanini Aya zake haziku pambanuliwa? Iweje lugha ya kigeni na Mtume Muarabu?} Fussilat: 44.

Na kauli yake:  {Hakika Sisi tumeifanya Qur`ani kwa Kiarabu ili mfahamu} Al-Zughruf: 3.

Hii inakusanya neema za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, kwa sababu lugha ya Kiarabu ni lugha kamilifu zaidi na mzuri katika kuelezea maana, hivyo kuteremka Qur`ani Tukufu kwa lugha hiyo ni neema kubwa sana kwa waja kuliko kuteremka kwa lugha nyengine, nayo imezungumza kwa lugha ya Kiarabu kwanza ili wapate kuifahamu kisha mwenye kujua lugha yao atawafahamisha kama walivyoifahamu, na asiyejua lugha yao atamtafsiria kwa lugha yao iliyozoeleka, ikawa kwanza Waarabu wajengee hoja na kuneemeka nayo kwa kufahamu kwao maana zake kabla ya kufahamika na wengine ([83])… na Taurati hii katika zama zetu na Injili pamoja na Zaburi hutafsiriwa kwa lugha ya Kiarabu na bila shaka yeyote kufahamika makusudio, basi ni vipi Qur`ani Tukufu ambayo watu wake wanafahamu maana yake na wanaelezea maana zake na kuitafsiri kwa uzuri zaidi ya watu wa Taurati na Injili ([84]).

Wenye kupinga hiyo tafsiri walijibu kuhusu maandiko haya kuwa yamevuliwa kwenye hukumu ya jumla – nayo kuharamishwa – kutokana na umuhimu na kuhitajika, na mfano wake katika hilo ni kama mfano wa kuvua uhalali wa kula mzoga kwa dharura, na dharura hii hukadiriwa kwa kiwango chake bila kuvuka mpaka na wala haifai kuijengea hukumu ya jumla, hivyo hatupitishi kuwa watu wa madhehebu ya Imamu Hambali wamepitisha tafsiri ya Qur`ani Tukufu ([85]).

Jibu la jawabu hili: Kuhukumu maandiko kwa mfano wa njia hii ni hukumu ya wazi, vile vile ni kuwazushia viongozi wa madhehebu na watu wake lau ingelikuwa sahihi basi wangelikuwa wao ndio wasemaji wa kwanza na watamkaji wa hilo, na kila chunga maandiko na akafahamu mwenendo wa Wanachuoni katika matamko yake atafahamu kwa uwazi kuwa Wanachuoni wa madhehebu ya Imamu Hambaly katika maandiko yaliyopita hawazungumzii kuhusu hali za dharura.

Tatizo lililopo kwenye ufahamu wa wapingaji ni kuwa wamekuja na kauli za madhehebu matatu – tofauti na madhehebu ya Abu Hanifa – juu ya uharamu wa kusoma tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa Kiarabu au kwa lugha nyengine katika swala, kisha makubaliano hayo yanalazimisha – kwao – kuharamisha tafsiri ya Qur`ani Tukufu pia nje ya swala, ukweli ni kuwa ulazima huu ni kwa jambo lisilo la lazima, na mtazamo umetengana kikamilifu kati ya hukumu ndani ya swala na nje ya swala, kwa sababu swala ni kuabudu kwa njia iliyoelezewa na Sharia haifai kinyume chake,

tafauti na amri nje ya swala, pia utoaji wao dalili kwa makubaliano haya ya pili kuna majibu ya madai yao, kwa sababu anashuhudia kuwa Wanachuoni wa madhehebu manne wanakubali na kupitisha kufaa tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa lugha isiyokuwa Kiarabu, na kama si hivyo basi wasingesema kutokufaa kuswalia, bali tamko lao litakuwa kutofaa kwake jambo ambalo lingepelekea kutofaa kuswalia ni bora zaidi, kwa sababu hukumu ya swala ni maalum kuliko hukumu zengine pamoja na makubaliano ya kufaa maana ya Qur`ani Tukufu kwa Kiarabu isipokuwa makubaliano pia juu ya uharamu wa kusoma hiyo maana ya Qurani ndani ya swala kwa msingi huu, na kwa vile lau ingekuwa kwao haifai au inafaa katika hali maalum wangelazimika kuelezea hilo na kulimtaka katika maelezo yao.

Kauli ya Zamakhshary na majibu ya wapingaji pamoja na majibu juu ya majibu haya:

Zamakhshary anasema wakati wa kuelezea kwake kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: 

{Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa watu wake ili apate kuwabainishia} Ibrahimu: 4. Ikiwa utasema Mtume wa Mwenyezi Mungu hakupelekwa kwa Waarabu peke yao bali amepelekwa kwa watu wote: 

{Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote} Al-Araaf:  158.

Bali na kwa majini pia na wao wakiwa na lugha tafauti, ikiwa kwa Waarabu si hoja basi kwa wengine ni hoja, hata kama kwa wengine si hoja, lau ingeteremka kwa lugha ya kigeni kwa Waarabu pia isingekuwa hoja. Nikasema: Haiepukani ima iteremke kwa lugha zote au lugha moja, hivyo hakuna hoja ya kuteremka kwake kwa lugha zote, kwa sababu tafsiri huchukuwa nafasi yake na inatosha kubakia kuteremka kwa lugha moja, hivyo ikawa lugha bora zaidi lugha ya watu wa Mtume S.A.W kwa sababu wao ndio watu wa karibu zaidi kwake, ikiwa watamfahamu na wakambaini na kusambaza ujumbe, watu wa tafsiri ([86]) watafanya kazi ya kufafanua na kufahamisha, kama hali inavyoonekana na kushuhudiwa ya wafasiri ndani ya kila umma katika umma wa kiajemi, pamoja na hayo miongoni mwa makubaliano na watu wa maeneo ya mbali na nchi zenye kuvutana pamoja na mataifa mbalimbali na kizazi tafauti juu ya kitabu kimoja, na jitihada zao katika kujifunza neno lake na kujifunza maana zake, na yanayogawanyika katika hilo miongoni mwa faida nyingi, na uwingi wa tabu kwa kujiweka  ukaribu na utiifu kwenda kwenye thawabu nyingi, na kwa vile yenyewe ipo mbali sana na upotoshaji na kubadilisha, na imesalimika na mvutano pamoja na tafauti, kwa sababu lau ingeteremka kwa lugha zote za wanadamu na majini – pamoja na tafauti zake na uwingi wake, na ikawa inajitegemea kwa sifa ya muujiza kwa kila lugha, na Mtume S.A.W Muarabu akazungumza na kila umma kwa lugha yake kama alivyozungumza na umma wake ambao Yeye anatokana nao akiwasomea muujiza – basi hilo lingekuwa ni jambo lilokaribu sana na kukimbiliwa ([87]).

Wapingaji wakajibu kwa tafsiri hii kwa maneno haya, kuwa Zamakhshary kwa hakika tafsiri anayokusudia hapa ni tafsiri ya kimaana ([88]), na hili halina shaka ni hukumu ya kwa wazi, hivi anachukuwa wapi maana hii ya kilugha ya tafsiri ambayo ndio kusudio la maneno yake pamoja na kuwa tafsiri inapoitwa kwa muundo huu hutumika kwenye kufikisha maneno kwa lugha nyengine kama ilivyoelezwa, haya pamoja na kuwa maneno ya mwenye kitabu cha Al-Kasshafu anapinga kuelezea maneno yake kwa maana hii, ambapo anasema katika jumla ya maneno yake “Wafasiri wakafanya kazi ya kufafanua”  kama hali inayoonekana na tunashuhudia kazi za wafasiri katika kila umma miongoni mwa umma za Kiajemi” maelezo yalitangulia kuwa neno “Taraajimu” ni uwingi wa neno “Turjuman” kwa maana ya wanaofanya kazi za kutafsiri na wala si uwingi wa tafsiri, na kwa maelezo hayo kusudio la Zamakhshary lipo wazi sana kuwa wafasiri watanukuu Qur`ani Tukufu na kuitafsiri kwa umma zengine, naye anataja haya kwa kukubali kikamilifu haya yanayoelezwa kwenye upingaji huu.

 

Kutokana na hayo inafahamika kuwa wengi wamepinga tafsiri ya neno kwa neno kwa aina zake lakini hawajapinga kwenye tafsiri hii ya kimaana, nalo ni jambo linalounga mkono hoja ya waliopitisha, hivyo Sheikh Bakhiit Al-Matwii amesema: “Fahamu kuwa tafsiri ya kimaana kwa kuandika Qur`ani Tukufu kwa maneno yake yaliyoteremshwa ya Kiarabu kisha akaandika maana zake pembeni mwake basi hili linafaa kwa lugha yeyote iwe ya Kiarabu au isiyo ya Kiarabu, na Al-Kamal Ibn Al-Himam na Imam Al-Haramaini amepitisha kwenye kitabu cha Al-Burhaan” ([89]) na akasema: “Katika hali yeyote kufikisha maana kwa njia ya tafsiri ni jambo linalofaa moja kwa moja,  na Abu Al-Suud akashiria kwenye tafsiri yake ya kauli ya Mola Mtukufu: 
 {Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa watu wake} Ibrahimu: 4. Na kupitishwa na Al-Aluusy” ([90]).

Sheikh Mustafa Swabriy amesema: “Hakuna maneno katika kufaa tafsiri ya kimaana, bali maneno yapo katika tafsiri inayochukuwa nafasi ya Qur`ani Tukufu katika swala na ibada zengine” ([91]), na anasema: “Ama tafsiri ya kimaana… yenyewe kwetu sisi inakutana na tafsiri ya kiufafanuzi” ([92]).

Sheikh Al-Shaatwir mwenyewe amekubali yale yanayopinga maneno yake ambapo anasema: “Hakuna yeyote katika Maimamu wanne… aliyesema kuwa kutafsiri Qur`ani Tukufu yote ni jambo la lazima… bali baadhi ya Wanachuoni wamesema ni jambo linalofaa lakini kwa masharti yanayokaribia kuwa ni magumu kutekelezeka” ([93]), ninadhani kuwa kukiri huku hakuhitaji kurefusha maelezo katika kuharamisha na kupinga ni yale aliyoeza mwenyewe katik kauli za  baadhi ya Maimamu za kufaa kwake wala si kwa wajibu wake, je, kuna yeyote mwenye kupinga kutokuwa lazima?

Sheikh Juzairy anasema: “Tafsiri ya maana ya Qur`ani Tukufu si tafsiri ya Qur`ani Tukufu, kwa sababu tafsiri ya kimaana ni ibara ya tafsiri ya ufafanuzi hutaja maana ya neno kwa lugha ya Kiarabu kisha maana hiyo hutafsiriwa, wala hakuna yeyote anayeweza kusema kuwa hiyo tafsiri haifai na haya ndiyo ambayo yamepitishwa na Jopo la Wanachuoni wakubwa na Wanachuoni wa Sharia” ([94]).

Na anasema katika sehemu nyingine:  “Ama tafsiri ya maana ya Qur`ani Tukufu ni maneno ya watu kwani yenyewe si yasiyowezekana bali wala kuwa na uzito, kwa sababu tafsiri ya watu si muujiza” ([95]) hivyo kundi la Wanachuoni wakubwa wamepinga tafsiri ya Qur`ani Tukufu ya neno kwa neno ([96]).

Sheikh Shaatwir mwenyewe anasema: “Ama tafsiri ya kimaana ni tafsiri iliyofahamika na wafasiri kwa yale waliyoyafahamu miongoni mwa sentensi changamano za Qur`ani Tukufu kwa kiwango cha uwezo wao, wala hakuna sharti ya kuwa maneno yawe visawe, na tafsiri hii inawezekana kwa upande wa kiwango ambacho watafsiri wameweza kuifahamu kwa sura ya uhakiki wa Aya Tukufu, ikiwa tafsiri haizidi maneno ya asili wala kupungua katika maana na uhakiki wa maaana ya Nassi” ([97]).

Ukweli ni kuwa haya ndiyo tunayoyataka na kuyapenda katika kupitisha kwetu tafsiri kwa vigezo vyake, na haya ndio yaliyopitishwa na Jopo la Wanachuoni wakubwa wa Al-Azhar wakati wa kutengeneza mradi wa tafsiri, nayo yamepitishwa na Wanachuoni wa zamani kama tulivyoelezea kauli zao.

Mlango wa Pili: Vigezo tunavyoviona katika tafsiri zinazotakiwa:

Hivyo hapa ni lazima kufahamu mambo muhimu kama vigezo vya tafsiri hizi:

Jambo la Kwanza: Wanachuoni wetu walikataza kuandikwa Qur`ani Tukufu kwa herufi zisizo za Kiarabu na kutokana na hili ni lazima wakati wa kutafsiri Qur`ani Tukufu i kwa maana hii kwa lugha yeyote ile kuandika Aya za Qur`ani Tukufu kwa herufi za Kiarabu ili kuepuka upotoshaji katika maneno yake na kupelekea kubadilisha na kuharibu maana zake.

Niliuliza kamati ya fat’wa ya Al-Azhar kuhusu kuandika Qur`ani Tukufu kwa herufi za Kilatini wakajibu: “Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumtakia rehma na amani Mtume wake S.A.W: Hakuna shaka kuwa herufi za Kilatini zinazofahamika zimekosa herufi nyingi uwiano na herufi za Kiarabu, hivyo hazifanyi kazi kama zinavyofanya kazi herufi za Kiarabu, lau Qur`ani Tukufu itaandikwa kwa hizo herufi za Kilatani kwa mfumo wa herufi za Kiarabu kama inavyofahamika basi kutatokea ukiukaji na upotoshaji katika matamshi, na kupelekea kubadilika maana na kuleta uharibifu, maandiko ya Sharia yametoa hukumu ya kulindwa Qur`ani Tukufu na kila yanayoashiria kubadilishwa na kupotoshwa, Wanachuoni wa Uislamu wa zamani na wasasa wamepitisha kuwa kila matumizi ndani ya Qur`ani Tukufu yanayopelekea upotoshaji wa maneno yake au kubadilisha maana zake ni jambo halikubaliki la kuzuiliwa moja kwa moja na ni haramu, Maswahaba Radhi za Mola ziwe kwao na waliofuata baada yao mpaka hii leo wamelazimika kuandika Qur`ani Tukufu kwa herufi za Kiarabu” ([98]).

Jambo la Pili: Tafsiri ya Qur`ani Tukufu inayozunguka kati yetu inazungumzia neno moja moja linalotokana na neno asili na pembezoni mwake kuna ufafanuzi wake au sherehe yake kisha huelezea jumla au Aya na sherehe yake inayoungana nayo mara nyingi, maana yake ni kuwa maneno ya Qur`ani Tukufu katika sifa zake yanachimbuka kutokana na mfungamano na hukumu ambapo lau tafsiri tutaitenga na maneno asili basi tafsiri itakuwa yenye maneno ya upuuzi na ukosefu wa maana, na sisi hapa hatutaki katika tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa lugha ya kigeni kutaja maneno ya Qur`ani Tukufu na sentensi zake zikiandikwa kwa lugha ya kigeni au kutafsiriwa kwa lugha hii, kisha iwe na uombezi kwa tafsiri yake iliyotajwa,  tumepitisha kuwa kuandika Qur`ani Tukufu kinyume na lugha ya Kiarabu haifai, bali hapa tunataka aina ya tafsiri inafaa kutokana na maneno asili kama yalivyo katika Kiarabu chake kiuandishi na kimatamshi pindi inapofikishwa kwenye kundi la Waislamu, kisha mwisho wake hutaja maana ambayo ameifahamu mfasiri bila ya kuchanganyika na maneno asili wala tafsiri yake, bali maana hii yote inakuwa kutokana na maneno ya mfasiri na kuunda muundo unaonesha kuwa ni maana na wala si tafsiri, kama kusema maana ya Aya iliyopewa namba fulani kutoka Sura fulani hiyo ni Aya fulani, au kusemwa mwanzoni mwa kila tafsiri ya maana ya sentensi au Aya fulani kisha kubainisha katika njia zote hizo mbili kuwa maana hii imepitishwa moja kwa moja au yenyewe inachukuliwa na kudhaniwa kuwa mahitaji ya wanaoambiwa ni makubwa kuliko maana kwa misamiati ya Kiislamu siri na hukumu za Kisharia, na kutanabahisha makosa ambayo yametokea kwenye tafsiri zinazokusudiwa na mfano wa hayo jambo linalopelekea hofu kwa msomaji kuwa anayoyasoma si tafsiri ya asili iliyozungukwa na maana zote pamoja na makusuduio yake, bali ni ufafanuzi tu haujabeba maana ya Qur`ani Tukufu na makusudio yake isipokuwa uchache katika kingi ni kama tone la maji katika bahari, ama Qur`ani Tukufu yenyewe ni kubwa kuliko hii tafsiri , basi iweje, nayo ni maneno muujiza katika maneno yake na maana zake ni maneno ya Mwingi wa elimu na Mwingi wa habari.

Jambo la Tatu: Tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa maana hii ni sawa sawa na tafsiri ya maana yake kwa Kiarabu, kwa sababu hapa tafsiri kwa uhakika haijazungumzia isipokuwa ni rai na mtazamo wa huyu mwenye kutafsiri na ufahamu wake kuhusu kusudio la Mwenyezi Mungu kwa kiwango cha nguvu ya ufahamu wake, uwe una makosa au upo sahihi, na wala haizungumzii makusudo yote ya Mwenyezi Mungu ya maneno yake, kana kwamba mfasiri huyu kwanza ameweka tafsiri ya Kiarabu kisha akaitafsiri hiyo tafsiri ambayo ameiweka, ikiwa utapenda basi sema kuwa ametafsiri maana ya Qur`ani Tukufu bila ya kuiandika, hakuna shaka kuwa tafsiri hii ni tafsiri ya ufafanuzi, sawa sawa mwenye kutafsiri ameiandika au hajaiandika.

Jambo la Nne: Baadhi ya aina hii na inayofanana nayo wameita tafsiri ya maana ya Qur`ani Tukufu kwa maana yenye kuzoeleka, na sisi pamoja na kujua kuwa hakuna mvutano kwenye msamiati isipokuwa huenda msamiati huu ukawa hauna mvuto, hivyo tafsiri ya maana ni mtazamo wa kila alichotaka mwenye kutafsiri kuelezea maana zake na makusudio yake, na Qur`ani Tukufu haiwezekani kabisa katika maana zake za makusudio ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa na makosa, ama tafsiri inawezekana katika maana zake zinazokusudiwa na mtafsiri kuwa na makosa,  hivyo inapasa kunasibisha hizo tafsiri kwa mwenye kutafsiri na wala si kwenye Qur`ani Tukufu ili yasinasibishwe makosa ya tafsiri – kama yatakuwepo – na Qur`ani Tukufu, pia Qur`ani Tukufu imejaa maana na siri nyingi zilizowazi na zilizojificha kwa kiwango cha viumbe kushindwa kufahamu,  pamoja na uwezo wake wa kuzungumzia na kusawiri kwa lugha ya Kiarabu au ya kigeni, na katika hili jicho muangaliaji yeyote linaweza kuangalia na kuiletea taswira tafsiri kwa lugha yeyote ([99]).

Jambo la Tano:  Inapendelewa mfano wa tafsiri kama hii kuitwa “Tafsiri ya ufafanuzi wa Qur`ani Tukufu” au “Tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa lugha fulani” na inafaa vile vile kuita “Tafsiri ya maana ya Qur`ani Tukufu” kwa mazingatio haya – nina maanisha mazingatio kuwa makusudio ya maana ni tafsiri – na kupinga uitaji huu kuwa neno tafsiri halitegemezwi isipokuwa katika maneno ya upingaji yasio kuwa sahihi;  kwa sababu maana ni maneno pia, na tafsiri ni maana za maandiko, ikiwa tutapitisha kuita “Tafsiri ya ufafanuzi” tutakuwa tumepitisha kuita “Tafsiri ya kimaana” kwa vigezo ambavyo tunaviangalia na kuvielezea, na kauli kuwa uitaji huu unafahamika kuwa tafsiri yenyewe ya Qur`ani Tukufu ni kauli ipo mbali na uhalisia, kama vile haifai kuita “Tafsiri ya Qur`ani Tukufu” kwa uitaji huu moja kwa  moja wa kilugha, kutokana na kutanguliwa kuelezewa kwake kuwa neno “Tafsiri ya Qur`ani Tukufu” linashirikiana kati ya maana nyingi, na maana inayokuja haraka kwenye akili wakati wa kutajwa si yenye kufaa kama ilivyoelezewa.

Jambo la Sita: Ni lazima mwenye kutafsiri kuleta utangulizi akikanusha kwa uwazi kuwa ni tafsiri ya Qur`ani Tukufu yenyewe, na kubainisha kuwa tafsiri ya Qur`ani Tukufu yenyewe kwa maana inayofahamika ni ni jambo lisilowezekana, kwa sababu asili ya Kitabu hiki hukataa kuwa na mwenzake anayekielezea si kwa lugha yake wala nje ya lugha yake, vile vile hiyo ndio maana ya muujiza wake wa kibalagha, na mwenye kutaka kuangalia aina hii miongoni mwa aina za muujiza wake basi na aangalie kwenye Kitabu hiki lugha yake na muundo wake, na katika yasiyowezekana kuhama Kitabu hiki Kitukufu kwa kuacha mazingira yake ambayo Mwenyezi Mungu ameyaandalia nayo ni mazingira ya lugha ya Kiarabu.

Na hivi ni vigezo ambavyo vimewekwa na kamati ya Al-Azhary ambayo ilipitisha kazi ya tafsiri:

Tafsiri isiwe na kinachowezekana miongoni mwa misamiati na tafiti za kielimu isipokuwa yale yanayopeleka ufahamu wa Aya.

Kutopingana na mitazamo ya kielimu kwa mfano asitaje tafsiri ya kielimu ya neno radi au umeta wa radi kwenye Aya inayotaja radi na umeta wake, wala mitazamo ya wana anga kuhusu mbingu na nyota kwenye Aya ndani yake imetaja mbingu na nyota bali tafsiri ya Aya iendane na kinachomaanisha neno la Kiarabu na kuweka wazi sehemu ya mazingatio na uwongofu.

Ikiwa kuna haja ya kupanua zaidi katika kuhakiki baadhi ya masuala, kamati itayaweka katika maneno ya pembeni ya tafsiri.

Kamati isifuate isipokuwa yaliyomo kwenye Aya Tukufu wala isifuate Madhehebu fulani miongoni mwa Madhehebu ya Kifiqhi wala madhehebu maalumu katika madhehebu ya elimu ya maneno na mengine, wala kamati kuwa na mtazamo katika ufafanuzi wa Aya za miujiza na mambo ya Akhera na mfano wa hayo.

Kutafsiriwa Qur`ani Tukufu kwa kisomo cha Hafswi wala isipingane na tafsiri za visomo vyengine isipokuwa ikibidi.

Kujiepusha na kazi ya kuunganisha Aya na Sura zenyewe kwa zenyewe.

Kutaja sababu ya kuteremka yaliyosahihi baada ya kutafiti na kutaabika kuifahamu Aya.

Wakati wa kutafsiri ataje Aya kamili ikiwa Aya zimefungamana na maudhui moja, kisha kuchambua maana ya maneno na undani wake kisha kutafsiri maana za Aya kwa mtiririko katika ibara zilizowazi zenye nguvu na kuweka sababu ya kuteremka na yanayozingatiwa kwenye Aya katika hali sahihi.

Kutofika kwenye kufuta Aya isipokuwa kunapokuwa na uzito wa kukutanisha kati ya Aya.

Mwanzoni mwa kila Sura huwekwa kilichofikiwa na kamati katika tafiti zake za Sura kama ni ya Makkah au ya Madina, na kuna nini katika Sura ya Makka kwenye Aya za Madina na kinyume chake.

Tafsiri huwekewa utangulizi katika kuelezea maana ya Qur`ani Tukufu na kubainisha mfumo wake kwa yote yaliyomo miongoni mwa ufundi wake kama vile kulingania kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kama vile utungaji Sharia visa mijadala na mifano ya hayo, kama kamati kutaja mfumo katika kutafsiri kwake ([100]).

Njia ya Tafsiri hiyo:

Baada ya hapo kama tume inavyoona kuweka kanuni maalum kwa njia ambayo hufuatwa katika kutafsiri maana ya Qur`ani Tukufu, tunazielezea kama ifuatavyo:

Kuangalia sababu za kuteremka na kutafsiri kwa maelezo sahihi yaliyopokewa hivyo kutafuta mapokezi yake na kuandika yaliyosahihi na tafsiri pamoja na kubainisha upande wenye nguvu na ule dhaifu.

Kuelezea neno moja moja la Qur`ani Tukufu kilugha na kanuni za muundo wa jumla za Qur`ani Tukufu kibalagha na kuandikwa.

Kuchambua mitazamo ya wafasiri kwa rai na tafsiri sahihi zilizopokewa na kuchagua kinachotafsiri Aya na kubainisha upande wa jibu linalojibiwa na kukubali yaliyokubalika, baada ya yote hayo huundwa tafsiri, na uundaji huu unakuwa kwa njia sahihi ili kuufahamisha uma unaojifunza, usio na sura isiyofahamika.

Mlango wa Tatu: Faida za tafsiri kwa maana hii:

Kwa ufafanuzi huu na hayo maelezo tunaweza kufikia faida zinazorudi kwenye dini yetu tukufu kutokana na hizo tafsiri zinazokubalika, na miongoni mwa hizo faida:

Faida ya Kwanza: Kuondoa uzio wa uzuri wa Qur`ani Tukufu na mema yake kwa yule asiyeweza kuona kwa jicho la lugha ya Kiarabu miongoni mwa Waislamu wasio Waarabu na kuwepesisha ufahamu wao kwa aina hii ya tafsiri ili kuongeza Imani pamoja na Imani zao na kutukuza heshima yao kwa Qur`ani Tukufu na kuimarisha nguvu zao kwenye Qur`ani Tukufu hivyo wakawongoka kwa uwongofu wake na kupasua bahari yake na kusikiliza yaliyoelezewa miongoni mwa malengo mazuri na nguvu katika dalili, na kukuza mafundisho ya kielemu pamoja na kuweka wazi na kwa kina zaidi katika akida, utwahara na  uwongofu katika ibada na msukumo wa nguvu kuelekea kwenye maadili mema na ukemeaji mkali wa machafu na madhambi pamoja na kuleta mabadiliko ya kimiujiza kwa mtu mmoja mmoja na jamii, na uteuzi sahihi wa visa vizuri na kuelezea habari nyingi za mambo ya ghaibu au yasiyonekana pamoja na kuelezea miujiza ya Mwenyezi Mungu aliyompa Mtume wake pamoja na umma wake, na yasiyokuwa hayo ambayo yanafanya kazi ya kuinua nafsi za mwanadamu na kujaza ulimwengu ustaarabu sahihi.

Tunaweza kuelezea faida hizi mbele ya macho yetu pindi tunaposhuhudia mwalimu bora akitoa somo katika masomo ya tafsiri kwa watu wote, akiwawekea wazi maana za Qur`ani Tukufu kwa ustadi mkubwa na kuteremka kwenye usawa wao na kuongea nao na kuteua maana sahihi zaidi na kuhitajika sana na wao, pamoja na kutatua wakati sahihi kile kinachofahamika kwa ujinga wao na kinachowatatiza, kana kwamba kwa somo hili la juu huenda likawapulizia roho ya Qur`ani Tukufu na kuhuhisha maiti zao na kuwatibu wagonjwa wao na kuwaongoza kwenye maendeleo pamoja na kuwafanya wanaamini Kitabu hiki kwa elimu baada ya kuwa wanakiamini kwa Imani inayofanana na uigaji usio na macho au hadithi za watoto.

Jaribio limetuonesha kuwa wengi miongoni mwa hawa ambao wamehisi utukufu wa Qur`ani Tukufu kwa njia ya tafsiri yake wamefikiria katika kuhifadhi kuionesha na kujifunza lugha yake na elimu zake ili wapate kuona wao wenyewe maono yake mazuri na kushiba lishe yake nzuri.

Faida ya Pili: Kuondoa mashaka ambayo yametengenezwa na maadui wa Uislamu na kuyabandika kwenye Qur`ani Tukufu na tafsiri yake kwa uwongo na uzushi, kisha wakatumia hizo shaka kuwapotosha hawa Waislamu ambao hawana ujuzi wa lugha ya Kiarabu katika sura ya fasiri zinazodhaniwa za Qur`ani Tukufu au vitabu vya kielimu na kihistoria kwa wanafunzi au vituo vya elimu au masomo na mihadhara au magazeti na majarida ya umma na binafsi.

Faida ya Tatu: Kuelimisha wasio Waislamu miongoni mwa wageni ukweli wa Uislamu na mafunzo yake hasa katika zama hizi zenye kusimama kwenye propaganda na kati ya moto wa vita hivi ambavyo moto wake umewashwa na watu wa mila zengine mpaka wakapotosha haki au ikakaribia kupotea ndani ya giza batili na kupungua sauti ya Uislamu au ikakaribia kupungua kati ya sauti na kelele za madhehebu mengine ya sera kali na dini potofu.

Faida ya Nne: Kuondoa viziwizi ambavyo vimewekwa na waovu wenye vitimbi kati ya Uislamu na wapenzi wa haki katika umma tafauti, na vizuizi hivi kwa sehemu nyingi vimejikita kwenye uwongo waliouzusha, wakati mwengine kwenye Uislamu na wakati mwengine kwa Nabii wa Uislamu na mara nyingi uwongo huu wanaunasibisha kwenye Qur`ani Tukufu na tafsiri yake na kwenye historia ya Mtume na mwenendo wake kisha wanaubambikiza katika kile wanachodhania tafsiri za Qur`ani Tukufu au katika wanayosoma watu na kusikia kuhusu Uislamu kwa njia zingine, pindi sisi tunapo tafsiri Qur`ani Tukufu au kuibainisha kwa kutumia lugha zengine pamoja na kuchunga masharti ya ubainifu na masharti ya tafsiri na kuchunga kikamilifu kuondoa mashaka na mambo batili katika kila mnasaba bila shaka kutaondoa msingi huo ambao wameusimamisha kutokana na uzushi na mambo batili na kuondoa vizuizi kupitia wanaotafuta haki na wapenzi wake kutoka kila upande.

Faida ya Tano: Kujitoa kwenye dhima ya wajibu wa kufikisha Qur`ani Tukufu kwa maneno yake na maana zake kwani tafsiri hii imekusanya kati ya Maandiko Matakatifu kwa maneno yake na maandishi yake ya Kiarabu na kati ya maana za Qur`ani Tukufu kwa ufahamu wa mtafsiri na sherehe yake kwa lugha ya kigeni. Imamu Al-Suyuutwy na Ibn Batwaal pamoja na Al-Hafidhu Ibn Hajar na wengine miongoni mwa Wanachuoni wamesema: Kwa hakika ufunuo au Wahyi ni lazima ufikishwe lakini upo sehemu mbili: Sehemu ufikishaji wake kwa mifumo yake na maana zake ni lazima nayo ni Qur`ani Tukufu, na sehemu inafaa kufikisha maana zake pasi ya maneno yake nayo ni isiyokuwa Qurani na kwa sababu hiyo hukamilika ufikishaji ([101]).

Mlango wa Nne: Kuondoa shaka kuhusu tafsiri hii:

Wanaweza kuonesha baadhi ya wenye wivu juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kuongozwa na chuki ya ya dini yake kuibuka  ili kupinga, pia tunayoyaandika  katika maelezo tunayoyaona katikafaida za tafsiri kwa kufuata vigezo vyake na masharti yake yaliyoelezwa, na wao katika hayo wana shaka nyingi lazima kuzielezea na kuziondoa:

Shaka ya Kwanza na jibu lake:

Wanasema kuwa wafasiri wa kimaana wanalazimika kufsiri tafsiri ya neno kwa neno isiyokubalika, nayo ni tafsiri ya kila kinachopelekea kayika kila kundi la tafsiri katika Aya, kwa sababu tafsiri ya maelezo ni lazima muelezaji aifahamu yeye kwanza kisha kuifahamisha, na kwa vile ikiwa tafsiri itatafsiriwa pasi na Aya tafsiri hiyo inakuwa si yenye kufikia makusudio kwa kukosekana muunganiko na yaliyokabla yake.

Hilo limetupelekea kuweka sharti la maneno asili kutokuwa yanatokana kati ya sifa za tafsiri kwa lugha ya kigeni, bali tumesema tafsiri inagawanyika vigawanyo mbalimbali na mwanzoni mwa vigawanyo hivi na huelekezwa Aya au aya nyingi katika kila kundi katika vigawanyo hivi kwa maneno au maandishi ya Kiarabu, ikiwa tunatafsiri hii inatafsiriwa kwa kundi la ndugu zetu Waislamu, kisha huashiriwa katika tafsiri yake na kusemwa:

Maana ya Aya hii au Aya hizi ni hivi, au kusemwa: Aya imepewa nambari fulani kutoka Sura fulani maana yake ni hivi na vile kwa maelezo yaliyokosa maneno ya asili na tafsiri yake ni tafsiri ya kawaida, inatosha katika kuunganisha mfasiri kwa maelezo yake kwa namna yeyote miongoni mwa sura za muunganiko nayo hapa kwanza imetajwa kwa neno lake na maandishi yake kwa Kiarabu kisha ikaashiriwa kwa jina la ishara au kuelezewa nambari yake kutoka Sura na jina la Sura yake kwenye Qur`ani Tukufu.

Ama muunganiko ni rahisi kuchunga maelewano kati ya sentensi za tafsiri zenyewe kwa zenyewe katika kila kikundi kwenye vikundi vyake zake, ama maelewano ya hizi vikindi hivi vyote vyenyewe kwa vyenyewe ambapo hutengeneza neno moja lenye kushikana kama vile mkusanyiko mmoja ni kitu kisichowekewa sharti na yeyote katika tafsiri, wala kutudhuru kwa kukosekana kwake kitu  chochote, madamu tafsiri ni maneno yaliyotafauti katika makundi yalitawanyika  si neno moja katika kundi  moja, ama uwiano wa Aya zenyewe kwa zinyewe ni jambo lisiloepukana lakini si lazima kuelezea tafsiri hii wala tafsiri zingine.

Shaka ya Pili na jibu lake:

Wanasema kuwa tafsiri ya Qur`ani Tukufu kawaida inakusanya namna ya utamkaji wa maneno yak,e maana zake, hukumu zake moja moja na za kimuundo, pamoja na maana zake ambazo zinabebwa na hali ya muundo na tafauti za kimaana wakati wa kusimama kwenye baadhi ya maneno na kuanza yale yanayofuata na wakati wa kuunganisha neno la kwanza kwa neno la pili, na kunajumuisha pia  kujua hadithi sababu inafafanua Qur`ani Tukufu,  na kauli za Maswahaba pamoja na kauli za Maimamu wenye kufanya jitihada na yasiyokuwa hayo, na tafsiri ya mfano huu pamoja na kukamilika ni jambo gumu.

Hilo linapelekea kuwa kukamilika mambo yaliyotajwa hakujashartishwa na yeyote katika asili ya tafsiri ya Kiarabu, na ni wazi kutoweka sharti hilo katika tafsiri yake nayo ni sura yake, ni vipi wakati tumefahamu kuwa tafsiri ni ufafanuzi hata kwa njia moja  tu, na mfasiri anachotakiwa kuwa mwenye hekima anafahamu hali za anaowatafsiria kadiri ya uwezo wake, hivyo tafsiri yake inakusanya yale wanayoyahitaji na kuacha yale yasiyofikiwa na akili zao, kinyume na hivyo basi itakuwa ni fitina kwao na huenda hilo ni siri katika siri za aina za tafsiri za Kiarabu ambazo tunazo miongoni mwa tafsiri fupi za kati na ndefu, na kati ya tafsiri ya mapokeo na tafsiri kwa kutumia akili na tafsiri ya maana kwa upande wa kibalagha na maana nyengine kwa upande wa kisarufi, na maana ya tatu kwa upande wa maneno, na maana ya nne kwa upande wa Kifiqhi na zisizokuwa hizo, ikiwa hizi zipo mbele ya macho yetu katika tafsiri za Kiarabu basi ni vipi tunapinga pindi inapotokea mfano wake katika tafsiri kwa lugha ya kigeni.

Shaka ya Tatu na jibu lake:

Wanasema hakuna haja ya tafsiri za ufafanuzi kwa lugha isiyo ya Kiarabu wala tafsiri ya maana yeyote ya Qur`ani Tukufu kutokana na kuwezekana kuachana nazo zote mbili kwa tafsiri ya mafunzo ya Uislamu na uongofu wake.

Na hilo limetusukuma sisi kuelezea upande wa uhitaji katika faida ambazo tumezitaja hapo nyuma kisha tafsiri ya ufafanuzi wa Qur`ani Tukufu na tafsiri ya Qur`ani Tukufu kwa lugha ya kigeni zote mbili ni mfano wa tafsiri ya mafundisho ya Uislamu na uwongofu wake, kwani yote ni maarifa ya kidini na yote ni katika maneno ya watu si maneno ya muujiza ya Mungu, kwa hakika mumepitisha tafsiri ya mafundisho ya Uislamu na uwongofu wake basi pitisheni pia tafsiri ya ufafanuzi na kimaana kwa lugha ya kigeni kwa sababu kilichofaa katika moja ya vifanano viwili kinafaa moja kwa moja kwa kifanano kingine, kisha jumbe zinazozungumza kuhusu Uislamu na mafundisho yake kwa lugha za kigeni zinaweza kuwa muhimu na lazima katika baadhi ya hali na minasaba lakini haiwezi kujitenga na tafsiri hii ambayo sisi hivi sasa tunaelezea faida ambazo tumezisherehesha hivi karibuni, uwepo wake – pamoja  na faida zake – kunabakia ni shahidi wa kweli juu ya ubatili wa yaliyokuja katika tafsiri  za kimakosa jambo linapolekea wepesi kwa watu wenye sifa na wanaotafuta  ukweli kuhukumu tafsiri hizo kwenye yaliyokuja katika tafsiri zetu hasa hasa pindi zinapotolewa na Taasisi ya Kiislamu inayokubalika kama vile - Al-Azhar Al-Sharif – na kuelezewa katika kila munasaba kama tulivyosema ufafanuzi wa yanayopotosha kwenye tafsiri potofu.

Huongezewa katika haya kuwa Muislamu asie Muarabu hutumia tafsiri hizo kwenye kufahamu na kuzingatia Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa Aya yeyote ya Sura yeyote anayotaka na ujumbe uliomo ni ngumu kuwezesha yote hayo ([102]), na imetangulia kuelezwa kauli ya Al-Zamakhshary wakati wa tafsiri yake ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa watu wake ili apate kuwabainishia} Ibrahimu: 4. Ikiwa utasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu hakupelekwa kwa Waarabu tu peke yao bali amepelekwa kwa watu wote:

{Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote} Al-Aaraaf:  158. Bali ni kwa majini na watu nao wakiwa wanatumia lugha tafauti, ikiwa kwa Waarabu si hoja basi kwa wengine ni hoja, nikasema: Haiwezi kuachana ima iteremke kwa lugha zote au lugha moja wapo kwani hakuna haja ya kuteremka kwa lugha zote kwa sababu tafsiri huchukuwa nafasi ya hizo lugha na inatosha kurefusha, na kubaki kuteremka kwa lugha moja hivyo ikawa lugha bora ni lugha ya watu wa Mtume S.A.W kwa sababu wao ni watu wa karibu zaidi kwake pindi wanapofahamu kutoka kwake na wakabainishiwa na kunukuliwa kutoka kwao pamoja na kueneza basi tafsiri inasimama kubainisha na kufahamisha, kama hali inavyoonekana na kushuhudiwa tafsiri kuchukuwa nafasi kwa kila taifa katika mataifa yasio ya Kiarabu, pamoja na hayo kuwepo makubaliano na watu wa maeneo na nchi hizo zilizombali na na mataifa mbalimbali vizazi tafauti juu ya kitabu kimoja na juhudi zao katika kujifunza maneno yake na kujifunza maana zake na yanayotokana na hayo miongoni mwa faida nyingi na tabu nyingi za nafsi kutokana na kujikurubisha utiifu mwingi na thawabu nyingi, na kwa vile ipo mbali sana na upotoshaji kubadilisha na kuwa salaam zaidi na mvutano na tafauti, na kwa kuwa lau ingeteremka kwa lugha za wote pamoja na uwingi wake na ikawa inajitegemea na sifa ya muujiza katika lugha moja na Mtume S.A.W Muarabu akazungumza na kila taifa au umma kwa lugha yao kama alivyozungumza na umma wake ambao Yeye anatokana nao akiwasomea muujiza basi hilo lingekuwa jambo la karibu sana na kukimbiliwa ([103]). 

Hitimisho:

 Tumemaliza utafiti huu na kufikia ukweli muhimu nina imani kuwa wenyewe ukisimamiwa kwa uadilifu basi utaondoa tafauti za wenye kutafautiana kwenye maudhui hii, au kufanya tafauti za kimaneno zisizoweza  kuleta na kuibua mijadala na sehemu ya mvutano:

Tafsiri ya maana ya Qur`ani Tukufu kwa lugha ya kigeni ni sawa sawa na tafsiri ya ufafanuzi ya Kiarabu ya Qur`ani Tukufu.

Tafsiri ya Qur`ani Tukufu ya neno kwa neno kwa aina zake lazima ifikie utimilifu wa kimaana zote za Qur`ani Tukufu na makusudio yake ni sawa sawa ikiwa tafsiri ya neno kwa neno la mfano au si la mfano.

Tafsiri za Qur`ani Tukufu zinashrikiana kimaneno kati ya maana nyingi zipo nyingi: Miongoni mwake zipo zilizokubaliwa kufaa kwake nazo ni:

Tafsiri kwa maana ya kufikisha maneno yake, na tafsiri kwa maana ya ufafanuzi kwa lugha ya Kiarabu, na miongoni mwazo: Ni zilizo lazima kukubaliana kutokubalika kwake nayo: Tafsiri kwa maana ya kunukuliwa kwenye lugha ya kigeni pamoja na kutimilika maana zake zote na makusudio yake, miongoni mwazo: Zipo zenye tafauti ndani yake lakini kuna dalili nyingi za kufaa kwake, nayo: Tafsiri kwa maana ya tafsiri ya maana zake au tafsiri yake kwa lugha ya kigeni pamoja na kutimia masharti ya tafsiri na ufafanuzi, pamoja na pingamizi ambazo tumezionesha na kuoneshwa na kamati ya Al-Azhar, hivyo ninazingatia kuwa tatizo linaweza kuondoka na tafauti ikapotea, watu waadilifu wanakutana kwenye neno moja lilo sawa ili tuungane kwa pamoja kwenye mambo yenye manufaa kwa nchi na waja, na kusimama na wajibu imara wa dini hii madhubuti, na wajibu wa kulingania walimwengu.

Shukurani zote mwanzo na mwisho anastahiki kushukuriwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

 

[1] Sehmu ya utangulizi wa Imamu Al-Ghazaly kwenye kitabu chake cha Al-Maani “Utenganisho kati ya Uislamu na Zindiki” ukurasa wa 13, uhakiki umefanywa na Mahmoud Bijou chapa ya 1413H,

[2] As-Sarkhasy: Kitabu cha Al-Mabsuut 1/37 chapa ya 1 ya Beiruti na kuchapishwa na Maktaba ya Saadah. An-Nawawi: Kitabu cha Al-Majmuu sherehe ya kitabu cha Al-Muhadhabu 3/380, sikuwa nakusudia kuleta hukumu kwenye mapokezi haya bali nimeorodhesha tu kisha hukumu itakuja kwenye sehemu yake.

[3] Kitabu cha Historia ya Bukhara cha Tarshakhy kimefasiriwa na Dr. Amin AbdulMajiid na mwenzake ukurasa wa 74 chapa ya 1 ya Dar Al-Maarif.

[4] Jarida la tafiti za Kiislamu juzuu ya 26 ukurasa wa 231.

[5] Kitabu cha Al-Bayaan wa Tabyiin juzuu ya 1 ukurasa wa 368, uhakiki umefanywa na Abdulsalam Harun chapa ya 7 ya mwaka 1998.

[6] Hapa nimenufaika na mengi yaliyokuja kwenye makala ya Sayyid Ahmad Abulfadhli kupitia jarida la tafiti za Kiislamu juzuu ya 30 ukurasa wa 258: 268.

[7] Unaweza rejea maelezo ya Sheikh Hussein Makhlour ambapo amezungumzia tafasiri zao katika utafiti wake ndani ya ukurasa wa 11: 12.

[8] Dr. Najda Ramadhani: Tafsiri ya Qurani na athari zake katika maana zake ukurasa wa 132.

[9] Muhammad Rashidi Ridha: Tafsiri ya Al-Manaal 9/321 – 323.

[10] Dr. Najdat Ramadhani: Tafsiri ya Qurani na athari yake katika maana zake, ukurasa wa 134.

[11] Ulitolea mwaka 1355 – 1936, inaonesha kuwa ni ndani ya wakati huo huo ambao zilichapishwa tena tafiti mbili za Sheikh Al-Maraghy na mwalimu Faridi Wajdy kama ambatisho la jaribu la Al-Azhar.

[12] Hayo yameelezwa na Sheikh Mustafa Swabry katika kitabu chake “Masuala ya tafasiri ya Qurani” ukurasa wa 41. Na mwalimu Ibrahim Al-Jabaly katika makala yake kwenye jarida la Al-Azhar toleo la 3 ukurasa wa 59, kwa masikitiko makubwa hazijatufikia hizo makala kwa sababu haikuwa wepesi kuchapisha ndani ya kitabu.

[13] Ilichapishwa mwkaa 1345H.

[14] Tafsiri ya Al-Manal 314/9 – 363.

[15] Kilichapishwa mwaka 1350H – 1932.

[16] Kilitolewa chapa ya pili mwaka 1355H.

[17] Kilitolewa mwaka 1355 – 1936.

[18] Kilichapishwa mwaka 1355H.

[19] Kilitolewa mwaka 1355H.

[20] Kitabu ambacho kilichapishwa kwenye kituo cha uchapishaji cha Salafi mwaka 1351H

[21] Dr.Ramadhani Abdultawwab: Tafsiri ya Qurani kati ya upingaji na kukubali, makala ndani ya jarida la Risala chapa ya 9, 10 – 1389H ukurasa wa 44 – 50.

[22] Ibn Fatiba: kitabu cha Taawil Mushkil Al-Qutani, ukurasa wa 12 uhakiki umefanywa na Sayyid Swaqru chapa ya 2 ya Dar Atturathi 1393 kimechapwa na chapa ya Al-Halaby.

[23] Al-Shaatwibi: Al-Muwafaqaat 64/2 uhakiki umefanywa na Sheikh Darraz chapa ya 2 ya Dar Al-Maarifa – Beiruti 1395 na kuchapishwa na Mkataba ya Kibiashara.

[24] Othman Swafi: Qurani Tukufu ubunifu wa tafsiri ya maneno yake na maana zake, ukurasa wa 38 chapa ya 1 maktaba ya Kiislamu.

[25] Al-Swahibiy katika fiqhi ya lugha na siri ya Kiarabu ukurasa wa 4.

[26] Othman Al-Swafi: Qurani Tukufu ubunifu wa tafsiri ya maneno yake, ukurasa 42

[27] Ibn Fatibah: kitabu cha Taawiil Mushkal Al-Qurani, ukurasa wa 12.

[28] Sehemu ya tafiti ya Sheikh Muhammad Ibn Salah Ibn Abdillah katika kongamano la Mfalme Fahdi la uchapishaji Msahafu Mtakatifu mwaka 1422H.

[29] Ismail Al-Jawhary: Kitabu cha Al-Swahah 5/1928.

[30] Ibn Mandhuur: Kamusi ya Lisaanul Arabi, 12/66, kwa maana anayefanya kazi ya kutafsiri, ama tafsiri yenyewe huwingi wake na tafsiri, na hii kinyume na maelezo yaliyoenea kwenye lugha za watu miongoni mwa matumizi ya uwingi wa neno tafsiri,

[31] Amesema kwenye sherehe ya kamusi: Nimeona pembezoni mwa kitabu – anakusudia kamusi – neno limeandikwa mtafsiri “Turjamani” kwa herufi ya jiim kuwa na silabi ya fatha lakini halijasikika kwa Wanachuoni kwa kuthibitishwa.

[32] Al-Muujamu Al-Waswitw 1/83.

[33] Marejeo yaliyopita.

[34] Kitabu cha Kauli Sadiid katika hukumu ya tafsiri ya Qurani Tukufu ya Mustafa Al-Shatwir ukurasa wa 10.

[35] Kitabu q111cha Manaahil Al-Urfan 2/91 uhakiki umefanywa na Fawazi Zumarl chapa ya kwanza ya Dar Al-Kitabu Al-Araby ya mwaka 1415H.

[36] Naye ni Sheikh Muhammad Hasanain Makhluf katika tafiti yake “Hukumu za tafsiri ya Qurani Tukufu” na Muhammad Mustafa Al-Shaatwir katika kitabu chake cha “Al-Qaulu Al-Sadiid” na wasiokuwa hao, na akachukuwa kutoka kwao Dr. Muhammad Ibn Salah Ibn Abdillah katika tafiti yake kuhusu masuala haya ambayo aliyafikisha kwenye kongamano ambalo liliandaliwa na Taasisi ya Mfalme Fahdi ya uchapishaji Msafahamu Mtakatifu mwaka 1422H, baadhi wakaongeza sehemu nyengine nayo ni tafsiri ufafanuzi, miongoni mwao wapo wenye kuona kuwa tafsiri ya maana ya ni sehemu inayojitegemea.

[37] Al-Zarkany: Kitabu cha Manahli Al-Urfaan 2/93.

[38] Al-Zarkany: Kitabu cha Manahli Al-Urfaan 2/93

[39] Al-Zarkany: Kitabu cha Manahli Al-Urfaan 2/93.

[40] Kitabu cha Hukumu ya Tafsiri ya Qurani cha Sheikh Makhlufu ukurasa wa 9.

[41] Angalia maneno ya Sheikh Hasanaini Makhluf – kuhusu hilo kwenye utafiti wake ukurasa wa 10.

[42] Angalia  tafiti ya Sheikh Hasanaini Makhluf ya hukumu ya tafsiri ya Qur`ani Tukufu ukurasa wa 4.

[43] Angalia  tafiti ya Sheikh Hasanaini Makhluf ya hukumu ya tafsiri ya Qur`ani Tukufu ukurasa wa 4.

[44] Kitabu cha Manahili Al-Irfaan cha Zarqawi juzuu ya 2 ukurasa wa 92 – 93.

[45] Ni kaitka maneno ya Sheikh Mahmoud Abu Dakika kwenye jarida la Al-Azhar la mwaka wa tatu ukurasa wa 31, na kunukuliwa na Al-Zarkany katika kitabu cha Al-Manahili juzuu ya 2 ukurasa wa 98.

[46] Somo hili ni sehemu ya kwenye kitabu cha Manahili Al-Irfaan juzuu ya 2 ukurasa 100: 105.

[47] Angalia makala ya Sheikh Ibrahim Al-Jibliy kwenye jarida la Al-Azhar toleo la 3 ukurasa wa 60: 61.

[48] Sahih Al-Tirmidhy

[49] Angalia kitabu cha Al-Hukmu Al-Atwaiyah: Hekima ya arobani na saba, ukurasa wa 54 pamoja na sherehe yake na Ibn Ibadi chapa

ya kwanza ya 1 ya Al-Ahraam 1408 – 1988.

[50] Miongoni mwa waliosema kutowezekana kwake ni pamoja na Sheikh Bakhiit Al-Mutwiii aliyesema sehemu mbalimbali katika tafiti zake kwa mfano angalia ukurasa wa 58, vile vile ameyasema hayo Sheikh Hasanain Makhluf katika utafiti wake ukurasa wa 8, na akasema kuwa hakuna tafauti katika hilo ukurasa wa 9, vile vile Sheikh Al-Juzairy katika tafiti yake ndani ya kitabu cha Ahsanul-Bayaan ukurasa wa 6.

[52]  Bali ni maelezo ya Sheikh Bakhiit ikiwa ni kubadili Qurani na jibu toshelezi kwa urefu juu ya hilo ndani ya kitabu chake “Hojjatullah Alaa Khaliiqatih” angalia ukurasa wa 31: 38.

[53] Angalia kitabu cha Al-Risaala ukurasa wa 48 uhakiki umefanywa na Sheikh Ahmad Shaakir, chapa ya Daru At-Turaathi.

[54] Manahilu Al-Urfaan juzuu ya 2 ukurasa wa 116: 121.

[55] Utafiti katika tafsiri ya Qurani ukurasa wa 27.

[56] Marejeo yaliyopita ukurasa wa 31.

[57] Hayo ni yamesemwa na kundi la Wanachuoni, miongoni mwao ni Sheikh Makhluf katika utafiti wake ukurasa wa 2. Kitbu cha Al-Jaamii Swahiih cha Imamu Bukhary juzuu ya 6 ukurasa wa 2742 na uhakiki umefanywana Mustafa Al-Baa chapa ya 3 ya Dar Ibn Kathiir Damascus 1407.

[59] Kitabu cha Al-Mabsuutw juzuu ya 1 ukurasa wa 37 na kitabu cha Haashiyatu Shalabi juzuu ya 1 ukurasa wa 111, na kitabu cha Fatawa Al-Ghayaathiyah ukurasa wa 27 na akachukuwa kutoka kauli sahihi ukurasa wa 69.

[60] Kitabu cha Tabyiin Al-Hakaaik na Haashiya yake juzuu ya 1 ukurasa wa 111.

[61] Kitabu cha Fakhru Raazi katika tafsiri yake juzuu ya 1 ukurasa wa 108, na angalia kitabu cha Al-Qaulu Sadiid ukurasa wa 67.

[62] Kitabu cha Masuala ya tafsiri cha Sheikh Mustwafa Swabry ukurasa wa 32, 33.

[63] Ni katika neno la Sheikh Mahmoud Abu Dakika Al-Hanafi kilichapishwa kwenye jarida la Al-Azhar la mwaka wa tatu ukurasa wa 32: 35, naye amesema kwa mfano wake Sheikh Bakhiit katika utafiti uliopita ukurasa wa 42.

[64] Kitabu cha Al-Mabsuutw 1/99 na kitabu cha Al-Muhiitwul-Burhaany cha Al-Burhaan Al-Diini Ibn Maarah 1/439.

[65] Kitabu cha Al-Majmou 3/375: 380.

[66] Al-Swaahibi katika kitabu cha Fiqhi lugha na siri ya Kiarabu 1/10.

[67] Kitabu cha Al-Bahru Al-Muhitw juzuu ya kwanza ukurasa wa 361: 362, uhakiki umefanywa na Dr. Muhammad Taamir chapa ya 1 Daru Al-Kutubi Al-Alamiah 1421.

[68] Al-Muwafaqatu cha Al-Shatwibi uhakiki umefanywa na Sheikh Daraz juzuu ya 2 ukurasa wa 6: 68.

[69] Angalia kitabu cha Al-Murafiqaat juzuu ya 2 ukurasa wa 103.

[70] Kitabu cha Manaahil Al-Urfaan juzuu ya 2 ukurasa wa 131.

[71] Kitabu cha Manahili Al-Urfaan juzuu ya 2 ukurasa wa 121: 123.

[72] Kitabu kilichotangulia ukurasa wa 124: 125.

[73] Ambapo anakuwa kuwa tafsiri ya maana kwa uhakika ni tafsiri ya Qurani ya neno kwa neno, angalia utafiti wake wa Qurani Tukufu lengo la kisiasa na fitina katika dini ukurasa wa 22: 25.

[74] Ambapo wengi miongoni mwa waliopinga tafsiri ya neno kwa neno kwa aina zake zote wamepitisha tafsiri ya aina hii kama vile Sheikh Hasanain Makhluof na Sheikh Mustafa Swabriy na wengine wasio kuwa hao.

[75] Sheikh Al-Maraghy ukurasa wa 25 kitabu cha Fathul-Qadiir juzuu ya 2 ukurasa wa 47.

[76] Utafiti katika tafsiri ya Qurani ya Sheikh Al-Maraghy ukurasa wa 25.

[77] Angalieni katika kitabu cha Quli Al-Sadiid ukurasa wa 143: 150.

[78] Kitabu cha Al-Bahru Al-Muhiitw juzuu ya 1 ukurasa wa 474 chapa ya pili ya Wizara ya Waqfu nchini Kuweit mwaka 1413 – 1992 pasi ya kauli yake “Kwa sababu tafsiri…..nk” kwani maelezo haya ya ziada yameletwa na Sheikh Hassanain Makhlouf katika utafiti wake ukurasa wa 38: 39.

[79] Kitabu cha Fat’hul-Baary juzuu ya 9 ukurasa wa 10 mlango wa ubora wa Qurani chapa ya Dar Al-Maarifa Beiruti.

[80] Kitabu cha Al-Furuu juzuu ya 2 ukurasa wa 177 kimefanyiwa uhakiki na Dr. Abdalla Al-Turky chapa ya 1 ukurasa wa 317: 318 Taasisi ya Al-Risalah 1424.

[81] Kitabu cha Kashafu Al-Qannai kwa matini ya Al-Qannai Al-Baihuty juzuu ya 1 ukarasa wa 317: 318, uhakiki umefanywa na Muhammad Amin Al-Dhawi chapa ya 1 ya Ulimwengu wa vitabu 1417.

[82] Kitabu cha Al-Jawabu Al-Swahihi juzuu ya 2 ukurasa wa 54: 56 chapa ya 2 ya Daru Al-Aswimah 1419H.

[83] Kitabu kilichopita 2/69.

[84] Kitabu kilichopita 2/62.

[85] Ufupisho wetu kwenye kitabu cha Al-Qaulu Al-Sadiid ukurasa wa 152: 153.

[86] Ni uwingi wa mtafsiri.

[87] Kitabu cha Al-Kashafu juzuu ya 3 ukurasa wa 362, uhakiki umefanywa na Adil Abdulmaujuud chapa ya 1 ya 1418.

[88] Kitabu cha Al-Qaulusadiid ukurasa wa 138: 139.

[89] Angalia kitabu cha Al-Burhan katika msingi wa Fiqhi kitabu cha Imamu Al-Haramaini juzu ya 1 ukurasa wa 421, uhakiki umefanywa na Dr. AbdulAdhiim Al-Diib chapa ya 4 ya Darul – Wafaau 1418.

[90] Kitabu cha Hojjatullah alaa khaliiqatih ukurasa wa 50:  52.

[91] Kitabu cha Mas’alatu tarjamatul-Qurani ukurasa wa 8 chapa ya 1 mwaka 1351.

[92] Marejeo yaliyopita ukurasa wa 9.

[93] Kitabu cha Al-Qaulu-Al-Sadiid ukurasa wa 104.

[94] Kitabu cha Ahsanul-Bayaani ukurasa wa 6.

[95] Chanzo kilichopita ukurasa wa 34.

[96] Chonzo kilichopita ukurasa wa 39.

[97] Kitabu cha Al-Qaulu Al-Sadiid ukurasa wa 105.

[98] Kama yalivyokuja hayo katika jarida la Al-Azhar la mwaka wa sabab ukurasa wa 45.

[99] Manaahilu Al-Urfaan juzuu ya 2 ukurasa wa 108: 109.

[100] Jarida la Al-Azhar la mwaka wa saba ukurasa wa 648: 649 mwaka 1355.

[101] Kitabu cha Manahilu Al-Urfaan juzuu ya 2 ukurasa wa 110: 111.

[102] Maerejo yaliyopita ukurasa wa 112: 113.

[103] Angalia kitabu cha Al-Kasshaf juzuu ya 3 ukurasa wa 362.

Share this:

Related Fatwas